SUNGURA ni
wanyama wastahimilivu wa mazingira mbalimbali kiasi cha kushindwa kuugua ovyo
kama ilivyo kwa wanyama wengine wa kufuga, lakini wanyama hawa ni laini, kiasi
ambacho wanaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa yanayochanganya,
hata kama watatunzwa vizuri namna gani.
Kama ilivyo
kwa hali yoyote ambayo inaweza kuwaathiri sungura wako au mnyama mwingine wa
kufugwa, kulitambua tatizo mapema na kulishughulikia haraka kwa kuwatibu linaweza
kuleta mabadiliko makubwa kuhusu kuishi kwa sungura wako na kupona kabisa.
Sungura siyo
wanyama wanaokula nyama wala si wanyama hatari na mara nyingi wako hatarini
kuliwa na wanyama wengine.
Kwa sababu ya
hali hiyo, sungura pia wanaweza kupatwa na maumivu au ugonjwa, na kuonyesha
dalili ambazo zinaweza kuwa ishara kwa wanyama hatari kuwashambulia.
Ninazungumzia kuhusu asili yao ya kuishi porini n ahata unapowafuga.
Hii
inamaanisha kwamba ni vigumu kwetu kama wafugaji wa sungura kubaini kwa urahisi
wakati mambo yanapokwenda mrama, na kujifunza kuhusu baadhi ya dalili za mwanzo
za tatizo kunaweza kuwa changamoto ya kujifunza kwa undani.
Yafuatayo ni
baadhi ya matatizo ya msingi yanayowapata sungura ambayo yanaweza kuwa vigumu
kuyatambua katika hatua za mwanzo, na jinsi ambavyo unaweza kuyagundua
0 comments:
Post a Comment