Habari za wakati huu wasomaji na wafuatiliaji wa website yetu inaolenga katika kuelimisha watu hasa vijana katika ufugaji wa kuku wa kienyeji na chotara,Hivi karibuni watu wengi wamekua wakilalamika juu ya utotoleshaji mbovu wengi wamekua wikidhani ni mashine za kutotolesha,lakini tatizo kubwa ni sisi wafugaji kushindwa kutunza mayai vizuri,Hapa chini ni maelezo ya namna bora ya kutunza mayai kwaajili ya kutotolesha.
Yai lisizidi siku 7 mpaka 8 tangu litagwe
- Zingatia Uwiano mzuri wa majogoo kwa matetea (1:8-10)
- Mayai ya mtago wa kwanza sio mazuri kwa kutotolesha
- Mayai ya kuku mzee sio mazuri kwa kutotolesha
- Kuku watagaji wanapaswa kupewa chakula bora na cha kutosha
- Mayai yahifadhiwe sehemu isio na joto kali
- Mayai machafu hayafai kwa kutotolesha
- Mayai madogo sana hayafai kwa kutotolesha
- Mayai yenye kreki(nyufa)hayafai kwa kutotolesha
- Mayai yenye umbo kubwa sana hayafai kwa kutotolesha
- Mayai yenye viini viwili hayafai kwa kutotolesha
- Yai lisihifadhiwe kwenye friji(hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isio na joto)
- Wakati unahifadhi mayai katika trei hakikisha sehemu ya yai iliyochongoka inaangalia chini
0 comments:
Post a Comment