script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




https://www.mshindoveterinarycentre.comSOMO: UFUGAJI KUKU WA NYAMA
Karibu ndugu mfugaji katika somo hili  la ufugaji wa kuku wa nyama au kwa jina la kitaalamu (broiler).
Ushauri wangu kwako mfugaji,  kabla hujaanza kufuga kuku hawa kwanza Fanya uchunguzi wa soko hasa kwa maeneo uliopo. Ili utakapofikia wakati wa kuwauza uwe na uhakika wa soko kwasababu kuku wa nyama watakapochelewa bandani hiyo ni athari kwa mfugaji.
Kuku wa nyama (BROILER) wanakua kwa muda wa wiki 4-6 mpaka kuuzwa wakiwa na  kilogram moja pia ukiwapa matunzo mazuri hufikisha mpaka kilo moja na nusu hata zaidi tunaanza na ulishaji wa chakula.
Wiki mbili za mwanzo hupatiwa broiler starter.
Wiki ya tatu hupewa broiler grower .
Wiki ya 4 hupewa broiler finisher
Mpaka kuuzwa ukizingatia hayo hakika watakua vizuri pia mazingira yake yawe ndani sehemu ambayo kuna joto la kutosha lisilokithiri.
Kama  unauwezo weka bulb au hata taa ya chemli kama utashindwa gharama za umeme pia kuweka jiko la mkaa kwa ajili ya joto hasa muda wa wiki mbili za mwanzo ni muhimu kwa ajili ya kuwapa joto.
Kuwa makini kwani joto likizidi  huleta madhara pia.
Chini ya sakafu kunatakiwa pawe na bedding material au kitaalam tunaita litters ila lazima utangulize maranda na magazeti hufuata kwa juu, magazeti hukusaidia wewe mfugaji katika kufanya usafi pale maji yanapo mwagika yanakurahisishia kusafisha au kingine n pale mfugaji unapotaka kufahamu iwapo mifugo wako wanaumwa au laah kwa kuangalia rangi ya kinyesi.
Kumbuka kubadilisha magazeti kila yanapochafuka na hata maranda pia yanapoonesha kubadilika rangi na kuwa mbolea basi huna budi kuyaondoa kwani kwa kuyaacha tu yataleta magonjwa na kusababisha vifaranga kufa pia usafi ni muhimu sana kwani kinyesi kinapozidi kinawachoma chini ya kifua wanapolala na kusababisha tatizo lingine.
Tumia feeders kwa kuwapa chakula kama huna uwezo kata ata madumu vizuri kwa kiwango kizuri ambacho watafikia kuweza kula chakula pia kwenye drinkers za maji fanya hivyo hivyo kama huna uwezo wa drinkers  kama ilivyo kwa feeders kumbuka, pia ni vizuri vifaranga kuwaweka kwenye brooder/ bruda.
Pia nyumba inatakiwa iwe na madirisha mapana, makubwa uzibe na turubai kwa ajili ya kuzuia baridi na upepo inakua hivyo kwa ajili ya kuwa rahisi kufunua wakati joto linapozidi japo upande mmoja wakati wa mchana.
Hairuhusiwi mtu yoyote ambaye hahusiki kama muhudumu kuingia hovyo ndani ya banda kwani anaweza kuleta maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama bacteria
Pia nje ya mlango ni lazima kuwekwa dawa kwenye sehemu iliyotengenezwa mlango ili watu wanapoingia waweze kukanyaga na viatu vyao ndipo waingie kitaalam tunaita disinfectant.
Pia lazima pawe na daftari la kurekodi vifo na walio hai kwa kila jioni na asubuhi hivyo hivyo kuwapima uzito kwa kila jioni na asubuhi na kurekodi kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho (weigh bridge)  kumbuka walemavu wanatakiwa watengwe sehemu yake mara nyingi wanashindwa kutembea hii huchangiwa na matatizo mengi huweza kuwa kwa kitaalam (genetic makeup yake ndivyo kizazi kilivyo amerithi kwa uzao wa nyuma au kukosekana kwa madini kama calcium hiyo pia huchangia.Kingine cha kutakiwa kufanya ni kufuata ratiba za chanjo kama ifuatavyo, kwa kuku wa nyama haina haja ya kuchanjwa Marek's kwani wanaishi muda mfupi na huo ugonjwa hutokea baada ya muda ambapo broiler hawatokua bado wapo hai watakua wamefikia kuuzwa.
Pia siku ya kwanza inashauriwa wakija vifaranga wapewe glucose kwa ajili ya kuwapatia nguvu shauri ya ule uchovu wa safari, glucose hiyo ichanganywe kwenye maji, siku ya 2 - 6 wapatiwe otc plus pamoja na vitamin. Siku ya 7 wapewe chanjo  ya Newcastle then siku ya 14 wapewe chanjo ya gumboro kufikia siku ya 21 wapewe chanjo ya gumboro na siku ya 28 wapewe chanjo ya Newcastle  hapo sasa mpaka kufikia mauzo ila katikati ya siku na kuendelea utatibu kulingana na dalili unazoona kutokea kama magonjwa mengine.
..............................................................................................................................

0 comments:

 
Top