HOMA YA MAPAFU KWA MBUZI I Mshindo Media
HOMA YA MAPAFU KWA MBUZI : Ugonjwa huu kitaalam hujulikana kitaalam kama Contagious Caprine Pleuropnemonia. Ugonjwa huu husababishwa na husababishwa na vimelea vya bakteria waitwao Mycoplasma mycodes var capri.
• Ugonjwa huu huenea kwa njia zifuatazo:
– Kuvuta hewa yenye vumbi iliyochanganyika na vimelea hao-droplet nuclei kutoka nje ya banda (upepo).
– Kuvuta hewa yenye vijidudu ndani ya banda:-
• Mnyama mgonjwa ambaye hajatambulika mapema
• Kugusana na mnyama mgonjwa (direct contact)
VIUNGO HUSIKA: MAPAFU (PNEUMONIA): PLEURA (PLEUTATIS)
DALILI:
– Vifo kwa wingi
– Homa
– Kukohoa
– Kuhema kwa nguvu
– Kutokwa na makamasi puani
– Kuacha kula
– Kutembea kwa shida
Tofautisho: Dalili kadhaa za ugonjwa hufanana na magonjwa yafuatayo:
– Pasteurellosis
– Lungworms
– Ammonia gas vapours
Ili kupata ufafanuzi wa haraka inabidi kufanya uchunguzi baada ya kifo (Post morterm examination) kwa mbuzi waliokufa au kuchimba mbuzi mmoja mwenye dalili za ugonjwa.
Mabadiliko kwenye mapafu na ‘pleura’ yataonyesha kuwa ugonjwa huu CCPP.
Pamoja na hayo inabidi kupeleka sampuli (specimen) ya mapafu, Pleuro section kuchunguzwa maabara kwa uthibitisho zaidi.
KUEPUKA UGONJWA:
– Epuka uingizaji wa mifugo kutoka nje bila kupata ushauri wa madaktari wa mifugo
– Mzunguko wa hewa ndani ya banda uwe wa kuridhisha(cross ventilation).
– Epuka msongamano wa mbuzi ndani ya banda.
CHANJO:
Ugonjwa huu unaweza kukingwa kwa kutumia chanjo ijulikanayo kitaalam kama CCPP vaccines.
TIBA:
Huweza kutibika kwa dawa iitwayo Tylosin 20% injectable solution na vitamini Multivitamin injectable solution.
....................................................................................................
0 comments:
Post a Comment