YAJUE MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE
Kila
ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa
mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha
mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu
No 1: NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili
kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea
mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu.
Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa
huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo
dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.
No 2: GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili
kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa
kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya
mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
NO 3: MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili
kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara
nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula
(crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea
wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
NO 4: NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa
huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara
waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au
vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.
No 5 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili
kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za uso, kichwa na macho, ute
mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.
No 6: FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.
NO 7 COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.
NO 8: FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.
NO 9 MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
_Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba:
Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa
wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa
umezining'iniza juu kidogo.
Kama
utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani
watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina
sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi
......................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment