asiyetaga au asiyezalisha na kumuondoa kwenye kundi la kuku wako wa mayai kwa kumchinja, kumuuza au kwa matumizi mengine ya nyumbani.
Kupunguza hasara za kupoteza chakula na dawa kwa kuku wasiozalisha (wasiotaga)
Kuwapa nafasi kuku wanaozalisha (wanaotaga)
Kupunguza uwezekeno wa magonjwa pamoja na matatizo kama kudonoana na kula mayai.
Kuna aina mbili za kufanya CULLING
- Kumuondoa kuku wakati wa ukuaji pale wanapokaribia kuwapeleka kwenye nyumba ya kutagia (Laying house).
kuku wa kuwaondoa ni wale wadogo kuliko wenzake, wenye vilema (deformities) kwenye midomo, miguu na mabawa, wenye majeraha maana wataweza kuleta matatizo wajati wa utagaji
- Kumuondoa kuku wakati wakiwa wameshaanza kutaga tayari baada ya wiki 8 au wiki 10 maana kuku watakuwa wameshakua vizuri
Kwa njia hii ya 2 tunaangalia muonekano wa nje wa viungo vya kuku mwenywewe mfano mdomo, macho, rangi ya kilemba, kichwa, kifumbatio, mfupa wa eneo la haja (pubic bone)
FANYA HILI ZOEZI SHABANI MWAKO, Kuna utofauti mkubwa sana kwa kuku anaetaga na asiyetaga kwa kuangalia hizi sifa…
Angalia yafuatayo kwa kuku wa mayai kwenye wiki ya 8 au 10 kuku wakishaanza kutaga tayari
KILEMBA(Comb); Kwa kuku anaetaga kilemba ni kikubwa, kimesimama kidogo, kinang’aa kwa rangi nyekundu…… Kwa kuku asiyetaga kilemba ni kidogo, kimelala na kimepaukaaa
MDOMO (Beak); kwa kuku anaetaga ana mdomo uliopauka (Bleached)….. asiyetaga ana mdomo wa njano (yellow beak)
JICHO (eye); kwa kuku anaetaga linang’aa alafu limejaa kwa kutokeza njee kidogo (prominent)…. kwa asiyetaga jicho limepauka na limedumbukia ndani kidogo (sunken eye).
TUMBO (Abdomen); kubwa kwa kuku anaetaga alafu ni laini….. kwa kuku asiyetaga ni ndogo alafu ngumu kidogo.
SEHEMU YA HAJA (vent); kwa kuku anaetaga vent ni kubwa, ina unyevu na imepukaa (bleached)….. Kwa kuku asiyetaga vent ni ndogo, kavu na ina rangi ya njano.
MFUPA KATIKA ENEO LA VENT (Pubic bones); kwa kuku anaetaga hiyo sehemu imachia nafasi unaweza kuweka vidole zaidi ya 3 vya mkono…. kwa kuku asiyetaga hili eneo ni dogo na kidole kimoja tu au 2 vinaruhusiwa.
KICHWA (Head); kuku anaetaga kichwa kimekaa katika mkao mzuri (neat) na kipo imara…. kuku asiyetaga kichwa kimelegea
............................................
0 comments:
Post a Comment