Pullorum Disease: Ugonjwa Hatari Sana Kwa Vifaranga
MUHARO MWEUPE(PULLORUM DISEASE:)
-Kuhara kinyesi cheupe
Ni ugonjwa unao enezwa na bacteria (salmonella
pullorum)
Mzunguuko wa maambukizi ya ugonjwa huu hupitia
kwenye mayai ya kutotolewa hadi kwa Vifaranga.
Vifaranga huambukizwa kirahisi mnamo wiki 3 za mwanzo
kwa kula chakula chenye bakteri wa ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa kwa Vifaranga:
_Vifo vingi kutokea kwenye siku 10 za mwanzo
_Kutokuwa na hamu ya kula
_Vifaranga kuzubaa
_Kulegea kwa mabawa na manyoya kuchachamaa
_Kuvimba matumbo
_Vifaranga kupiga kelele na kuzubaa huku wamefumba macho
_Kuharisha kinyesi cheupe kama chaki /kinyesi kuganda kwenye
sehemu ya kutolea haja
_Vifaranga kuchechemea na kuanguka kabla ya kufa
_Vifaranga kuvimba magoti
Kupasua mzoga wa kifaranga:
1.Maini na mapafu kuvimba
2.Mapafu kupauka
3.Maini kuwa meusi mno
4. Moyo kuwa Si wakaida na kuwa na maji maji ya damu
5. Viungo vya miguu na vidole kuvimba.
Dalili za ugonjwa kwa kuku.
_Vilemba au upanga kusinyaaa
_Vifo kutokea Kati ya siku 4 au 5
_Manyoya kuchachamaa
_Kuku kutoa uharo mweupe kama chaki
_Uzalishaji wa mayai kuwa chini sana.
Kupasua mzoga wa Kuku.
1. Mayai kwenye sehemu ya kizazi kuwa na rangi ya kijani
kibichi /hadi weusi
2. Mfuko wa kizazi kujaa kiini cha njano cha mayai
3. Ini kuvimba.
4. Uvimbe mdogo mdogo wa kijivu ulioenea kwenye misuri
ya moyo
MATIBABU:
Tumia dawa yenye uwezo wa kuuwa bacteria kama
Esb3
Trisul
Tremazine 30%
NB:
ZINGATIA USAFI BANDANI, KUKU WAGONJWA SANA UNAWEZA WATENGA ILI KUDHIBITI UGONJWA KUENEA
...................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment