script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




NG`OMBE BORA WA MAZIWA, BANDA, CHAKULA PAMOJA NA HUDUMA ZA  CHANJO.

Sifa za Ng’ombe wa maziwa.

Kabla ya kuchagua ng’ombe wa maziwa zingatia kuwa uchaguzi huu huanziea pale ngombe anapokuwa  heifer huu ni umri mzuri wa kuchagua na kuanzia ufugaji wenye tija kwa wale ng’ombe wanaotoa maziwa, pia
  - Awe ametoka kwenye koo au familia inayozalisha vyema maziwa na isiyokuwa na historia ya magonjwa.

- Awe na umbo lenye kupanuka kwa nyuma na kupungua kuelekea mbele
- Pia mgongo wake uwe umenyooka
- Pia kiwele chake kiwe na chuchu nne
- Kiwele chake kiwe kimeshikamana vizuri
- Miguu iliyo nyooka vizuri.
- Asiwe amekonda sana pia asiwe mnene sana (awe na umbo la wastani).
- Asiwe na matiti makubwa sana ama matit madogo sana bali ya ukubwa wa wastani.
- Pia awe na umbo la wastani.


SIFA ZA BANDA.

Sifa hizi ni kwa ng’ombe ambao hufugwa katika mifumo ya ndani au nusu ndani nusu nje, kwa wale wanaofugwa katika mfumo huri cha kuzingatiwa ni banda tu kuwa na sakafu, ukuta pamoja paa.
Pia ng’ombe anahitaji nyumba yenye sifa zifuatazo
- Nafasi.
Ng’ombe mkubwa anahitaji kuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili ya chakula, kupumzika pamoja kufanya mazoezi.
- Paa.
Ni vyema kukawa na paa kwa ajili ya kuilinda mifugo dhidi ya upepo, mvua pamoja na jua kali. Hakikisha paa linakuwa juu, ili kuipa uhuru mifugo yako kutembea ndani ya banda bila tatizo lolote. Hakikisha mteremko wa paa hauwezi kuathiri sehemu ya mifugo kupumzika na sehemu ya lishe hasa kwa kuruhusu maji kuingia katika sehemu hizo.
- Sakafu
Hakikisha sakafu inakuwa na mfumo mzuri wa mifereji kwa ajili ya kuruhusu maji na mkojo kupita hivyo kuwaweka mifugo katika hali nzuri. Sakafu inaweza kuwa imetengenezwa kwa saruji, tofali au mawe na hata pengine kwa moramu, zingatia kuwa sakafu haitelezi.
- Sehemu za chakula na maji.
Chakula cha mifugo kama nyasi na pumba, Hii ni kwa wale wanaofungwa katika mifumo ya nusu ndani nusu nje pamoja na wale ambao wanafungwa ndani tu.
- Kibanio
Kibanio haswa haswa kwa matumizi kama kukamulia na kwaajili ya matibabu ya wanyama pale wanapoitaji matibabu au chanjo
- Sehemu za kunywea maji.
Kwa ng’ombe watakao fungwa katika mfumo wa ndani, au nusu ndani nusu nje sehemu za kunywea maji ni muhimu sana kuwekwa, ziwe zimenyanyuliwa juu kiasi ambacho mnyama anaweza kufikia kwa urahisi na kunywa maji bila bughuza wala usumbufu, kisiwe juu sana au chini sana, juu sana haitakuwa rahisi mnyama kufikia na chini sana upelekea wanyama kuchafua maji.
Pia kwa wanyama ambao hufungwa katika mfumo huru sehemu za kunywea maji ni muhimu sana wawe na sehemu maalumu za kunywea maji iwe katika mabwawa maalumu
Usafi wa banda ni muhimu sana kuzingatiwa kila siku na isiache banda likiwa chafu hali hii itapeleka mlipuko wa magonjwa kama kuoza kwa miguu.
Shimo au maala maalumu kwaajili ya kuhifadhia samadi ni muhimu sana kuwekwa kwaajili matumizi ya shamba au hata kwa kufanya biashara ya kuuza samadi.

