script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Bila kuku kulishwa chakula bora na kupewa maji safi ,salama,yasiyokuwa moto na yanayopatikana muda wote wa mchana na usiku ,usitegemee mayai mengi wala nyama nyingi ,laini na nyeupe.
Ulishaji bora uanzie kwa vifaranga wa siku  moja hadi kipindi chote cha utagaji au kuku kuuzwa kwaajiri ya kuchinjwa.
Chakula bora cha kuku ni mchanganyiko maalum uliozingatia uwiano wa:-
~Vyakula vya aina ya protin (protin nyama,protin mimea) kwa kujenga mwili na kuunda sehemu za mwili zilizoharibika.
~Madini kama chumvi na chokaa kwa kujenga mifupa na kutengeneza makaka ya mayai
~Vyakula vya wanga kwa kutia nguvu mwili wa kuku.
~Mchanga kwaajiri ya kusaga chakula
~Vitamin kwa kutia afya mwili na kumfanya kuku awe mchangamfu
~Kazi ya maji ni kuwezesha chakula hicho kumeng'enywa ili kiweze kuingia mwilini na kufanya kazi iliyokusudiwa
~Kuku hukua haraka
~Kuku hukomaa mapema
~Kuku huwa na afya nzuri
~Kuku kutaga mayai mengi,makubwa na yenye makaka magumu
~Utagaji huendelea kwa muda mrefu
~Nyama huwa nyingi,laini na nyeupe
~Uzito wa kuku huongezeka

0 comments:

 
Top