RATIBA YA CHANJO KWA VIFARANGA MAPAKA KUKU WAKUBWA
SIKU 1.
Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa
muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa
vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa
vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus
Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe
2. SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii
huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa
vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga
mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au
kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa
vitamini
3. SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika
maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo
vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu
unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti
vyekundu kama hapo pichani
4. Siku ya 21 (wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri)
5. SIKU 28 (Mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
6. SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.
7. WIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa
mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi
hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8. WIKI YA 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle
...........................................................................................................................................................
...........................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment