script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




BANDA BORA LA KUKU NI LAZIMA LIWE NA HIVI



Zifuatazo ni sehem za banda bora la kuku kulingana na aina ya kuku:-

1. Sehem za kutagia (kama ni kuku wa mayai au wa kienyeji).

Katika banda bora la kuku wanaotarajiwa kutaga inapaswa kuwepo na sehem za kutagia zijulikanazo kwa jina la viota. Viota vinaweza kutengenezwa kwa mtindo wa kuku mmoja mmoja au ushirika.


2. Sehem ya kutembelea.

 Ni ukumbi mkubwa kulingana na idadi ya kuku, ambao ndani yake kunakuwa na vyombo vya maji na chakula, pamoja na kuku wenyewe.


3. Sakafu

Zipo aina mbalimbali za sakafu kama ifuatavyo:-

a) Sakafu ya saruji

Ni vema zaidi ukajenga sakafu ya saruji kisha ukaweka maranda juu yake ili kuzuia ubaridi

         unaotoka sakafuni, na vilevile kupata wepesi wakati wa kufanya usafi.


 b) Sakafu ya udongo au mawe

 Jaza udongo wa mfinyanzi au mawe kisha siliba vizuri acha pakauke mwisho weka Maranda kwa wingi.


c) Sakafu ya chaga

   Banda hujengwa kisha huwekwa chaga umbali wa futi mbili kutoka chini, chaga inaweza

   ikawa ya banzi, "chicken wire" au fito ili kuruhusu kinyesi cha kuku kudondoka choini.


4. Ukuta

Unaweza kujenga ukuta kwa kutumia nguzo, pamoja na mabanzi au fito kisha kuzibwa vizuri na kuacha sehemu kubwa kwa ajili ya madirisha. Pia unaweza kutumia tofali za kuchoma, saruji au tofali za udongo kwa kujengea na kuacha sehem kubwa kwa ajili ya madirisha.


5. Paa

Vifaa vya kuezekea vinaweza kuwa ni vigae, nyasi, makuti au bati.


Kwa heshima na taadhima napenda kutumia fursa hii kukusalimia wewe mdau wa mifugo na ambaye  si mdau wa mifugo lakini unapenda kufuatilia mafunzo yetu.


Pia napenda kuwakaribisha katika darasa letu la ufugaji, tutakuwa tunawaletea

mada mbalimbali zinazohusu masuala mazima ya ufugaji.


Lengo kuu la darasa letu la ufugaji ni kumfanya  mfugaji afuge kwa......

kufuata kanuni za ufugaji  bora  ili ufugaji wake uwe ni wenye tija na kumpatia faida kwa ujumla.


Malengo mengine kama yafuatayo:

Kumfanya mfugaji aboreshe maisha yake kupitia ufugaji mifugo yake

Kuboresha afya za watumia mazao ya mifugo kama vile, Nyama, Mayai, na Maziwa kwa kuwa watatumia mazao ya mifugo kwa kanuni bora za ufugaji.

Kuongeza upatikanaji wa ajira  kwa vijana, watu wazima na wazee kwa ujumla kupitia ufugaji mdogo wa kati na mkubwa.

kuongeza matumizi sahihi ya nguvu kazi  na rasilimali watu kupitia ufugaji.

Hivyo basi ukiwa kama mdau wa mifugo au si mdau  lakini unapenda kufatilia darasa letu, tunakukaribisha tena na tena  katika kufatilia mfululizo wa mada mbalimbali katika darasa letu tunasema karibu sana
Usisahau kupitia app yako Kila siki kupata Updates mbalimbali
......................................................................................................................................

0 comments:

 
Top