Utambuzi wa mwanzo wa
magonjwa ya mifugo
Sifa za mnyama mwenye afya
i.
Mchangamfu wakati wote macho maang’avu huku mkia na masikio vikimsaidia
kufukuza
inzi
ii. Kula na
kucheua, kunywa maji vizuri kila siku
iii.
Kuonyesha ushirikiano na kutembea pamoja kwenye kundi
iv.
Kutembea vizuri
v. Anastuka
na kukimbia anapostuliwa na mnyama hatari anapomkaribia kama vile
mbwa mwitu,
fisi, chui, simba.
vi. Mwili
wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya
kutosha
kama vile maziwa.
vii.
Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukuna wanaongezeka
uzito kwa
muda mfupi
viii. Kwa
mnyama anayekamuliwa mara kwa mara kupiga kelele za kumtafuta mtoto
wake,kiwele
huwa kimejaa maziwa, chuchu huwa wakati mwingine zimetanuka
upande kwa
ajili ya kujaa maziwa
ix. Ngozi
ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wapomtambaa
x. Kwa
madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
Miili yao
hujengeka vizuri. Pumbu hujengeka na kukaa vizuri kwenye nafasi yake
(yaani
katikati ya miguu)
xi. Pua na
midomo huwa na unyevu unyevu wakati wote.
xii. Ngozi
kuwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung’aa.
xiii. Kwa
kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka
Dalili za Mnyama anayeumwa
i. Hukosa
hamu ya kula na kunywa maji
ii. Mwili
kunyong’onyea na kuonekana mchovu
iii. Mnyama
kutembea pole pole na kwa taabu na mara nyingi hujitega na wenzake
iv. Pua
zake na midomo huonekana kukauka.
v.
Kupunguka kwa kiwango cha uzalishaji kama vile maziwa. Kwa madume huduwaa
na
kuinamisha shingo chini na kukosa hamu ya kuwapanda majike wanaoingia
kwenye
joto.
Vyanzo vya magonjwa
Magonjwa
mengi ya mifugo husambazwa na vijidudu ambao huingia kwenye mfumo wa
damu na
kusababisha homa na baadae madhara makubwa. Mangonjwa mengi ya mifugo
husababishwa
na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mfano mazingira machafu
anayoishi
mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (Vitu vyenye ncha kali) husababisha
vidonda
ambapo vimelea vinaweza kukaa.Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana
na hali za
ndani ya mwili kama upungufu wa lishe, mfano: madini, na na magonjwa ya
kulithi.
19
Mfano wa
wadudu hao ni;
Vimelea (bacteria)
Mfano wa
magonjwa yanayosababishwa na bacteria ni chambavu, Blackquarter, Kimeta,
Kifua kikuuu,
brucellosis (ugonjwa wa kutupa mimba) na ugonjwa wa kiwele.Ng’ombe
dume
huvimba mapumbu.
Virusi (virus) Otatis
Mfano wa
magonjwa yanayosababishwa na virusi ni kichaa cha mbwa (Rabies), Ugonjwa
wa
midomo,miguu (foot and mouth disease) na Sotoka (Rinderpest)
Protozoa
Magonjwa
yanayo sababishwa na protozoa ni kama ndigana baridi, ndigana kali, ndigana
mkojo damu,
ndigana maji moyo na nagana.
Angalizo:
Magonjwa
yote ya Ndigana husambazwa na makupe, wakati ugonjwa wa nagana
husambazwa
na ndorobo.
Lishe duni
Upungufu wa
viinilishe katika chakula cha mifugo husababisha madhara katika mwili kama
ifuatavyo;
i.
Husababisha majike kutopata joto mapema
ii. Ndama
kuzaliwa na viungo visivyo komaa
iii.
Upungufu wa uzalishaji maziwa
iv. Kiwango
cha uzalishaji kushuka
Vidonda/michubuko
Kupitia
vidonda au michubuko, wadudu wasababishao magomjwa huweza kuingia mwilini
kwa mnyama
Magonjwa
ya kurithi
Kama mmoja
wa wazazi ana ugonjwa wa kurithi basi kuna uwezekano mkubwa kwa
mmoja wa
ndama watakaozaliwa kurithi ugonjwa huo
Magonjwa yanayoenezwa na kupe
Ndigana kali
Dalili zake
i. Homa
kali hadi nyuzi joto 42c
ii. Povu
kutoka mdomoni na puani
iii. Kuhara
choo kilichochanganyikana na kamasi na damu
iv. Tezi
kuvimba sana na zenye joto
v. Kuacha
kula
vi. Ukungu
kwenye macho
vii. Kifo
baada ya wiki moja hadi mbili
Tiba
Butalex,
Parvexon, tiba iambatane na sindano moja ya kuondoa uvimbe kwenye mapafu
kama hali
hiyo tayari imeshajitokeza. Tumia Multivitamin ili kuongeza hamu ya kula na
Raxis ili
kuondoa maji kwenye mapafu.
Kinga/zuia
Zingatia
uogeshaji sahihi na Chanjo ya ECF
Ndigana baridi (Anaplasmosis)
Dalili zake
i. Homa
hadi nyuzi joto 42C
ii. Kukosa
hamu ya chakula
iii. Choo
kigumu na makamasi na harufu mbaya
iv. Kifo
baada ya siku 8 hadi 10
Tiba
i.
Antibiotic kama vile Oxytetracycline
ii. Imizol.
Kinga
Zingatia
uogeshaji sahihi
21
Ndigana
mkojo damu (Babesiosis) ugonjwa wa kukojoa damu
Dalili zake
i. Mkojo
kuwa na rangi ya damu isiyokolea zambarau
ii. Mkojo
hutoka kidogo kidogo na kwa muda mrefu
iii. Homa
hadi nyuzi joto 40C
iv. Kuacha
kula
v. Choo
kigumu au kuhara wakati mwingine
vi. Kifo
baada ya wiki 1
Tiba
Berenil
ikisaidiwa na antibiotics za sindano kama vile oxytetracycline (OTC) pia tumia
Multivitamin
kuongeza hamu ya kula.
Kinga
Zingatia
uogeshaji sahihi
Ndigana maji moyo (heart water)
Dalili zake
i.
Kizunguzungu na kuanguka,
ii. Kifo
baada ya siku 2
Tiba
Antibiotics
za sindano kama vile oxytetracycline.
Kumbuka
tiba lazima ifanywe mapema
iwezekanavyo
Kinga/kuzuia
0 comments:
Post a Comment