script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




FAHAMU UTOAJI CHANJO KWA KUKU.
FAHAMU UTOAJI CHANJO KWA KUKU.


Changamoto za kiufugaji ni nyingi ila zisikukatishe tamaa ukifuata kanuni na taratibu za Ufugaji unaweza ukasahau kabisa kama kuna changamoto hizo.

Moja wapo ya kitu cha muhimu kwa kuku wako ni chanjo, chanjo ni kitu muhimu ili kuwafanya kuku wako wasipatwe na magonjwa hatari kama mdondo( kideri) , Ndui,gumboro nk.

Pia ni moja kati ya vitu vya muhimu kwa kuku vitakavyo fanya ufuge kwa amani na kusahau changamoto.

Ukizingatia chanjo pia itakuwa rahisi wewe kufikia ndoto zako za kiufugaji, kwani ili kuku wazaliane na mradi wako ukuwe ni lazima udhibiti vifo, kwa kupawa kuku wako chanjo utadhibiti vifo visivyo vya lazima.

ZINGATIA WAKATI WA KUTOA CHANJO KWA KUKU

_Hakikisha unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: jinsi ya kuhifadhi, kutayarisha na

njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa

chanjo ili isipoteze nguvu.

_Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaaa ya chanjo.

_ Watoa chanjo wapatiwe mafunzo ya jinsi ya kutayarisha na kutoa chanjo

_ Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku.

_ Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira.

_  Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya kuchanganyia chanjo, k.m. maji ya kisima,

mvua, n.k. Maji ya kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.

_  Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.

_  Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika

muonekano mzuri

_ Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa masaa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa

haraka.

_  Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.

_Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.

_Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri

_  Baada ya kila zoezi la kuchanja, wafanyakazi wabadilishe mavazi, viatu/buti zisafishwe na kuwekwa dawa,

na vifaa vilivyotumika viwekwe dawa ya kuua vimelea.

_ Weka kumbukumbu za uchanjaji vizuri

MAMBO AMBAYO HUTAKIWI KUFANYA WAKATI WA UTOAJI CHANJO

•  Kumwaga chanjo ovyo na kuchafua mikono au nguo

•  Kuchanganya chanjo za aina mbili au zaidi, isipokuwa pale tu mtengenezaji wa chanjo atakavyoagiza

hivyo, au kwa ushauri wa daktari wa mifugo.

•  Kutumia chanjo iliyopita muda wake

•  Kutumia chanjo iliyobaki ili itumike kwa kazi ya siku nyingine

•  Kuchanja kuku ambao wamepatiwa dawa aina ya antibiotiki.

•  Kuchanja zaidi ya chanjo moja kwa wakati, iwapo haikuagizwa hivyo



0 comments:

 
Top