script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Turkey
MAGONJWA YA KUKU, DALILI, KINGA NA TIBA Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:
Newcastle/ Kideli
Gumboro
Homa ya matumbo/fowl typhoid
Ndui ya kuku/ fowl pox
Ukosefu Wa Vitamin A
Kuhalisha damu/coccidiosis
Minyoo
Wadudu kama viroboto,Utitiri na chawa
Mafua ya kuku

1. NEWCASTLE (KIDELI)

Ugonjwa huu ndio huathiri kuku na kusababisha hasara kubwa. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.
Dalili
Kuhalisha choo cha kijani na njano
Kukohoa na kupumua kwa shida
Kuficha kichwa katikati ya miguu
Kukosa hamu ya kula na kunywa
Kutoa kamasi na machozi
Kupooza na kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
Idadi kubwa ya vifo hadi 100%
Kinga
Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
Epuka kuingiza kuku wageni
Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
Zingatia usafi wa mazingira
2. GUMBORO
Ugonjwa wa gumboro hudhoofisha kinga ya mwili ya kuku ambao hutokea kati ya umri wa majuma mawili na miez miwili na huleta vifo zaidu ya asilimia hamsini.
Dalili
-kuku hujikunyata, hushusha mabawa na kuvimba kichwa.
-maranyingi kuku huarisha mharo mweupe ulio na ulenda kitu kama (milendalenda).
-kama utawachinja kuku waliokufa chini yangozi wanakuwa na vidonda vya michipuko hasa mapajani.
-vifo hutokea kwa wingi kuku hulaliana kutokana na kusikia baridi pia kwa kukosa maji mwilimi kutokana na kuharisha.
Kinga
Ni vyema chakula cha vifaranga wa kuku wa mayai kiwe na dawa aina ya Coccidiostants wakati wa malezi.
Vifaranga wapewe chanjo kati ya umri usiopungua wiki mbili na kurudiwa baada ya wiki mbili.
Tiba
Ugojwa huu hauna tiba bali unatakiwa uwape kuku wako chanjo kila baada ya umri wa wiki mbili na na kila baada ya miezi mitatu.
3. FOWL TYPHOID {HOMA YA MATUMBO}
Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
Kuku hukosa hamu ya kula
Kuku hukonda
Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
Kinyesi hushikamana na manyoya
Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga
Usafi
Fukia mizoga
Usiingize kuku wageni
Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6
4. FOWL POX { NDUI YA KUKU}
Ndui huathiri sana vifaranga wanaokua hasa wakati wa mvua, Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hauna tiba
Dalili
1) Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana kama kishungi,usoni na chini ya mdomo
2) Kukosa hamu ya kula
3) Vifo vingi
Kinga
• Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
• Epuka kuingiza kuku wageni
• Zingatia usafi wa mazingira
5. VITAMIN A DEFICIENCY {UKOSEFU WA VITAMIN A}
Huathiri zaidi kuku wadogo wanaokua, macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowa maji, kuku wenye ukosefu wa vitamin A hawaponi na hatimaye hufa.Mara kwa mara ugonjwa hujitokeza wakati wa kiangazi,kinga ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara pia wape kuku wote dawa ya vitamin za kuku zinazouzwa maduka ya mifugo ili kuzuia
6. COCCIDIOSIS {KUHALISHA DAMU}
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili
• Kuharisha damu
• Manyoya husimama
• Hulala na kukosa hamu ya kula
7. WORMS {MINYOO}
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutibu minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya nipiperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur audawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu
8. WADUDU KAMA VIR
[17/10, 11:42 a.m.] Mr Bathuel Msafiri (Jahazi La Kuku): MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE
Published Under kilimo
Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu
No 1: NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.
No 2: GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe kama chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na kama matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NO 3: MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukakamaa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.
NO 4: NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya kama vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic kama Otc 20%.
No 5 MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za  uso, kichwa  na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au  Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.
No 6: FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.
NO 7 COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
_Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.
NO 8: FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.
NO 9 MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
_Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.
Kama utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo kama utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi

................................................................................................................................................

0 comments:

 
Top