
Tofauti na ndege wengine au bata
wengine wa kawaida, mfugaji wa bata bukini anaweza kupata kipato kikubwa kwa
haraka na kwa gharama ndogo ukilinganisha na bata wengine.
Kuna aina mbili ya bata bukini ambao
ni weupe na wenye mchanganyiko wa rangi. Hali kadhalika hutofautiana katika
utagaji wa mayai.
Chakula
Ndege hawa wanakula chakula kama wanacholishwa kuku,
wanapendelea kula majani jamii ya mikunde kwa 50% na hawahitaji chakula kingi.
Vifaranga ni lazima wapatiwe lishe kamili hasa protini kwa wingi ili waweze
kujenga mwili, kukua vizuri na kuwa na afya nzuri.
Kwa maana hiyo, vifaranga
wanahitajika kupata walau 20% ya protini kwa wiki mbili za awali na baada ya
hapo waweza kupunguza hadi 15% kulingana na kukua kwao hadi wanapokuwa
wanaelekea kukomaa.
Kama ambavyo mfugaji anaweza
kutengeneza chakula kwa ajili ya mifugo wengine, pia anaweza kutengeneza cha
bata bukini kama ifuatavyo:
Mahitaji
1. Mahindi kilo 10 ( hakikisha hayana dawa)
2. Chokaa kilo 5 (ya kulishia mifugo)
3. Dagaa kilo 10 (wanaotumika kulishia kuku)
4. Mashudu kilo 20.
Utengenezaji na Uhifadhi
Baada ya kupima vyakula hivi kwa usahihi chukua pipa, changanya
vizuri kisha walishe bata kulingana na wingi wao na uhakikishe wanapata chakula
cha kutosha.Vipimo hivi hutegemea wingi wa bata unaowafuga lakini hakikisha
uwiano huo unazingatiwa. Baada ya kutengeneza chakula unaweza kuhifadhi katika
mifuko na kuweka katika eneo lisilokuwa na unyevu.
Kuatamia
Jinsi ilivyotofauti katika idadi ya utagaji wa mayai hivyo
ndivyo uwezo wa kuatamia pia ulivyo. Bata Bukini weupe huatamia mayai 6 na wale
wa rangi huatamia mayai 12
Ndege hawa huatamia kwa siku 29, huangua vifaranga kwa siku 3 na
mara nyingi hutotoa mayai yote, si rahisi mayai kubaki bila kutotolewa au
kuharibika.
Namna ya kutunza vifaranga
Mara tu vifaranga wanapoanguliwa, wachukue na kuwatenga na mama
yao kisha waweke katika banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa
ya umeme kama una uwezo ili kuwatengenezea joto.
Pia, waweza kuzungushia banda lao kitu kizito kama blanketi ili
kuwakinga na baridi au upepo.
Banda
Bata Bukini wanahitaji nafasi ya kutosha hivyo andaa banda
kulingana na wingi wa bata unaotarajia kufuga.
Hakikisha banda limesakafiwa au banda
la udongo lisilotuamisha maji au unaweza kuweka mbao au mabanzi kisha unaweka
maranda ili kuwakinga na baridi.
Maji
Ni lazima bata wapatiwe maji ya kunywa kila siku na hakikisha
banda halikosi maji wakati wote. Safisha chombo cha maji na kubadilisha maji
kila siku.
Ndege hawa wanahitaji maji ya kunywa ya kutosha kama ilivyo kwa
kuku. Hakikisha maji yako kwenye chombo ambacho hayatamwagika , kwani kumwagika
kunaweza kusababisha kuibuka kwa magonjwa. Bata Bukini hawapendi uchafu. Hivyo
maji yawe mahali ambapo hayatachafuka.
Magonjwa
Ni mara chache sana bata bukini kushambuliwa na magonjwa kama
watawekwa katika hali ya usafi. Magonjwa yanayoweza kuwasumbua ni mafua na
wakati mwingine kuharisha.
Tiba za asili
Unaweza kutibu bata bukini kwa njia za asili. Tumia mwarobaini,
vitunguu (maji na saumu).
1. Mwarobaini
Unaweza kutumia dawa hii kutibu mafua kwa bata bukini wakubwa au
vifaranga.
Maandalizi
Chukua kiasi kidogo cha mwarobaini kisha twanga vizuri kupata
maji maji. Kamua maji ya mwarobaini, kisha changanya na maji uliyo andaa
kuwanywesha vifaranga.
2. Kitunguu Saumu na Kitunguu Maji:
Dawa hii hutumika kukinga na kutibu bata bukini wanaoharisha.
Maandalizi
Unachukua kitunguu saumu au maji na kuondoa maganda ya nje kisha
safisha na kukata vipande vidogovidogo na kuwawekea kama chakula.Unaweza
kuwapatia kila siku hadi watakapopona.
3. Majani: Bata Bukini
chakula chao kikubwa ni majani. Majani yana vitamini A, hivyo hakikisha
unawapatia ya kutosha. Wapatie majani jamii ya mikunde.
Kutaga
Bata Bukini huanza kutaga baada ya miezi saba na hutaga mara
tatu kwa mwaka. Isipokuwa, utagaji wa bata bukini weupe na wa rangi
hutofautiana katika idadi ya mayai, Bata Bukini weupe hutaga mayai sita tu
lakini wale wa mchanganyiko wa rangi hutaga mayai kumi na mbili (mara mbili ya
weupe)
.........................................................................................................................................................................
.........................................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment