script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)
Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.
Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba
Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.
Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.
Kwa matokeo chanya na yenye faida  vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.
Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye seat ya gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka stress.
Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba
Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea  vifo au kuku kutokua vizuri.
Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.
Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.
Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.
JOTO
Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na heater or chanzo chochote cha joto.
Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya 40-41 degree centrigrade. (na njia sahihi ya kupima joto la vifaranga  chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo lako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto).
Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

MAJI
Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida)

Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

CHAKULA
Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders. Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).
Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa  feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au  fangasi wa chakula.
Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula  uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.

AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA
Chick starter
Wape 0.5kg kwa kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2
Grower
Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2
Finisher
Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza

BROILER TIPS
SIKU 1-5
Wape glucose na mchanganyo mmoja  wapo kati yah ii ifuatayo;
Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte
CHAKULA
Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi  wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.
SIKU YA 6
Vitamini (vitastress)
SIKU YA 7
Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)
WIKI YA PILI
Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)
WIKI YA TATU
Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7
WIKI YA NNE
Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)
WIKI YA TANO
Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)
WIKI YA SITA
Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni
Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo
................................................................................................................................

0 comments:

 
Top