MABANDA BORA YA KUKU

Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni miongoni mwa
mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au
wale walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwahiyo
ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze
kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.
Mambo muhimu katika ujenzi wa banda la kuku ni;
1. Liingize hewa safi wakati wote.
2. Liwe kavu daima.
3. Liwe nafasi ya kutosha.
4. Liwe la gharama nafuu lakini la kudumu.
5. Lizuie kuingia wanyama na wadudu hatari kwa kuku.
6. Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na maji.
7. Lizuie upepo wakati wa baridi kali.
HEWA NA MWANGA:
Hewa ni muhimu kwa kila
kiumbe, hivyo banda la kuku ni lazima liingize hewa safi na kutoa ile
chafu na liweze kuingiza mwanga wa kutosha.
1. Kwa kifupi ni kwamba madirisha ya banda ni lazima yawe makubwa na ya kutosha ili yaingize hewa safi na kutoa ile chafu.
2. Ni vema madirisha haya yawe juu kiasi cha meta moja (1) kutoka chini ili hewa ipite juu ya vichwa vya kuku.
3. Hewa
safi siyo upepo, hivyo jaribu kuzuia upepo mkali kuingia ndani ya banda
la kuku ama sivyo kuku wataugua ugonjwa wa mafua na niumonia na
vifaranga vinaweza kufa kwa ugonjwa wa baridi.
4. Jenga Banda
lako kwa kukinga upepo unakotokea na kupanda miti kuzunguka banda hilo
la kuku ili kupunguza kasi ya upepo na kuweka kivuli dhidi ya jua kali
na joto.
UKAVU NA USAFI WA NDANI:
Kwa vile kuku si ndege wa majini kama bata , ni jambo la busara kuhakikisha kuwa mahali anapoishi hapana unyevunyevu.
§ Banda la kuku lijengwe mahali palipoinuka ili kuzuia maji ya mvua yasiingie.
§ Wajengee
kuku uchaga wa kulalia kwa kuweka viguzo vyenye urefu wa meta moja na
kutandika miti juu yake ili usiku walale hapo, kuliko kuwalaza ardhini
au sakafuni.
§ Ukavu
wa banda ni muhimu sana hasa kwa vifaranga na kuku wanaotaga. Ndani ya
banda lenye unyevu mayai kuchafuka sana hata wakati mwingine huoza kwa
urahisi na jitihada zako zitakuwa ni bure.
§ Sakafu
ya banda ni vizuri ikawa ya zege lakini kutokana na uhaba wa fedha
sakafu inaweza kutengenezwa kwa mabanzi (mabanda yaliyoinuliwa) au
udongo mgumu na au mchanga ambao utafunikwa kwa mabaki ya taka za mpunga
na yale ya mbao.
§ Ili kuepuka unyevunyevu ni vyema eneo/mahali pla kujenga banda pawe pameinuka na penye kupitisha hewa ya kutosha.
PAA LA BANDA:
Paa la banda liwe madhubuti ili kuzuia maji ya mvua kuingia hasa wakati wa masika. Sakafu ya banda iwe juu zaidi ya usawa wa nje.
Paa linaweza kuezekwa kwa mabaki ya vipande vya bati , madebe na kama
ikishindikana tumia nyasi zinazofaa kwa ajili ya kuezeka nyumba katika
eneo hilo.
NAFASI YA KUFANYA KAZI:
Banda la kuku lisiwe na nguzo au mbao nyingi sana
ndani kiasi cha kumfanya mhudumiaji wa kuku ashindwe kufanya kazi zake.
Hali hiyo itamfanya apoteze muda mwingi katika kuzizunguka nguzo hizo,
hasa wakati wa kuokota mayai au kufanya usafi.
VIFAA:
Unapotaka kujenga banda la kuku kwanza kabisa tayarisha vifaa vinavyotakiwa. Vitu kama miti au nyasi, nyavu au fito, misumari au kamba ni muhimu kuviandaa mapema.
Pili ni lazima uwe na plani/ramani kamili ya banda
hilo. Kwa wastani kila kuku anahitaji nafasi ya Meta za eneo la 0.11
hadi 0.22 (futi 1 hadi 2 za eneo.) kutegemeana na umri wa kuku.
UJENZI RAHISI:
Kuku wafugwao hatimaye ni lazima wafidie gharama za
Ujenzi wa mabanda na chakula. Gharama zikiwa kubwa sana huenda ukaifanya
shughuli ya ufugaji isiwe na faida hata kidogo hali hiyo itamfanya
mfugaji aone ufugaji hauna maana yoyote kwake. Lakini ukijenga banda
lako kwa kutumia vifaa vinavyopatikana kwa urahisi utaongeza faida zaidi
kwakuwa umepunguza gharama za uendeshaji wa mradi.
VIPIMO:
Banda la
kuku linatakiwa liwe na Meta 15 hadi meta 22 za eneo yaani Meta 3 hadi
4.5 za upana kwa meta 5 za urefu. Banda hili linaweza kutunza kuku 100
wakubwa kwa wakati mmoja.
HITIMISHO;
· Ujenzi wa mabanda unasisitizwa katika kuboresha ufugaji wa kuku wa asili ili;
· Kuongeza
uzalishaji na kupunguza vifo vya vifaranga kwa majanga mbalimbali kama
vicheche ,mwewe, mapaka, mbwa na wizi wa kuku wanaozurura holela.
· Vile
vile inatarajiwa kwamba kuku wanaozuiliwa kwenye banda na kuwekewa
chakula mchanganyiko wataongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.

UTAGAJI NA UATAMIAJI WA MAYAI:
a. Kuku
huanza kutaga wakiwa na umri wa majuma 22-32 baada ya kuzaliwa
kutegemeana na ukoo ,afya na lishe.Kwa kawaida kuku wa kienyeji /asili
watachelewa kutaga kuliko wa kisasa . Matetea hufikia kiwango cha juu
cha utagaji wakiwa na umri wa wiki 40-50 na baada ya umri huo utagaji
huanza kupungua kidogokidogo. Hali hiyo inapoanza kujitokeza wafugaji
wanashauriwa kuuza au kuchinja kuku waliofikia umri huo.
b. Kuku
wanaotaga ni lazima wapate chakula chenye madini ya chokaa ya kutosha.
Chakula hiki kinaweza kuboreshwa kwa kuongezewa maganda yaliyosagwa ya
mayai na ya konokono
c. wapatie
viota vya kutagia katika mabanda yao , kwa njia hii ni rahisi kuyapata
mayai na pia mayai yanakuwa safi. ilikuwafundisha kuku kutaga kwenye
viota unaweza kuweka mayai machache katika kiota au mawe yanayofanana
na mayai . kuku wanapoaanza kuatamia hukoma kutaga , kutokana na kuokota
mara kadhaa kwa siku unaweza kuepuka kuku kutaka kuatamia .unashauriwa
kutenga mara moja matetea wanaoanza kuatamia
kwa kuwaweka katika kibanda kidogo kilichotulia akae pekee yake sehemu isiyo na kiota kwa siku chache.
d. joto la kadri kwa kuku wanaotaga ni kati ya 18ºC -29ºC.
Mauzo ya mayai:
1. Hakikisha unafanya utafiti kabla ya kuanza kufuga.
2. Uza mayai kwa kuzingatia viwango kama vile rangi, ukubwa na maumbile yake.
3. uza
mayai safi kwa kuhakikisha unapanga mayai safi kwenye trei na yale
ambayo ni machafu unayasafisha kwa kupanguza na pamba au kitambaa
kilicholowekwa maji yasiyo na sabuni( kitambaa kisiwe kimetota maji).
Mayai haya yasafishwe kabla ya kuuzwa.
4. Punguza
uvunjaji na uchafuzi wa mayai. Hii inawezekana tu pale
utakapohakikisha unatengeneza viota vya kutagia na kuyaokota mara kwa
mara. Inapendekezwa uokote mayai mara tatu kwa siku. Asubuhi wakati
kulisha mchana na jioni. Kuvunjika kwa mayai huongeza hasara kwa mradi
na kuchafua matrei ya kutunzia .
Kuatamia.
Mayai ya kuku huanguliwa kwa siku 21 kabla ya vifaranga kutotlewa ilhali bata hutotoa baada ya siku 28.
Uatamiaji wa asili na utotoleshaji vifaranga:
Mayai kwa ajili ya kuatamiwa ni lazima yawe mapya;
1) Umri
wa mayai baada ya kutagwa usiwe zaidi ya siku kumi (10) na yawe
yamehifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi usozidi nyuzi joto 20ºC .Iwapo
hali ya joto iko juu kuliko 20ºC basi mayai ya kutotoa vifaranga
yasihifadhiwe kwa zaidi ya siku tano (5).
2) Ili
kupata matokeo mazuri, mayai ya kuatamiwa (mayai yaliyochaguliwa)
yanatakiwa yawe na umbo la kawaida na ukubwa wa wastani kwa aina ya kuku
wanaohusika.
3) Ganda
la mayai ya kuangua lisiwe na mikwaruzo au nyufa kwani likiwa na nyufa
yai hupoteza unyevunyevu ambao ukipungua kiiini cha yai kinaweza kufa
au linaweza kuingiza vimelea kama fangasi na bakteria ambavyo
husababisha kutotolewa kwa vifaranga vyenye afya mbaya au vilivyokufa.
4) Hifadhi
mayai ya kuangua kwenye makasha makavu ndani ya shimo lililopo ardhini
katika sehemu yenye ubaridi kuliko sehemu zote ndani ya chumba.
5) Kabla
mayai hayajaatamiwa chunguza mayai ambayo yana mbegu na yale yasiyo na
mbegu . Mayai ya kuku aliyepandwa na jogoo yanakuwa na mtandao wa
mishipa ya damu mapema sana ambayo inaweza kuonekana kwa kutumia mwanga
mkali wa kurunzi.
6) Kabla

7) Baada
ya mayai kuatamiwa kwa siku saba hadi kumi yanaweza kuchunguzwa mayai
yasiyorutubushwa na yenye viini vilivyokufa yanaweza kutambuliwa katika
siku saba baada ya kuanza kuanguliwa
8) Wakati
wa kupima kwa kutumia mwanga wa kurunzi mayai yaliyorutubishwa yanakuwa
na mishipa ya damu inayoonekana, na doa jeusi ambalo ndicho kiini cha
uhai.
9) Iwapo kiini cha uhai kimekufa, kinaoonekana kama kitu cha mviringo mfano wa pete kuzunguka kiini hai.
10) Mayai
ambayo hayajarutubishwa yanakuwa na nafasi kubwa ya hewa na kiini cha
uhai kinaoonekana kama kitu cheusi ndani ya ndani ya yai.
Mayai
ambayo hayajarutubishwa na yale yenye viini vilivyorutubishwa inabidi
yatengwe na kuondolewa ili yasije yakaozea ndani ya kiota, yakapasuka na
kuharibu mayai mazuri ambayo yapo katika kuatamiwa.
Kiota cha kuku anayeatamia;
1) Kuku anayeatamia atengwe katika kundi ili asisumbuliwe na kuku wengine ,
2) Mtengee kuku kiota ambacho kinampa nafasi ya kupata maji safi na chakula kwa karibu.
3) Kiota au kikapu ni lazima kiwe kikubwa kiasi cha kumpa kuku nafasi ya kuatamia mayai yote.
4) Weka matandazo makavu ambayo ni mapya yaliyonyunyizwa majvu kidogokuzuia visumbufu.
5) Iwapo
vifaranga wanaototolewa ni wachache njia nzuri ya kuatamia mayai ni
kumtumia kuku kuliko mashine ya kutotolesha vifaranga kwasababu kuku ana
uwezo mkubwa wa kutotoa vvifaranga kwa asilimia 80- 100 ukilinganisha
na mashine ambayo hutotoa mayai kwa asilimia 60-80 tu.
Vifaranga vikishatotolewa
vinaweza kulelewa kwa kumtumia mama ikiwa ni wachache. Lakini vifaranga
wanaweza kulelewa kwa kutumia kifaa maalum ya kulelea vifaranga.
LISHE YA KUKU NA KUCHANGANYA CHAKULA
LISHE YA KUKU:
Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na
kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula kingi na chenye ubora
unaotakiwa. Uwingi na ubora wa lishe ya kuku unaweza kuainishwa katika makundi ya vyakula kama ifuatavyo:
1. Vyakula vya kutia nguvu
2. Vyakula vya kujenga mwili
3. Vyakula vya kuimarisha mifupa
4. Vyakula vya kulinda mwili
5. Maji.
Makundi ya vyakula:
- Vyakula vya kutia nguvu:
Vyakula vya mifugo vifuatavyo vinawekwa katika kundi hili;
a. Pumba za mahindi, pumba laini za mpunga, na, pumba laini za ngano.
b. Nafaka kama vile mtama , chenga za mahindi ,chenga za mchele, uwele , na ulezi
c. Mimea
ya mizizi kama vile muhogo, viazi vitamu na magimbi. Kabla ya kulisha
kuku hakikisha mizizi hiyo inalowekwa kwa muda wa saa moja au kupikwa
kabla ya kukausha ili kuondoa sumu ambayo kwa asili imo katika vyakula
vya aina hii.Inashauriwa kuwa mizizi hiyo ilishwe kwa kiasi cha
asilimia 10% ya chakula chote anacholishwa kuku.
Katika kundi hili la kutia nguvu ,vyakula vya mafuta
kama vile mafuta ya kutoka kwenye vyakula vya mafuta kama mashudu ya
mimea ya mafuta, mafuta ya samaki husaidia kuongeza nguvu na joto
mwilini. Vyakula vya kutia nishati huchangia asilimia 60-70 ya
mchanganyiko wote wa chakula.
1. Vyakula vya kujenga mwili:
Mashudu
:Haya ni makapi ya mbegu za mimea aina ya mikunde na vyakula v
vinavyotoa mafuta kama vile alizeti, mawese, karanga, soya ,korosho, na
ufuta .
Damu
ya wanyama iliyokaushwa (waliochinjwa na kukaguliwa), hii inafanywa ili
kuepusha uwezekano wa kuku kupata magonjwa ya kuambukiza .
Mabaki ya samaki ya samaki/dagaa na nyama.
Vyakula
asilia kama vile minyoo, mayai ya mchwa, Masalia ya nyama toka kwenye
ngozi/mifupa, wadudu walioteshwa kutokana na damu au nyama iliyooza na
vyakula vya aina nyingine.
Vyakula hivi huchangia asilimia 20 hadi 30% ya mchanganyiko wote wa chakula cha kuku.
2. Vyakula vya kuimarisha mifupa(madini): a)Hivi
ni vyakula vya madini ambavyo huhitajika kwa ajili ya kujenga mifupa,
maganda ya mayai, kukua na kuuweka mwili wa ndege (kuku) katika hali ya
afya njema kwa ujumla.
b) Madini
ya muhimu ni madini ya chokaa (calcium) na fosiforasi (phosphorus). Ili
kuku watage mayai yenye ganda gumu ni lazima wapate madini ya chokaa
maganda ya konokono na mayai yaliyosagwa vizuri. Lakini inapendekezwa
kwamba unapoongeza madini ya fosforasi inakubidi uongeze pia madini ya
chokaa kadri inavyopasa ,kwasababu kiwango cha aina moja kikizidi kuliko
cha aina nyingine husababisha upungufu wa kile kidogo
Viinilishe vya madini vinavyotakiwa ni pamoja na;
Majivu
ya mifupa yaliyosagwa vizuri, unga uliosagwa wa magamba ya konokono wa
baharini, konokono wa nchi kavu na maganda ya mayai yaliyochomwa . Kabla
maganda ya mayai na nyumba za konokono havijatumika inashauriwa
yachomwe moto mkali au yachemshwe ili kuua vijidudu vya maradhi.
Chumvi ya jikoni
Madini yaliyotengenezwa viwandani kama vile Di-calcium phosphate
Magadi (kilambo).
4. Vyakula vya kulinda mwili:
Kundi hili linajumuisha vyakula vya mbogamboga kama vile;
Ø Mchicha, samadi ya ng’ombe ambayo haijakaa muda mrefu baada ya kunyewa, mchicha pori, Chinese kabeji n.k.
Ø na Mchanganyiko wa vitamini uliotengenezwa na viwanda vya madawa (vitamin premix).
Ø Jua
ni muhimu katika kuhakikisha vitamini A na D zinatumika vizuri mwilini,
kwahiyo banda ni lazima lijengwe kwa mtindo ambao unaruhusu mwanga
kupita hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Ø Chakula cha kuku wanaofugwa ndani ni lazima kichanganywe na vitamini zinazotayarishwa viwandani.
KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU:
Njia za kuchanganya chakula cha kuku;
Kuna njia kuu mbili za kuchanganya chakula cha kuku, nazo ni;
Kuchanganya chakula kwa mashine;
o Njia hii hutumika viwandani kuchanganya chakula kwa ajili ya kuku wanaofugwa katika mashamba makubwa.
Kuchanganya chakula majumbani (home made ration): Hii
ni njia inayotumika kuchanganya chakula kwa ajili ya kulisha kundi dogo
la kuku na njia ambayo inaweza kutumiwa na wafugaji wadogowadogo.
VIFAA; Beleshi /koleo(spade), Turubai/sakafu safi, Viinilishe , Viroba/Magunia kwa ajili ya kuhifadhia chakula kilichochanganywa.
Chakula kilichochanganywa kinaweza kuwekwa katika uzani wa kilo 25-kilo 50, au kilo 100.
Aina ya chakula kiasi
i. Vyakula vya kutia nguvu mwilini:
Ø Pumba za mahindi kilo 48
Ø Pumba laini za mpunga kilo 26
Jumla kilo 74
ii. Vyakula cha kujenga mwili :
Mashudu ya alizeti kilo 18
Damu ya wanyama kilo 1
Mabaki ya samaki /dagaa kilo 3
Jumla kilo 22
iii.Vyakula vya kuimarisha mifupa (Madini):
- chumvi ya jikoni kilo ½
- chokaa(dicalciumphosphate)… kilo 2
- poultry premix/ kilo ½
- unga wa mifupa kilo 1
Jumla kilo 4
Ø Mahitaji halisi ya viinilishe kwa muhtasari:
Ø Vyakula kutia nguvu mwilini kilo 74
Ø Vyakula vya kujenga mwili kilo 22
Ø Vyakula vya kuimarisha mifupa (Madini) kilo 4
JUMLA 100
Jumla ya mchanganyiko wa vyakula kilo 100
HATUA ZA KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU:
HATUA YA KWANZA:
Katika hatua ya kwanza utaanza kuchanganya vyakula vya madini
Changanya , chokaa, chumvi na majivu ya mifupa pig mix vizuri - huu utauita mchanganyo Na.1
HATUA YA PILI:
Changanya mchanganyo huo na damu pamoja na samaki waliosagwa - huu utauita mchanganyo Na. 2
HATUA YA TATU:
Mchanganyo Na.2 uchanganye na mashudu vizuri ambao utauita mchanganyo Na.3.
HATUA YA NNE:
Mchanganyo Na.3 umwage juu ya rundo la pumba iliyochanganywa (pumba ya mahindi na pumba laini ya mpunga).
o Chukua beleshi /koleo safi lililo kavu na kulitumia kuchanganya rundo la chakula ili kusambaza viinilishe vizuri.
Mambo ya kuzingatia katika kulisha na kutunza chakula cha kuku:
a) Baada ya kuchanganya chakula kitawekwa kwenye viroba
au magunia na kutunzwa ghalani (stoo) hadi pale kitakapohitajika kwa
ajili ya kulisha kuku.
b) Hakikisha kuku wanapata lishe kadri inavyopendekezwa na wataalamu.
c) Chakula kilichochanganywa ni lazima kiwekwe sehemu
kavu ili kisiharibiwe na unyevunyevu kama vile kwenye chaga mabanzi
yaliyotandazwa juu ya mawe yalipangwa vizuri
d) Chakula kilichoharibika hakifai kulisha kuku kwani kinaweza kusababisha matatizo ya afya.
d) Chakula kilichochanganywa kinatakiwa kisikae muda mrefu baada ya kutayarishwa.
Vyakula vya ziada:
Ili kuhakikisha kwamba kuku wanapata viinilishe vya kutosha kuku wanaweza kupewa mchwa na mafunza.
Vilevile vitu mbadala aina ya nafaka vinavyopatikana hutegemea sana aina ya mazao yanayolimwa katika eneo husika.
Mbinu za kuotesha mchwa na funza: Funza
na mchwa ni chakula kizuri na rahisi chenye viinilishe aina ya protini
kwa kuku wanaofugwa kwa mfumo huria unaoboreshwa. Hata hivyo vyanzo hivi
vya chakula cha protini huchangia tu vile ambavyo kuku wanatakiwa
kupewa.
a. Inashauriwa uwape vifaranga hao funza na mchwa kwa sababu ndio wanaohitaji protini kwa kiasi kikubwa na cha kuaminika.
Funza na mabuu yanaweza kuoteshwa kwa njia rahisi na kutumika kuboresha chakula cha vifaranga.
c) Mafunza na mabuu yanaweza kuoteshwa kwa
kutumia damu, viungo vya ndani ya tumbo la ng’ombe pamoja na samadi ya
ng’ombe.
d) Chungu kijazwe maji theluthi moja ya ujazo wake,
inzi watakuja na kutaga mayai katika mchanganyiko ambao mafunza
walioteshwa wataanza kula mchanganyiko huo.
e) Baada ya hapo vitu hivi vyote vitachanganywa
pamoja katika chungu kimoja kikubwa ambacho kitaachwa wazi wakati wa
mchana na kufunikwa wakati wa usiku.
f) Siku tano baadaye maji yatajazwa kwenye mtungi
huo na mafunza yatakusanywa wakiwa wanaelea juu. Baada ya kukusanya
waoshe vizuri na maji halafu lisha kuku moja kwa moja.
g) Kumbuka kuweka chungu kinachooteshwa mafunza kuweka mbali na maeneo ya watu ili kuepuka harufu inayoweza kusumbua watu.
Makadirio ya chakula cha kuwalisha vifaranga 100/siku moja:
Umri (wiki baada ya kuzaliwa)
|
Idadi ya
vifaranga
|
Kiasi kinachotakiwa
Kwa siku moja(kilo)
|
1
|
100
|
1
|
2
|
100
|
1
|
3
|
100
|
2
|
4
|
100
|
3
|
5
|
100
|
4
|
6
|
100
|
5
|
Maelezo kwa ufupi kuhusu kulisha kuku:
Ni
vigumu kukadiria mahitaji ya chakula cha kuku wanaojitafutia chakula,
lakini inakadiriwa kuwa kuku mmoja mkubwa wa uzito wa kilo 1-2 anahitaji
chakula chenye uzani wa gramu 80-160 kwa siku kwa kuku wanofugwa ndani
lakini wale kuku wanafugwa kwa mfumo wa huria nusu huria mahitaji
yanakadiriwa kupungua hadi kufikia gramu 30-50 kwa siku .
Ifahamike
pia kuwa kiasi cha chakula hutegemea mahitaji kutokana na uzito na
uzalishaji, mfano kuku anayetaga na anayekua wanahitaji chakula kingi
zaidi ya wale ambao hawatagi au wamekoma kukua.
Hakikisha kuku wanawekewa chakula na maji safi kwenye vyombo safi na kubadilisha kila vitakapoisha.
0 comments:
Post a Comment