CHAKULA

Malisho ya kijani ni mlo mkuu kwa mifugo.
Mlo muhimu na wenye virutubisho kwa mifugo ni majani. Lakini malisho bora ya kijani ni yale yanayoweza kumpatia ng’ombe wa maziwa virutubisho muhimu vinavyohitajika. Malisho bora yanakuwa na zifuatazo.
- Ni ya kijani kibichi na machanga hii ina maana kuwa, majani ya malisho ni lazima yakatwe na kuhifadhiwa yakiwa bado machanga na kabla ya kuchanua.
- Ni lazima mfugaji afahamu kuwa mimea ambayo imepoteza rangi yake halisi ya kijani inaweza tu kuwasaidia mifugo kuishi lakini haina virutubisho muhimu vya kuwapa mifugo nguvu, madini, protini na haiwezi kusaidia katika uzalishaji wa maziwa.
- Malisho yenye viwango vya chini vya virutubisho ni lazima yaongezewe kwa chakula cha ziada chenye virutubisho vya kutosha kitakachoziba pengo la virutubisho vilivyokosekana.
Vyakula vya kutia nguvu
Aina zote za majani ni chanzo kizuri cha vyakula vya kutia nguvu kwa mifugo, endapo tu yatalishwa yakiwa bado machanga. Majani yaliyo maarufu kwa malisho ni pamoja na matete, ukoka, majani ya tembo, seteria na Guatemala. Majani ya mahindi au mtama ni chakula kizuri sana kwa kuwapa nguvu mifugo. Vyakula vya kutia nguvu vilishwe kwa kiasi kidogo. Vyakula hivi vinaweza kutokana na aina zote za nafaka, punje za ngano, au molasesi.
Vyanzo vya Protini
Kanuni ya 1: Mimea michanga ina kiasi kikubwa cha protini kuliko mimea iliyokomaa. Mahindi machanga pamoja na majani ya viazi vitamu ni mahususi kwa protini.
Kanuni ya 2: Mikunde ina protini nyingi zaidi kuliko nyasi. Mfano, mabaki ya majani ya maharage, njegere, desmodium na lusina. Majani yanayotokana na mimea kama lusina, calliandra au sesbania ina kiwango kikubwa cha protini pia. Ng’ombe wasilishwe kwa kutumia aina zote za jamii ya mikunde kwa zaidi ya asilimia 30 ya uwiano wa mchanganyiko wa malisho ili kuepuka matatizo ya kiafya. Aina nyingine ya vyakula vyenye protini ni mashudu ya pamba, mashudu ya alizeti na soya.
Madini: Mifugo wanahitaji madini ya ziada. Ni lazima yapatikane muda wote, mfano kama jiwe la chumvi. Wanyama wanaokuwa, wenye mimba, na ng’ombe anaenyonyesha wanahitaji kiasi kikubwa cha madini, mfano calcium na phosphorous. Mimea ya jamii ya mikunde na mengineyo isipokuwa nyasi inatoa kiasi kikubwa cha calcium na madini mengineyo.
Pumba Ndiyo lakini si kwa kiasi kikubwa!
Pumba aina ya chakula cha ng’ombe chenye kiwango kikubwa sana cha madini. Lakini ina madhara kwa mifugo endapo wanyama watalishwa kwa kiwango kikubwa. Malisho yanayotokana na majani au nyasi kavu ni lazima yabakie kuwa chakula kikuu kwa mifugo. Haishauriwi kulisha zaidi ya kilo 6 za pumba kwa siku kwa ng’ombe mwenye kilo 450. Ni lazima wapewe kwa kiwango kidogo sana, ambacho si zaidi ya Kilo 2 kwa mara moja na kichanganywe na majani. Kuongeza kiwango cha pumba kabla na wakati wa kunyonyesha/kukamuliwa, kisizidi kiasi cha kilo 2 kwa wiki ili tumbo la mnyama lizoee
Resheni 1
Mahita
Mabua ya mahindi yaliyokatwakatwa - Debe 2
Majani ya viazi vitamu yaliyokatwakatwa - Debe 2
Matete yaliyokatwakatwa - Debe 2
Mahindi - Sado 3
Mbengu ya pamba - Sado 11/2
Chumvi ya ng’ombe - Vijiko 2
Resheni 2
Mahitaji Pamoja na Kiwango
Mabua ya mahindi yaliyokatwakatwa - Debe 2 zilizoshindiliwa
Lusina iliyakatwa - Debe2
Matate yaliyokatwakatwa - Debe 2
Pumba - Sado 5
Chumvi ya ng’ombe - Vijiko 2
Kwa kipindi cha kiangazi ambapo majani mabichi ni nadra sana kupatikana wapatie mifugo wako maji kwa wingi pamoja na chakula chenye uwiano ufuatao.
Pumba za mahindi kilo 47, mahindi yaliyoparazwa kilo 20, mashudu ya pamba/ alizeti kilo 20, unga wa lukina kilo 10, chokaa ya mifugo kilo 2 na chumvi kilo 1.

FAHAMU PIA CHANJO MUHIMU ZA KUWAPATIA NG’OMBE

- Chanzo dhidi ya minyoo.
- Chanjo ya ugonjwa wa cha mkono (black quater)
- Chanio dhidi ya ndigana kali (east coast fever)
- Chanjo dhidi ya ndigana baridi (anaplasmosis)

0 comments:

 
Top