
Sehemu zinazozunguka
nyumba pia zisafishwe. Vyombo vya maji , chakula na vitu vinginevyo
lazima viwe safi. Kwenye milango ya nyumba za kuku ziwekwe dawa za kuuwa
wadudu wa magonjwa. Nyumba za kuku zisiruhusiwe wageni kuingia mara kwa
mara kwa sababu wanaweza kuingiza magonjwa kutoka sehemu walizotoka.
Panya
na wadudu wengine wazuiwe kabisa kuingia ndani ya nyumba za kuku.
Pamoja na usafi katika nyumba ya kuu, kuna baadhi ya magonjwa ya kuku
ambayo ni ya hatari sana kwa sababu yanapoingia huuwa kuku wengi kwa
mara moja.
Baadhi ya magonjwa ni kama ifuatavyo.
1. Mharo Mweupe ( Pullorum au Bacillary White Diarrhoea)
Dalili za ugonjwa huu ni kama ifuatavyo:
1. Toka siku tatu hadi majuma mbili baada ya kupata vijidudu vya ugonjwa, vifaranga huharisha kinyesi cheupe na vingi hufa.
2. Kuku wakubwa wanaotaga, hupunguza kutaga mayai ghafla na baadhi yao hufa ghafla.
3.
Mpaka sasa hakuna matibabu ambayo yanafahamika yanayoweza kutibu
ugonjwa huu. Kitu ambacho mfugaji anawezaa kufanya ni kuchoma moto
kuku
wote wanaougua, na kusafisha nyumba nzima kwa dawa. Mfugaji amjulishe
haraka bwana mganga wa wanyama aliye karibu naye. Njia nzuri ya kuzuia
magonjwa, kwa mfugaji kununua vifaranga kutoka vituo vyenye sifa nzuri
ya kutokuwa na ugonjwa huu, hasa vituo ambavyo hupitisha uchunguzi wa
mara kwa mara kutafuta kama ugonjwa huu upo kwenye kutuo chao. Kituo
hicho cha kuangua vifaranga lazima kiwe kinatumia dawa za kusafisha
mashine za kuangua vifaranga.
Kuku
walioathiwa na ugonjwa huu huonyesha dalili zifuatazo. Kati ya majuma
manne hadi kumi hivi, baada ya kuambukizwa kuku huharishadamu , Kuku
ambao wameshikwa sana na ugonjwa huu, huonekana wemedhoofika sana na
huwa kama wemavaa koti, na shingo yao huinama chini. Kuku hao
hawashughuliki kutafuta chakula wala maji, na husinzia mara kwa mara
kwenye pembe za nyumba. Vifo hutokea vingi kila siku. Kuku wakubwa ambao
hawakufa hukuwa taratibu sana. Utagaji wa mayai hucheleweshwa au
hupunguzwa. Wakati mwingine kinyesi cha kuku hao huwa na rangi ya
kahawia baadaye kuwa na damu.
Ugongwa huu
hupona haraka kama matibabu yaanza mapema. Mfugaji amwone haraka bwana
mganga wa wanyama aliye karibu naye, ili amshauri dawa ambazo
zinatumika, kwa sehemu mbalimbali. Uzingatiaji wa masharti ya dawa ni
jambo muhimu sana. Kuushinda ugonjwa huu kunategemea usafi wa mfugaji.
Mfugaji inampasa ahakikishe kuwa haruhusu unyevunyevu kwenye takataka
zinazowekwa ndani ya chumba kwa kulalia kuku, hasa kwenye nyumba ya
kulelea vifaranga sehemu ambazo humwagwa sana maji ovyo kuzunguka vyombo
vya maji. Sehemu hizi ni lazima zitupiwe macho mara kwa mara.
Ikiwezekana vyombo vya maji na chakula viwekwe kwenye chakula au maji.
Vifaranga
wasisongamane sana kwenye chumba kidogo. Chakula cha vifaranga kitiwe
dawa ya kuzuia ugojwa huu, na hii ndio njia iliyo bora zaidi na yenye
uhakika katika kuzuia ugonjwa huu. Dawa huleta matokeo mazuri sana iwapo
itaambatana na usafi.
Haya
ni magonjwa ya kooni, nayo hutokana sana katika kuku waliosongamana, na
kwenye nyumba zilizojengwa vibaya. Sehemu za joto kama Tanzania
magonjwa haya ya kooni yanaweza kuzuiliwa kwa urahisi kwa kujenga nyumba
zenye kupitisha hewa ya kutosha, kwa sababu hakuna hofu ya baridi kali.
Kuku wadogo wanaweza kuugua ugonjwa huu kama kuna upepo mkali. Kwa hiyo
nyumba za kulelea vifaranga ziwekewe pazia la gunia, au vitamba au
makaratasi. Vumbi lipanguswe mara kwa mara kwenye kuta za nyumba za
kuku.
Hii
ni ndui ya kuku. Kuku huonekana na vipele vya rangi ya kijivujivu,
kwenye ngozi yake, hasa kwenye upanga wa kichwa. Baada ya muda mfupi
vipele hivi huwa vikubwa na kukutana na kufanya majeraha mabichi na
yenye kutoa damu . Baada ya siku kumi hadi kumi na nne hivi, majeraha
haya hukauka na kufanya makovu meusi. Kuku wanaougua wanaweza kutibiwa
lakini mfugaji inampasa atoe taarifa haraka kwa bwana maganga wa wanyama
aliye karibu naye ili ampatie dawa zinazofaa. Kuku wanaougua watengwe
haraka wanapoonekana ili wasiambukize wazima. Usafi ni muhimu katika
kuzuia ugonjwa huu usitokee. Kuku wapewe nafasi ya kutosha na
wasisongamane. Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kabisa kwa kuchanja dawa kuku
wote mapema.
Kuku
walioshikwa na ugonjwa huu huwa wazembe na hutokwa na hamu ya chakula.
Shingo ya kuku hulegea na manyoya hukunjamana. Upanga na ndevu hugeuka
na kuwa na rangi ya bluu. Koo la chakula huwa kubwa na hutoa mate
yanayotoa harufu mbaya. Kuku huyu hulemewa kuvuta pumzi, na huharisha
kinyesi chenye rangi ya kijani. Kichwa cha kuku huinamia nyuma au mbele
au pembeni. Kuku wengi, hasa wachanga hufa. Ugonjwa huu haujapata dawa
maalum ya kutibu. Mfugaji awatenge kuku haraka na amwarifu mganga wa
wanyama aliye karibu naye. Usafi wa nyumba na uwanja wa kuku ni jambo
muhimu sana katika uzuiaji wa ugonjwa huu. Kuku wachanjwe dawa mapema.
Kuku ambao wamepata ugonjwa huu wachomwe moto au wazikwe kwenye shimo
lenye kina kirefu kwenda chini.
Ugonjwa
huu unapomjia kuku kwa nguvu, hufa ghafla. Unapomjia taratibu kuku
husinzia na manyoya yake huvurugika. Shingo huinamia nyuma. Upanga na
ndevu hupanuka. Kuku huishiwa hamu ya kula chakula, na kuharisha kinyesi
cheupe. Baadhi ya kuku huvuta pumzi kwa shida na kutoa sauti ya
mkwaruzo. Mfugaji amwarifu bwana mganga wa wanyama aliye karibu naye, na
atamshauri dawa za kutumia. Usafi wa nyumba na uwanya wa kuku ndiyo
msingi wa kuzuia ugonjwa huu. Kuku walioshikwa na ugonjwa huu watengwe
haraka na baadaye wachomwe moto. Kuku wachanjwe dawa mapema kwenye
sehemu ambazo ugonjwa huu hutokea mara kwa mara.
Kuku
anapojiwa na ugonjwa huu kwa nguvu sana upanga na ndevu zake
hukunjamana. Kuku hufa ghafla japokuwa huonekana bado ana afya sana.
Ikiwa ugonjwa unamjia kwa taratibu hadi ukakomaa, upanga na ndevu
hufifia na kunyauka. Kuku huhara kinyesi cha rangi ya manjano. Hamu ya
chakula humtoka, isipokuwa hunywa maji mengi, na kuku huyo huonekana ana
wasiwasi sana. Kuna dawa nyingi ambazo zinaweza kusaidia kuponya baadhi
ya kuku wakati ugonjwa huu unapoingia.
Dawa
hizi mara nyingi hutengenezwa ili zitumiwe kwenye chakula au maji.
Mfugaji amwone bwana mganga wa wanyama aliye karibu naye ili amshauri
dawa ya kutumia. Nyumba za kuku ziwekwe kwenye hali ya usafi, na uwanja
usafishwe pia. Vyombo vya maji na chakula visafishwe kwa dawa. Kuku
wanaougua wote wachomwe moto. Kuku wazima wachanjwe dawa mapema na
ikiwezekana wachunguzwe kila mmoja kuona kama wapo wenye ugonjwa huo.
Mfugaji
inampasa awachunguze kuku wake mara kwa mara, ili ahakikishe kuwa kuku
wake hawana viroboto , chawa , papasi au wadudu wengine ambao ni wadogo
sana hata ni vigumu kuwaona kwa urahisi kwa macho. Wadudu hawa
huwasumbua kuku na kuwapunguzia uwezo wao wa kutoa mazao mengi ya mayai
au nyama. Ni jambo la busara kutumia dawa za wadudu ambazo hutengenezwa
katika hali ya unga. Dawa hizi hutumika kwa kuwapaka kuku au kumwagia
sakafu, au kwenye masanduku ya kutagia, au kwenye ngazi za kupumzika
kuku.
Mfugaji amwone maganga wa wanyama aliye
karibu naye ili amshauri dawa zinazofaa kwa sehemu yake. Kuna baadhi ya
wadudu wa kuku ambao wanakaa kwenye miguu ya kuku na kufanya magamba
miguuni. Mfugaji anaweza kutumia mafuta ya taa kwa kupaka miguu mpaka
atakapoona kuwa wadudu wote wametoweka.
Kuku
hushambuliwa na aina nyingi za minyoo ambayo huishi tumboni na
kuwanyonya damu au chakula na kuwadhoofisha, au kuwauwa kabisa. Njia
iliyo bora ya kuzuia minyoo hii ni usafi wa nyumba na uwanja wa kuku.
Hali ya kuambukiza ya minyoo ikizidi, mfugaji amwarifu bwana mganga wa
wanyama aliye karibu naye, ili amshauri dawa za kutumia.
Kudonoana manyoya, vidole, kulana wenyewe kwa wenyewe na kula mayai
Tabia
hizi mbaya za kuku hutokana na sababu nyingi mbalimbali. Sabubu
mojawapo ni upungufu wa nafasi ambayo hufanya kuku wasongamane sana. Kwa
hiyo kuku wapewe nafasi ya kutosha ya chakula maji na ya kupumzika.
Kuku wanaweza kuanzisha tabia hizi ikiwa chakula chao hakina aina zote
za chakula hasa nyama au chumvi au vitamini . Kwa hiyo njia mojawapo ya
kuepukana na tabia hizi mbaya ni kuwapa kuku chakula bora.
Wakati
mwingine kuku hushawishiwa kula mayai kutokana ukosefu wa kuondoa mayai
kwenye nyumba ya kutagia, mara kwa mara. Kwa hiyo mayai ni lazima
yaondolewe kwenye nyumba za kutagia mara tatu au zaidi kwa siku.
Uchovu
wa kukaa mahali pamoja unaweza kuwafanya kuku waanze baadhi ya tabia
hizi mbaya. Wafugaji wengi wenye busara huwazuia kuku wasianze tabia
hizi kwa kuwapatia majani mabichi ambayo huwafanya wawe na mchezo wa
kupoteza na kusahau kudonoana. Majani hayo hutundikwa kwa kamba.
Njia
nyingine ambazo hutumika kwa kuzuia tabia hizi mbaya za kuku ni
kuwakata midomo kwa kutumia kisu kilichopashwa moto , au chuma cha moto
wanachotumia mafundi kuungia. Ubora wa chombo kilichopashwa moto ni
kwamba mdomo wa kuku hukatwa na kuzuia damu isitoke. Kwa hiyo jeraha
hupona haraka. Kuku wakubwa na wadogo wanaweza kutumia vyombo hivi,
lakini mfugaji inambidi kukata kuku midomo kati ya majuma matatu hadi
tano. Mdomo unaokatwa ni wa juu, na ukatwe kuanzia robo hadi nusu ya
mdomo. Majogoo ya kupandisha yasikatwe kwa sababu yatashindwa kupanda.
.......................................................................................................................
.......................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment