script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Related image


Kasuku ni ndege wapendwao na watu wengi sana hasa maeneo ya mjini. Ndege huyu hupendwa kwa sababu ana kasumba ya kuwa na rangi nzuri za kuvutia, achilia mbali rangi lakini pia ndege huyu ana sauti ambayo huwa haichoshi masikioni mwa watu, pia ni kivutio cha wengi.
Lakini licha ya kuwa na sifa hizo, ndege huyu amekuwaa na hulka moja ya kujinyofoa manyoa. Hii nikutoka na sababu mbalimbalia ambazo nitazieleza hapa na njia za kujikinga ili kasuku wako asinyofoke manyoa.
Kwa kuanza tuangalie sababu za kunyofoka kwa manyoa hayo


1. Lishe duni, upweke na kukosa matunzo ya jumla

2.  Kama atakuwa anatafuna kucha zako unapomshika

3. Viroboto au utitiri

4. Maambukizi ya bakteria au fangasi

5. Banda dogo sana

6. Lishe yenye vitamini A kwa wingi zaidi


Nini kifanyike ili kuzuia tabia hii ya kunyofoka kwa manyoya
1. Hakikisha ndege wako anapata mlo kamili, unaweza kununua chakula kwenye maduka au ukachanganya mwenyewe baada ya kupata utaalam, apate matunzo yote muhimu na pia asiwe mwenyewe ni vizuri ukafuga dume na jike.

2.  Kama unatabia ya kumshika ndege wako hakikisha unavaa kitu cha kukinga asiweze kula kucha zako kama vile gloves

3. Viroboto na uttiiri vidhibitiwe kwa kutumia dawa maalum kama vile akheri powder

4.  Maambukizi ya bakteria na fangasi yadhibitiwe mara moja kwa kutumia dawa kama ancobal

5. Ndege wako anaishi kwenye banda lenye ukubwa wa kutosha

6.  Punguza vyakula vyenye vitamini A kwa wingi kama vile karoti


.............................................................................................

0 comments:

 
Top