MBWA ni mnyama anayethaminiwa na wengi na hususan hufugwa kwa minajili ya kuimarisha usalama katika makazi ya wafugaji.
Mnyama huyu huaminika ndiye mwaminifu zaidi kati ya wanyama wote wanaofugwa nyumbani.
Kuna wale wanaomfuga pia kwa sababu humchukulia kama 'kipenzi' chao (pet).
Je, wajua mbwa ni kitega uchumi kwa baadhi ya wanaomfuga? Mnyama huyu ametajirisha baadhi ya wafugaji wanaomthamini.
Mahitaji ya kufuga mbwa ni haba mno ikilinganishwa na wanyama wengine kama vile mbuzi ama ng'ombe
Mbwa hawa hufugwa na kutunzwa kwa msingi wa malengo matatu, 1.wale wa kunusa (sneaver dogs),
2.wa kulinda/kuhifadhi usalama (guard dogs) na
3.wa kuongoza (guide dogs) maafisa wa usalama.
2.wa kulinda/kuhifadhi usalama (guard dogs) na
3.wa kuongoza (guide dogs) maafisa wa usalama.
Mbwa huzaa mara mbili kwa mwaka ambapo hubeba ujauzito kwa kipindi cha siku 63 (miezi 2).
Kwa kawaida mbwa mmoja huzaa kati ya vilebu/pappies 8 - 12.
Lishe
Anachohitaji mbwa ni lishe bora pekee huku magonjwa yanayomwathiri yakiwa finyu kinyume na wanyama wengine.
"Lishe
ni kiungo muhimu kwa mbwa, hulishwa kwa chakula anachokula binadamu
japo kuna vyakula vingine vinavyonunuliwa kwenye maduka,"
Vilebu
hulishwa mara mbili kwa siku huku walionenepa na kukomaa wakilishwa
mara moja kwa siku. Hulishwa kwa nyama, mifupa iliyosagwa, chakula
halisi cha mbwa kinachojulikana kama 'Top dog', punje za mchele, samaki
aina ya 'omena' ama masalia ya chakula.
"Chakula
chake huchanganywa na vitamini mbalimbali (multi-vitamin) ili kuboresha
afya yake, manyoya, meno na mifupa iwe dhabiti na yenye nguvu. Vitamini
hivo ni: CAL-VITAMAX yenye madini ya Calcium,"
Ikumbukwe
usafi wa makazi ya mbwa ni jambo la muhimu kuzingatia kwa minajili ya
kufurusha wadudu kama vile viroboto na kupambana na magonjwa
yanayotokana na uchafu.
"Makazi ya mbwa
yanafaa kusafishwa na kupuliziwa kwa dawa aina ya dudu dust kila siku
ili kufurusha viroboto. Kisha mbwa waoshwe kwa dawa aina ya Dudu Krin
mara moja kwa wiki
Magonjwa
Magonjwa
kwa mbwa ni jambo linalofaa kutiliwa maanani wakati wa malezi yake.
Magonjwa kama vile: Canine Distemper, Canine Herpatitis, Lep Tospirosis,
Parvo Virus (ugonjwa wa kuendesha damu), Rabbies (Kichaa) ndio huathiri
mbwa.
"Ili kuepuka athari za magonjwa haya
hupewa aina tatu ya chanjo kwa mwaka. Kibwa azaliwapo na kufikisha wiki 6
hudungwa chanjo ya Parvo Virus, akiwa na umri wa miezi 3 hudungwa ya
DHLP na anapohitimu miezi 4 hudungwa sindano ya chanjo ya Kichaa
(Rabbies)," aeleza Dkt/Officer Mshindo Vet
Mbali
na chanjo hiyo, pia hupewa dawa za minyoo (deworming) kila baada ya
miezi 2. Dawa za minyoo hupewa kulingana na umri wa mbwa. Mbwa
aliyefikisha umri wa mwezi mmoja na nusu hupewa nusu tembe ya dawa aina
ya Plozin, miezi 6 hupewa tembe moja na aliye zaidi ya miezi minane
hupewa tembe mbili.
"Kuna haja ya mbwa
kuhusishwa kwenye matembezi ili kunyoosha viungo vyao vya mwili na
almuradi wapunge hewa mwanana," adokeza Bw David Mbithi.
Kauli
ya Bw Mbithi inaenda sambamba na ile ya Bw Ng'ang'a mfugaji wa mbwa
Kimbo Githurai 45 ambaye kila siku jioni hupeleka mbwa wake alionao sasa
wapatao takriban 25 ziara kunyoosha viungo vya mwili na kupunga hewa
safi.
"Mbwa wangu ni sharti kila siku jioni
niwapeleke ziara kwenye sehemu tambarare ili pia niwafunze mambo ya
usalama na kunusa kutambua adui. Nimeajiri kijana mmoja anayenisaidia
kutekeleza kazi hii naye pia nimemfunza lugha ya mbwa ya kuwasiliana
nao," aeleza Bw Ng'ang'a akifichua wateja wake wakuu wa mbwa ni kampuni
za usalama na maafisa wa polisi kutokana na mafunzo yake ya kipekee kwa
mbwa.
Wateja wakuu wanaonunua mbwa ni makampuni ya usalama (security firms) na wanaowahifadhi kwa minajili ya kuimarisha usalama katika makazi yao na wanyama wa kucheza nao (pets)........................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment