script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




JINSI YA KUZALISHA KUKU CHOTARA KIRAHISI

Ufugaji wa kuku wa  chotara. Tunaposema chotara tuna maanisha ni mchanganyingo wa aina mbili za kuku. Mfano mchanganyiko wa kienyeji na kenbro wanajulikana kama kuku wa kenya. Sifa ya kuku chotara ni kama ifuatavyo,

1. Wanastahimili sana magonjwa.
2 Wanataga mayai mengi mpaka 240 kwa mwaka kama ukiwalisha vizuri kwa miaka mitano
3. Wanakua haraka sana. Wanafikisha mpaka kilo 3 kwa muda wa miezi mitatu kama ukiwalisha vizuri
4.Anatumika kama kuku wa nyama na mayai

Ukitaka kufuga kuku kibiashara usimwachie kuku kuhatamia mayai kwani unampotezea muda wa kutaga. Kusanya mayai weka kwenye mashine ya kutotolea vifaranga.
Ukitaka kupata faida kubwa usinunue chakula bali tengeneza mwenyewa kwani bei za vyakula zimepanda sana.
Kwenye ufugaji asilimia 80 inaenda kwenye ulishaji na asilimia 20 inaenda kwenye madawa.

Hatua ya kwanza, andaa banda lako ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku, banda la kuku linatakiwa liwe linapitisha hewa ya kutosha.

Hatua ya pili,  andaa kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina ya kocks au aina yoyote ile ambayo inafaa, wachanganye kuku wa kienyeji na jogoo la kisasa katika banda moja ili uweze kupata mayayi yenye mchanganyiko wa kuku wa kienyeji na kisasa.
Kumbuka jogoo mmoja (1)anatakiwa kuwa na matetea kumi na tano (15) au matetea yasizidi kumi na tano hii ni kwa ufugaji huria haisumbui

Hatua ya tatu kutotolesha mayayi ambayo umeyapata kutokana na mchanganyiko wako, unaweza kutumia mashine za kutotolesha mayayi au unaweza kuwatumia matetea yako ya kuku wa kienyeji kuatamia mayayi yako.

Hatua ya nne baada ya siku ishirini na moja (21), vifaranga vyako chotara vitakuwa tayari kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga kwa ajilia ya matunzo mpaka wakiwa wakubwa.
Vifaranga vikishakuwa tayari chanjo muhimu wanahitaji ili kuzuia vifo na mripuko wa magonjwa.
Vifaranga kwa muda wa wiki tatu hadi nne wanahitaji joto la kutosha, kwa ajili ya ukuaji afya njema
NB:Ikiwa Vifaranga wanafugwa mfumo wa ndani,joto linatakiwa kwa kipindi Cha siku 21
.......................................................................................................

0 comments:

 
Top