script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




https://www.mshindoveterinarycentre.com



MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA KUFUGA NG’OMBE WA MAZIWA
  : Kwa kawaida unapotaka kufuga ng’ombe wa maziwa unakuwa na malengo mawili makubwa yafuatayo:

• Kuongeza kipato ili kukidhi mahitaji ya kifedha na ya familia, pamoja na kuweza kuweka akiba ya uzeeni.

• Kuwa ufugaji huo ndiyo kazi yako itakayokuridhisha, na kupendwa kuitwa mfugaji.

Ufugaji wa ng’ombe wa maziwa inayoendelea na inayorithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine, unahitaji kuzingatia mambo muhimu yafuatayo:-

• Kama unazo sifa zinazohitajika kuwa mfugaji wa ng’ombe wa maziwa

• Kama unazo nyenzo muhimu kwa ufugaji huo.

• Aina gani ya ufugaji kulingana na nyenzo na matakwa yako mwenyewe; na

• Jinsi ya kuanza kufuga.

Ni muhimu sana kupata aina nzuri ya ng’ombe kwa uzalishaji wa maziwa

SIFA ZA KUWA MFUGAJI STADI

• Kuyaelewa na kuyaheshimu mazingira yote yanayohusika katika kufanikisha ufugaji wa ngombe wa maziwa .
• Kuwa na shauku ya kutaka kujifunza wakati wote na kuwa na mwamko wa kibiashara:

• Kukiri kwamba ufugaji ndiyo mfumo wako wa maisha na msingi wa kipato chako.

• Kukubali kujituma na kuitumia akili yako pamoja na kukubali hasara (personal sacrifices) hasa katika miaka ya mwanzo.

• Epukana na kujiamini sana na kuwa na matarajio yasiyowezekana, hasa katika viwango vya uzalishaji, bei ya maziwa, faida kubwa. Haya yanaweza kukukatisha tamaa mapema!

• Kuwa na uzoefu, uwezo wa kutumika taaluma unayopata. Uzoefu unamsaidia mfugaji kuwa na mawazo na matarajio yaliyo sahihi.

• Uwezo wa kudhibiti rasilimali ng’ombe, ardhi, pesa na watu. Mara nyingi mtaji wa kuanzisha ufugaji huwa ni wa kukopa, kwa hivyo udhibiti wa rasilimali ni muhimu sana.

• Kuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo yeyote yatakayojitokeza katika uendeshaji wa kazi hii.

Katika ufugaji mzuri hakikisha kunakuwepo malisho stahiki na ya kutosha.

NYENZO ZINAZOHITAJIKA

Nyenzo muhimu zinazohitajika kuanzisha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na ambazo huhitaji mtaji mkubwa ni hizi zifuatazo:

• Ng’ombe mzuri kwa kutoa maziwa

• Ardhi itakayofaa kwa kustawisha chakula cha mifugo.

• Majengo na zana zinazostahili.

• Fursa za soko la maziwa.

Kwa kawaida wafugaji wengi huanza kwa kununua ng’ombe na kujenga mabanda yanayohitajika na kuacha kuwekeza katika ardhi (kwa ajili ya malisho) na kuandaa mfumo wa soko. Matokeo yake wafugaji huingia gharama kubwa ya kuwapatia chakula ng’ombe wao na kukosekana kwa soko la uhakika la maziwa. Uwekezaji katika nyenzo zote hizi ni muhimu. Inakadiriwa kuwa ng’ombe mmoja anahitaji mtaji kati ya Tshs.2,000,000/= hadi Tshs. 4,000,000/= ikiwa nyenzo zote muhimu zitajumlishwa wakati wa kuanzisha ufugaji.

Kuwa na mipango mizuri ya majengo na ardhi kutaongeza tija na ufanisi katika ufugaji. Vema kupata ushauri wa kitaalamu..

AINA ZA UFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA

• Kuamua ni aina gani ya ufugaji itategemea;-
• Mapendezo ya mfugaji mwenyewe
• Mtaji na nyenzo alizo nazo mfugaji
• Mfumo wa masoko

Kuna aina zifuatazo za ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kulingana na vigezo vya hapo juu

• Aina ya kwanza ni ufugaji wa ng’ombe waliosajiliwa, na uzawa wao (lineage) unaweza kupatikana kupitia jumuiya za wazalishaji kwa madhumuni ya kuuza MAZIWA, MITAMBA na MADUME ya mbegu.

• Ufugaji wa aina hii huhitaji mtaji mkubwa ili kuweza kupata mbegu bora, na yenye afya nzuri. Mapato yatokanayo na mauzo ya ng’ombe na maziwa huwa ni makubwa. Kwa kawaida wafugaji wa aina hii hulazimika kusajiliwa katika jumuia za wafugaji hawa baada ya kutimiza masharti. Kwa mfano, nchini Marekani kuna jumuiya 6 za wafugaji hawa kulingana na kabila sita za ng’ombe wa maziwa kama ifuatavyo;-

(a)The Ayshire Breeders Association; Brandon, Vermont 05733. Journal- THE AYSHIRE DIGEST.

(b)The brown Swiss Cattle Breeders Association; 800 pleasant St. Beloit, Wisconsin 53511. Journal- THE BROWN SWISS BULLETIN.

(c) The American Guernsey Cattle Club; 70 Main st. Peterborough, New Hampshire 03458. Journal- THE GUERNSEY BREEDERS JOURNAL.

(d)The Holstein- Fresian Association of America P.O.Box 808 Brattleboro, Vermont 05301; Journal- HOLSTEINFRIESIAN WORLD.

(e)The American Jersey Cattle club; 2105- J.S. Hamilton Rd; Columbus, Ohio 43205. THE JERSEY JOURNAL.

Ufugaji wa ng’ombe ambao wanazo sifa za kabila (Breed) fulani la ng’ombe wa maziwa lakini usajili na uzawa wao (lineage) havijulikani. Ni rahisi kwa mfugaji kuanza na ng’ombe wa aina hii kwa vile hawahitaji mtaji mkubwa. Hata hivyo, mapato huwa madogo.

UFUGAJI WA MAKOO PEKEE:

Katika mfumo huu, mfugaji huweka makoo pekee na hununua mitamba yenye mimba wakati wa kubadilisha. Mfumo huu hupunguza gharama, hasa za kununua ardhi, ng’ombe, zana na vifaa wakati wa kuanza. Kasoro kubwa ya aina hii ya ufugaji ni pale mfugaji anapokosa chanzo cha kupata mitamba iliyo bora.

UFUGAJI WA MAKOO PAMOJA NA NDAMA
Katika aina hii, mfugaji huweka makoo na ndama wote wanaozalishwa kwa ajili ya kukuzwa ili wawe mitamba ya kubadilisha na makoo walio wazee, wenye kutoa maziwa kidogo na wenye matatizo mbalimbali. Faida ya mfumo huu ni pale mfugaji anapokuwa na uwezo wa kukuza mitamba mizuri yeye mwenyewe na kuweza kuitumia kuendeleza na kuongeza uzalishaji wa maziwa. Tatizo kubwa ni mahitaji ya ziada ya chakula ndama hadi anapokuwa mtamba.

Mfugaji kuzalisha mwenyewe chakula chote (hasa nyasi) kinachohitajika. Faida kubwa ya aina hii ya ufugaji ni uhakika wa kuwa na chakula bora (forage) kwa ajili ya mifugo wakati wote. Vilevile, kama mfugaji anatumia mbinu bora za kilimo, basi gharama huwa ndogo sana katika uzalishaji wa nyasi na majani.

Mapungufu makubwa ya mfugaji kuzalisha chakula mwenyewe ni mahitaji makubwa ya mtaji wa kuanza kwa ajili ya ardhi ya kutosha, zana huduma ya wataalam na malipo ya vibarua. Wakati mwingine ardhi inaweza kuwa taabu kupatikana.

Ufugaji wa aina hii ndiyo mara nyingi unapendekezwa kwani hutoa matumaini ya mafanikio. Kwa wafugaji wenye ng’ombe kidogo (5-10), hushauriwa kutumia kilimo mseto ili kuweza kutumia mabaki ya shambani kulishia mifugo.

Mfumo huu ulifanikiwa sana kule Zanzibar katika miaka ya 80 kwa msaada wa programu ya chakula duniani (World Food Program)

MFUGAJI HUNUNUA CHAKULA CHOTE KINACHOHITAJIKA KWA MIFUGO

Mfumo huu huondoa yale mahitaji makubwa ya kifedha wakati wa kuanza, pamoja na kupunguza muda unaohitajika kwa uzalishaji na utunzaji wa malisho.

Hata hivyo mapungufu yake mara nyingi ni kule kutopata malisho ya kutosheleza na yaliyo bora. Vilevile gharama ya ununuzi na usafi rishaji mara nyingi kujiandaa vizuri.

VIPI UANZE

Kuna aina nyingi za kuanzia, lakini la msingi ni kujiandaa vizuri. Katika sifa, mfugaji anahimizwa kuwa awe anahamasika, awe mvumilivu, mchapakazi na aweze kuzikubali hasara zinapotokezea.

Katika kupanga, lazima mfugaji awe na makisio yanayokubalika. Asiwe na pupa katika suala la mikopo ya kuendeleza mifugo, malisho, uzalishaji, uzazi, afya na kadhalika. Vilevile anapaswa kuwa na bajeti ya kila mwaka. Mfugaji anapaswa kupanga matumizi ya mtaji kwa mujibu wa umuhimu kama;-

• Ununuzi wa ng’ombe wenye kutoa maziwa kwa wingi.
• Ununuzi wa ardhi kwa ajili ya malisho
• Kugharamia mfumo wa mauzo ya maziwa
• Ununuzi wa zana na vifaa vinavyotakiwa.
Njia za kumpatia fedha za mtaji zinaweza kutokana na kukusanya akiba polepole kutokana na kazi nyingine, kukopa baada ya kutayarisha mchanganuo unaokubalika.

Kupata mchango wa kifamilia au vyama vya kuweka na kukopa. Kama umekusudia kudumu katika ufugaji, unaweza kutumika mtaji mdogo ulio nao kununulia nyenzo muhimu na kukodi nyenzo nyingine hadi ufi kie lengo ulilolikusudia.

Zingatia kwa makini somo hili kisha jadili yafuatayo:-

• Kama wewe ni mfugaji tayari, unafi kiri ni jambo gani lingefaa kutangulia kati ya kujijengea sifa za kuwa mfugaji, au kuwa na mtaji wa kununulia nyenzo muhimu zinazokubalika? Kwa nini?

• Ni matatizo yapi yanayokukabili katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa? Yataje pia pendekeza njia za kuyatatua

....................................................................................................................................................................



0 comments:

 
Top