NDIGANA KALI (EAST COAST FEVER ) UGONJWA HATARI UNAOSHAMBULIA NG’OMBE, MBUZI, KONDOO NA NYATI
UGONJWA wa Ndigana Kali au kitaalamEast Coast Fever (ECF) hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, nyati na nyati wa India wakaao kwenye maji (Water Buffalo).
Visababishi Vya Ugonjwa
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea (protozoa) vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo husambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanao kama Rhepicephalus Appendiculatus.
Kwa kawaida, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine.
Ndigana Kali ni ugonjwa ulioenea sana hapa nchini kwetu na Afrika Mashariki, ambapo ng’ombe huanza kuugua siku 10 – 25 (wastani siku 14) tangu kuambukizwa.
DALILI ZAKE
•Joto kali hadi kufikia 42c badala ya joto la kawaida la ng’ombe la nyuzijoto 38c
•Homa kali
•Mnyama kushindwa kupumua vizuri
•Kukohoa
•Kuharisha
•Kuvimba matezi ya shingoni na mabegani
•Manyoya ya mgongoni husimama muda wote na huwa na rangi ya udongo (brown) kwa mbali.
•Kutoa makamasi laini puani.
•Mnyama hushindwa kula vizuri
•Pua (muzzle) huwa kavu bila unyevu unyevu.
MATIBABU
Mnyama inabidi achomwe sindano ya dawa za BUTALEX.
Pia mnyama achomwe dawa ya OTC 20%kipindi chote cha matibabu.
Dawa aina ya BUTALEX ni maarufu sana hapa nchini kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu, ni muhimu dalili za mwanzo zinapoonekana kumtaarifu mtaalam wa mifugo na ikithibitika ni Ndigana Kali tiba ianze mara moja.
KINGA
Kinga kubwa ni kuogesha mifugo yako mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo.
Tumia dawa za kuogeshea zilizopo kwa sasa mfano: t Tik Tik, Taktic, Tik Fix, Steladon, Dominex au drop on.
Wastani wa kuogesha ni kila baada ya wiki 2 mara moja. Hakikisha unachanganya dawa katika vipimo sahihi.
NB:Kumbuka Wanyama wapewe maji ya kunywa ya kutosheka
...............................................................................
0 comments:
Post a Comment