Watu wengi huwa tunatumia asali
pasipo kujua wametokana na asali wa aina gani, hivyo kila asali ambayo unaitumia
kuanzia leo ni lazima ujue wanatakona na nyuki wa aina gani. Asali za NYUKI
WAKUBWA na WADOGO zina tofautiana katika mambo kadhaa
na hvyo ni muhimu kujua tofauti hizo kabla hujanunua ili kua na uhakika.
NYUKI WADOGO
1. Ni nyepesi zaidi kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24
2. Ina ladha ya UCHACHU ingawa ni tamu sana.
3. Mara nyingi ina rangi ya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoenda kwenye
WEUSI
NYUKI WAKUBWA
1. Ni nzito kuliko ya nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji
kuanzia asilimia 17 hadi 20.
2. Ni tamu moja kwa moja bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki
wadogo
3. Ina rangi nyingi kuanzia NYEUPE, NYANO, KAHAWIA ILIYOPOA,
KAHAWIA ILIYOKOZA n.k
Hizo
ni tofauti za muhimu kuzijua kwani zitakuwezesha kupata asali unayoitaka na
kuepuka kuibiwa
.........................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment