MAMBO SITA (6) YA KUHAKIKISHA UZAO WA
Karibu sana ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala hizi za ufugaji wa kuku aina zote kulingana na fursa tuliyonayo katika nchi yetu. Nimatumai ya kwamba u mzima wa afya
Karibu katika mada ya leo ambayo itakusaidia kuweza kutatua changamoto ya kuweza kuwa na kuku wengi kwa kadri, Mungu atavyo kujalia uhai.
Mada yetu ya leo inahusu izao wa uhakika wa kuku wako bila kubahatisha. Hasa kwa wafugaji wa kuku wa kienyeji majumbani kwetu. Tumekuwa na mazoea ya kumwachia kuku ajilee mwenyewe na kutarajia kupata kitu bora. Katika uharisia haiwezekanai. Ufwatiliaji wa karibu ni muhimu ili kujihakikishia angalai asilimia 80 hadi 90 ya kufanikisha kile unachokitaka.
Yafuatayo ni mambo sita (6) ya kuhakikisha uzao wa kuku wako
1. Kuchukua mayai kila yanapotagwa.
Kuku pindi atakapofikia kuanza kutaga mayai, ni muda muafaka kuanza zoezi hili la hatua ya kwanza lakini subiri atakapo taga mayai mawili hadi matatu ndipo uanze kuchukua na hapo naomba tuelewane kwamba, kuku wako akifikisha mayai mawili itakuwa na maana ni siku yake ya pili kutaga. Kuku kwa kawaida hasa wa kienyeji hutaga yai moja kwa siku. Hivyo zoezi la kuchukua mayai ni pale atakapotaga yai la tatu ndipo uchukue na kuacha yale mawili yaliyotangulia kutagwa. Ni muhimu sana kuchukua yai jipya.
2. Kuweka alama katika kila yai .
uwekaji wa alama katika mayai ni muhimu sana ili kuweza kutambua yai limetagwa lini na kwa pendekezo hakikisha una kalamu ya mkaa (penseli) na uweke alama ya namba ( kama vile 1, 2, 3,.......) hii itasaidia kujua ni yai la ngapi kutagwa tangu kuku wako aanze kutaga. Kabla ya kuweka alama hakikisha mikono yako haina harufu yoyote ile, hivyo kama mikono yako ina harufu, chukua majivu yanawe kama maji, yatakusaidia kuondoa harufu. Andika namba kwenye yai moja kila linapotagwa kwa kuanza na namba moja na kuendelea.
3. Kuhifadhi sehemu salama.
Baadaya kuchukua na kuweka alama hakikisha umeanda sehemu nzuri ambayo haina joto na watoto hawawezi kuchezea. Sehemu hiyo inaweza kuwa kwenye treyi lako au boxi ambalo umeweka malanda ya mbao au pumba ya mpunga na kuyapanga vizuri kulingana na namba ulizo weka kama alama na kimsingi utakuwa umeanza na yai la tatu tangu kutagwa. Hakikisha sehemu uliyoweka hakuna joto maana yai likipata joto litaharibika.
4. Kuchuka mayai yasiyozidi wiki mbili kwa ajili ya kuatamiwa.
Yai bora kwa ajili ya kuatamiwa ni lile lisilozidi wiki mbili tangu kutagwa. Katika zoezi hili hakikisha unachukua mayai yote uliyoyahifadhi. Kuku aliye vizuri katika utagaji hutaga mayai kumi na tano hadi ishirini, hivyo kwa kuwa uliweka alama katika mayai uliyo ya hifadhi anzia namba ya mwisho kuandikwa kurudi nyuma,kwa maana anza na yai la mwisho kutagwa kurudi nyuma lakini hakikisha unakumbukumbu ya tarehe ya kuku alipoanza kutaga, hiyo itakusaidia kujua mayai ya wiki mbili tangu kutagwa ni yapi. Muwekee kuku mayai 12 hadi 15 kulingana na umbo la kuku wako. Mfano kuku wako kataga mayai 15, hivyo utachukua yai la 15 hadi namba ya yai itakalo kuwa ndani ya muda unaofaa. Kuku wa kienyeji hutagi siku zote mfululizo kuna baadhi ya siku anaruka kwa hiyo hayo mayai kumi na tano yanaweza kuwa yametagwa kwa wiki tatu.
5. Siku ya kumi baada ya kuatamiwa, yapime mayai.
Hii ni sehemu au zoezi muhimu sana ilikuweza kujua kuwa mayai yaliyoatamiwa yatafaa au la. Upimaji hufanyika usiku kwa maana giza likiingia ambapo kuku wote watakuwa bandani. Zoezi hili linaitaji watu wawili ili kuweza kufanikisha. Mmoja kumshika kuku na mwingine kufanya zoezi la upimaji.Chukua tochi, mikono ya mpimaji isiwe na harufu, hivyo kujiridhisha kwa kunawa majivu na kuanza zoezi la upimaji. Chukua yai mojamoja, halafu kiganja chako kimoja kitengeneze umbo la sifuri kwa kutumia kidole gumba na kidole kinachofuatia baada ya hapo weka yai kwa juu yake kwa kutanguliza sehemu iliyochongoka iwe chini. Halafu chukua tochi na murika kwa chini kule kulikochongoka yai, utaona mambo mawili kwanza, kama yai ni zima utaona kitu cheusi ndani ya yai ujue linafaa kuendelea kuatamiwa. Pili, kama utaona yai ni jeupe ( transparent) ujue ilo yai halifai kwa kutotolewa. Zoezi litaendelea mpaka mayai yote yaishe hapo utakuwa umejihakikishia kuwa ni mayai mangapi mazima na yatatotolewa.
6.kutotolewa kwa mayai yote yaliyoatamiwa
Mpaka kufika hapo zoezi zima litakuwa limefanikiwa kwa asilimia 90 hadi 100 kwa maana ya kutotolewa vifaranga vyote ambavyo katika upimaji utakuwa umejiridhisha kuwa ni mayai mangapi yatatotolewa na ni uhakika idadi iyo iyo ya upimaji kufika katika utotolewaji.v
Hitimisho, nipende kusisitiza kuwa katika zoezi zima la hatua ya kwanza hadi ya mwisho mayai yako yawe yamewekwa kwa kutanguliza sehemu iliyochongoka chini na pana juu hasa kwenye hatua ya kuhifadhi pindi unapoyachukua yanapotagwa. Nikushukuru ndugu msomaji kwa kuwa nami tangu hatua ya kwanza hadi ya mwisho. Hakiki utakuwa umepata kitu na kukifanyia kazi. Karibu sana tena katika makala zinazofuata
.............................................................................................................

0 comments:
Post a Comment