UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI WENYE TIJA
Safari
yangu ilianza baada ya kukutana na mhamasishaji aliyenitia chachu
kwamba 10 x10 x 10 you become a millionea! Kwamba ukianza na kuku 10
kila mmoja akazaa 10 na hao watoto na mama zao wakazaa kila mmoja 10
unakuwa millionea! Wakubwa kuongea ni rahisi utekelezaji ukawa mgumu
sana!
Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha
vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na
kukupa kipato cha uhakika!
Safari
ya ufugaji niliianza kwa kununua mitetea 30 na jogoo watatu! Ilibidi
nisubiri muda hadi kuku waanze kutaga! Muda ukafika kuku wakaanza kutaga
kwa fujo sana! Nilikuwa na banda moja tu ambamo kuku wote walikuwa
wakilala humo. Nilitengeneza viota vingi kwa ajili ya kuku kutagia.
Asubuhi nilikuwa nawafungulia! Changamoto nilizoanza kupambana nazo
kwanza kama mjuavyo kuku tofauti walikuwa wanataga kwenye kiota kimoja!
Ilipofika wakati wa kuatamia ikawa kila kwenye kiota kimoja kuna kuku
kadhaa wamebanana wanaatamia! Hali hii haipaswi kutokea kwani kuku mmoja
anaweza kuwa amejilundikia mayai mengi ambayo hawezi kuyapajoto la
kutosha na kuku mwingine anakuwa amekaa kando tu hana hata yai moja. Hii
ilibadilika ikawa kero kubwa! Nilijua utotoaji unaweza kuathirika sana!
Ili
utotoreshe vifaranga vingi kwa wakati mmoja badala ya kutumia
incubator, tumia hao hao kuku. Wakianza kutaga kila siku okota mayai na
kuyahifadhi mahali salama ili kuku wasiyatie joto! Kuku wengi wanapotaga
kwa pamoja hufikia wakati mayai huishatumboni unakuta wamelala kwenye
viota wakiwa wameatamia mayai yaliyopo au udongo tu! Kuku anaekuwa
amefikia kuatamia utamjua kwani ukimshitua haondoki kwenye kiota. Kuku
anaetaga ukimshitua hukimbia! Kwa hiyo kama nimepanga kutotolesha
vifaranga 100 kwa mara moja nikishagundua kuwa kuna kuku 8 wameanza
kuonesha dalili ya kuatamia hapo husubiri usiku ninawawekea mayai
amabayo nilikuwa nimeyahifadhi. Ambapo mimi huwekea kila kuku mayai 15.
Kwa hiyo kuku 8 hufanya jumla ya mayai 120.
Kwa
kuwa banda langu ni hilo moja tu kuku wengine wanaoendelea kutaga
walikuwa wanaendelea kutagia kwenye viota ambavyo kuku wengine walikuwa
wanaatamia! Hali hii ilikuwa inaleta tabu sana kwani ilikuwa si rahisi
kutambua mayai mapya na yenye siku nyingi. Kuondoa shida hii nilinunua
MARKER PEN (rangi yoyote) na siku ya kuwawekea mayai kuku ili waatamie
niliyachora mduara kuzunguka yai ili iwe rahisi kuyatambua mayai mapya.
Huo mchoro hauwatishi kuku na hakuna dosari yoyote. Kwa hiyo kila siku
jioni ninapokuja kuokota mayai yaliyotagwa nilikuwa pia nakagua kila
kiota cha kuku walioatamia na kuondoa mayai mapya. Kumnyenyua kuku
anaeatamia na kuondoa yai haileti shida yoyote!
Kuku
akifikia wakati wa kuatamia ukamnyima mayai hawa wanatabia kuendelea
kung'ang'ania kuatamia, hapo ilibidi kutengeneza JELA! Watu wengine
wanambinu tofauti kumwachisha kuku asiatamie! Mbinu ya kumtia kuku
stress inafanya kazi nzuri sana! Jela inaweza kuwa ni Tega, au Box kubwa
au chumba kidogo kilichopo. Ukimfungia kuku JELA bila maji wala chakula
kwa kutwa mbili siku ukimfungulia akili yake huwa ni kutafuta chakula
tu hakumbuki kurudi kwenye kiota! Njia hii ilifanikiwa sana na ilifanya
kuendesha shughuri zangu bila bughudha! Kuna wakati JELA ilikuwa na kuku
kibao hivyo unapaswa kutengeneza kibanda cha JELA. Hawa kuku wakitoka
JELA hutaga mapema sana amabapo bila hivyo wangekuwa wanaatamia.
Pia
kuku wakishaatamia kwa muda wa siku 10 nilikuwa nayapima mayai ili
kubaini kama kuna mayai yasiyoweza kuanguliwa! Ni rahisi sana kama una
Tochi! Ukimulika yai Kwa kulizungushia vidole kiganjani kama ni yai zima
linakuwa na giza kama ni yai bovu linapitisha mwanga kama yai
lililotagwa siku hiyo! Jinsi ya kuzungushia vidole yai, tengeneza duara
kwa vidole vyako na dole gumba kisha pachika yai katikati ya duara ili
mwanga wa tochi upenye kwenye yai! Kwahiyo unaweka tochi inayowaka chini
ya yai na hii ifanyike gizani au ndani ya chumba chenye mwaga mdogo.
Kadri ya yai linavyokaribia kutotolewa ukilimulika huwa na giza zaidi!
Ukimulika mayai toa mayai yasiyoweza kutotolewa maana hayo hutumia joto
la Mama bure!
Bado
ntaendelea kuwaletea makala hii kuhusu ufugaji kuku bado sijamaliza
nimeona niwarushie hii kwanza kwa kuanzia. Mwenzenu nilikuwa nahangaika
kufukia tanuru la mkaa nimekuta limefunguka! Si mnajua maisha jamani!
Vijana tuamke na kujiingiza katika miradi hii soon tutaona mabadiliko
.........................................................................................................................................................................................
Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na kukupa kipato cha uhakika!
.........................................................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment