Banda bora ni muhimu ili ufugaji wa
kuku wa kienyeji uweze kuleta manufaa kwa mfugaji. Kuku huhitaji banda bora ili
wasiathirike na madhara mbalimbali kama wezi, wanyama wakali, jua kali au mvua.
Liwe na kuta, paa na sakafu imara. kuta na sakafu zisiwe na
nyufa Liwe na sehemu ya kuku kutagia, kuatamia na sehemu ya kulea vifaranga.
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala. Liwe na nafasi ya
kutosha kulingana na idadi ya kuku Liwe na uwezo wa kuingiza mwanga na hewa ya
kutosha. Liwe na nafasi inayoruhusu mtu kuingia na kufanya usafi.
2.SEHEMU INAYOFAA KUJENGA BANDA LA KUKU.
Isiyokuwa na mteremko mkali. Isiyoruhusu maji kutuama. Iwe sehemu inayoruhusu hewa na mwanga wa kutosha. Ikiwezekana iwe sehemu yenye kivuli.

3.AINA ZA MABANDA YA KUKU.
Uchaguzi wa aina ya banda la kuku hutegemea mazingira. Kuku wanaofugwa kwenye mazingira ya joto wanahitaji banda lenye ukuta mfupi na sehemu kubwa ya uwazi wenye wavu hadi kufikia kwenye paa kulinganisha na sehemu zenye baridi ambapo,banda linahitaji kuwa na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu,iliyo na uwazi wenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.vilevile eneo lenye matatizo kama ya majimaji au wanyama wanaoshambulia kuku inabidi kujenga aina ya banda lenye sakafu iliyonyanyuliwa juu.

4.VIFAA VINAVYOTAKIWA KATIKA UJENZI WA BANDA.
Vifaa vya kujengea banda vizingatie gharama na upatikanaji wake katika eneo husika.Vifaa hivyo vimepangwa katika makundi yafuatayo:

1. Vifaa vya kujengea sakafu Sakafu la banda la kuku linaweza
kujengwa kwa kutumia,saruji,udongo,mbao,mianzi au fito.
2. Vifaa vya kujengea kuta kuta zinaweza kujengwa kwa kutumia ,
fito,udongo,matofali,mawe,mabati,mianzi,wavu,mabanzi au mbao.
3. Vifaa vya kujengea paa. Paa la banda la kuku linaweza
kuezekwa kwa kutumia nyasi, makuti, bati, migomba na vigae kulingana na uwezo
wako.
4. Vifaa vya kujengea wigo Wigo unaweza kujengwa kwa kutumia
mbao,mianzi,matete,wavu,matofali,miti, au fito,mabanzi au mabati.
UKUBWA WA BANDA LA KUKU KULINGANA NA IDADI YA KUKU
Ukubwa wa banda la kuku unategemea na idadi ya kuku na aina ya kundi la kuku.Kuku wanaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kutegemea umri wao na madhumuni ya uzalishaji.
•BANDA LA VIFARANGA WADOGO WA KUKU NA UKUBWA WAKE

(UKUBWA WA BANDA LA VIFARANGA WADOGO)
Vifaranga wa siku moja hadi wiki nane Kundi hili la kuku wadogo hivyo wanahitaji eneo dogo la mita mraba 0.075 kkwa kuku mmoja,hivyo vifaranga 100 wanahitaji eneo la mita mraba saba na nusu (urefu wa mita 2.5 X na upana wa mita 3).

•BANDA LA VIFARANGA WAKUBWA
banda la vifaranga wa kuku wa wiki tisa hadi 20. Kuku mmoja wa umri huu anahitaji mita za mraba 0.15,hivyo kuku 100 wanahitaji mita za mraba 15 (urefu wa mita 5 X na upana wa mita
..............................................................................................................................................

0 comments:
Post a Comment