script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X





Siku ya leo tutaendelea na kwa kuangalia magonjwa mengine  ya kuku ambayo hutibika kwa dawa kama ifuatayo:
 Ugonjwa huu husababishwa na virusi.
Dalili. 
Kuku huzubaa na kujikunyata

Kuku kuharisha kinyesi chenye damu au kinyesi cha kahawia

Kuku hudhoofika,manyoya huvurugika na kulegea mabawa na kuonekana kama wawevaa koti

Kuku hupungukiwa homa ya kula

Vifo huwa vingi kwa vifaranga
Tiba ya ugonjwa huu.Wape kuku wako dawa kama Esb 3, Amprolium, au Basulfa.
Kinga za ugonjwa huu.Zingatia usafi wa banda la kuku na usiruhusu unyevuunyevu katika banda la kuku.
2. HOMA YA MATUMBO(Fowl typhoid)
        Husababishwa na bakteria
 Dalili za ugonjwa huu ni;
   Kuku hupata homa kali

   Kuku huarisha kinyesi cha kijani au njano

   Vifo huwa vingi hasa kwa vifaranga wenye wiki 1-2

   Kuku huzubaa,kuvimba viungo vya miguu,kuchechemea,kukosa hamu ya kula

   Kuku wanaotaga hupunguza utagaji,hutaga mayai yenye ganda laini na hupata   vifo vya ghafla
 Tiba za ugonjwa huu.
  Dawa za oxytetracycline kama Furamax,Typhoprim hutibu ugonjwa huu.
 Kinga za ugonjwa huu.
  Hakikisha usafi wa banda na vyombo vya chakula na maji kwa kuku.
  Tenganisha kuku wagonjwa na wazima
3. MINYOO
Hushambulia kuku wote wakubwa na vifaranga
 Dalili za ugonjwa huu
Kuku hukonda

Kuku huarisha

Kuku hukohoa

Kuku hupunguza utagaji

Kuku hudumaa katika ukuaji/hawakui vizuri

Kuku hupungua uzito
Tiba za ugonjwa huu.
Tumia dawa za minyoo kama piperazine
Kinga za ugonjwa huu.
Wapewe dawa za minyoo mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu
4.VIROBOTO/CHAWA/UTITIRI
   Hushambulia sana vifaranga na hutokea vifo kwa wingi kwa vifaranga Kwa kuku wakubwa tatizo halionekani kwa sana lakini nao huathiriwa sana.
Dalili za ugonjwa huu.
 Kuku kutochangamka

 Ukuaji mdogo wa kuku

 Kuku kutotaga na kuhatamia vizuri kutokana na kusumbuliwa na chawa,utitiri au  viroboto

 Viroboto huonekana kuganda machoni wakinyonya damu
Tiba za ugonjwa huu
Tumia dawa za unga kama sevin dust 5% ,Malathion ,akheri powder kwa kuku wote na mabanda yao.
Kinga za ugonjwa huu.
 Boresha usafi wa mabanda ya kuku.
..........................................................................

0 comments:

 
Top