script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




https://www.mshindoveterinarycentre.com
Athari za upungufu wa virutubisho kwenye chakula cha mifugo

- Kudumaa.
- Kupungua uzito,
- Kulemaa viungo
- Kuvunjika mifupa kwa urahisi
- Kutaga mayai yenye ganda laini,
- Kutaga mayai machache,
- Kutoata manyoya yakutosha.
- Kunyonyoka na kujikunja manyoya.
- Kujaa kwa tumbo, kifua na ngozi.

Tiba:
 Athari zinazotokana na upungufu wa
virutubishi zinaweza kurekebishwa kwa
kuwapa kuku virutubishi vilivyopungua
katika chakula.

Kinga:
Kuwalisha chakula kilicho na
mchanganyiko wenye uwiano sahihi
katika wanga, protini, vitamini, madini
na maji ya kutosha.


Athari zinazosababishwa na wadudu

Kudhibiti
Viroboto, Papasi, chawa
na utitiri
Uchafu, hasa
vumbi ndani ya
banda la kuku.
Viroboto hujificha
na kuazaliana katika
vumbi.
Kama hapo juu
Wadudu weusi
huonekana
wanamshambulia
kuku kwenye
kishungi, kichwani,
na uso kwa ujumla.
Wadudu wadogo
wengi husambaa
katika mwili mzima
wa kuku hunyonya
damu.
Tunza usafi wa
banda. Nyunyizia
dawa za kuua
wadudu katika
banda. Kwa mfano
Akheri powder au
Servin.


Dalili za Ugonjwa wa minyoo Kinga
Tiba
Athari zinazosababishwa na Minyoo
- Kudumaa.
- Kuku anakuwa mwepesi au
kupungua uzito.
- Kukohoa.
- Kukonda
- Kupauka sehemu sisizo na
manyoya kama upanga,
ndevu masikio na macho.
- Utagaji wa mayai hupungua
au kusimama kabisa.
- Kuharisha.
- Minyoo inaweza kuonekana
kwenye kinyesi.

Tiba:
 Minyoo inaweza kutibika kwa kutumia
madawa mbali mbali kama itakavyoshauriwa na
mtaalam wa mifugo.
 Kinga:
Kusafisha vyombo vya chakula na vya
kunywea maji kila siku kwa kutumia maji na
sabuni au dawa za kuua wadudu.
- Kutenganisha kuku wakubwa na wadogo.
- Kubadilisha matandazo kwenye sakafu kila
baada ya miezi mitatu.
- Kuzingatia usafi wa banda.
- Kuwapa dawa ya kuzuia aina nyingi za minyoo
kila baada ya miezi mitatu.

Kumbuka 
Usafi Ni _Kinga_ Kubwa Sana Ya Kudhibiti Magonjwa Kwa Mifugo Yetu

0 comments:

 
Top