Karibu ndugu mfuatiliaji wa makala hizi za ufugaji wa kuku. Nimatumai yangu una afya njema ili kuweza kuwa pamoja na mimi katika kujifunza changamoto na namna ya kufanikiwa katika swala zima la ufugaji. Karibu leo katika mada nyingine inayohusu banda la kisasa ( kwa lugha ya kigeni inaitwa"cage") ambalo inafaida nyingi nzuri katika kupunguza changamoto mbalimbali za ufugaji wa kuku. Cage imeleta utofauti mkubwa japo ni gharama lakini ukitazama kwa jicho la tofauti au kwa kina utagundua ufugaji wa kawaida una changamoto nyingi ambazo zinaweza pelekea kufikia gharama za kuwa na cage.
Zifuatazo ni faida za kutumia cage (banda la kisasa)
1.kuzuia upotevu wa chakula. Banda hii limetengenezwa katika ubora ambao unawezesha kuku kupata nafasi ya kutoa kichwa nje ya banda na kula chakula chake bila kuchakua na mdomo au miguu ambayo mara nyingi ndio inayosababisha umwagaji wa chakula chini na kupelekea upotevu wa chakula kingi chini. Namna inavyokuwa ni kwamba kuku anakuwa kwa ndani lakini sehemu ya chakula ipo kwa nje.
2. Unatumia muda mchache kuhudumia kuku wengi. Hii ni faida nyingine ya banda hili la kisasa maana hapa tunaweza kuzungumzia ufugaji mkubwa wa kuku kuanzia kuku 200 na kuendelea. Namna ya kuwa hudumia wakiwa chini katika banda la kawaida ni changamoto, kwa namna ya kuwapa chakula, kuokota mayai kama ni kuku wa mayai, kusafisha banda n.k lakini matumizi ya cage hurahisisha namna zote kwa maana ulishaji wa chakula, kuokota mayai na kusafisha banda kwa urahisi ndani ya muda mfupi unaweza kuhudumia kuku zaidi ya 1000.
3. Hupunguza magonjwa ya kuambukizwa. Katika mabanda yetu ya kawaida kwa maana ya chumba ambacho kuku wanakuwa chini mara nyingi, kuku hula kinyesi chake au cha mwingine kulingana na eneo husika. Hivyo ni rahisi sana kwa kuku mgonjwa kuweza kuambukiza kuku wengine hasa kupitia kinyesi. Lakini hii ni tofauti ukitumia cage, kinyesi chote kinadondokea chini bila kufika katika sehemu nyingine ambapo kuku wapo.
4. Kujua idadi kamili. Kwa kawaida kuku wanaofugwa chini ni vigumu sana kuweza kuwa hssabu na kujua idadi kamili hasa kuanzia kuku mia na kuendelea na pia hata kama kuna wizi unafanyika kugundua si rahisi, lakini matumizi ya cage hurahisisha kuwa na takrimu sahihi za kuku wako, kwa sababu cage moja inakaa kuku 96 na ndani yake kuna visehemu ambavyo hukaa kuku wa 4 kila kisehemu. Hivyo ni rahisi kujua idadi ya kuku wako kila siku.
5. Inarahisisha zoezi la ukusanyaji wa mayai. Namna cage ilivyotengenezwa inaruhusu kuku kutaga na yai kushuka toka ndani na kuja nje ya banda ambapo kuna sehemu maalumu kwa ajili ya mayai yaliyotagwa ilikukusanywa kirahisi, tofauti na utaratibu wa kawaida tuliouzoea kuokota mayai chini. Ambapo muda mwingine kama kuku wana upungufu wa madini ya calcium hula mayai yake lakini kwenye banda hili hawezi fanikiwa kula yai kwa namna banda lilivyotengenezwa.
6. Inarahisisha kusafisha na kukusanya mbolea. Hili zoezi liko kama ifuatavyo, banda hili lina ngazi tatu kwa namna lilivyotengenezwa katika pande zote kushoto na kulia ila kila sehemu ya banda ambapo kuku hukaa ina uwazi wa kudondosha kinyesi chini bila kuangukia kwa wengine na kwa namna banda lilivyo kinyesi chote kitakuwa chini ambapo kuna uwazi mkubwa wa kuruhusu mfugaji kuweza kusafisha kwa urahisi na kuku sanya mboleo.
Himisho kwa faida za kuwa na zao bora la mradi wako. Tunashauriwa ni vyema tukatumia banda la kisasa. Lina matokeo mazuri zaidi, japo ni gharama lakini ubora wake ni maradufu ya ufugaji wa kawaida. Changamoto nyingi zinapungua katika matumizi ya cage ( banda la kisasa ). Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru ndugu msomaji na mfuatiliaji kwa kuwa pamoja na mimi kuanzia mwanzo wa makala hadi kufikia hapa. Karibu tena katika mfululizo wa makala zijazo siku kama ya leo
.............................................................................................................
0 comments:
Post a Comment