UTARATIBU WA KUCHANJA KUKU WA MAYAI
SIKU YA 1-5 NEW CASTLE VACCINE (ND)
Ni vizuri Zaidi ukapata chanjo iliyochanganywa NCD(ND) + IB
Vigosine
Antibiotic (Quinocal,Trisulmycine etc)
SIKU YA 7 -10 GUMBORO (cevac gumbo L)
SIKU YA 14-16 GUMBORO (cevac IBDL)
SIKU 18 vetacox or Anticox
SIKU YA 21 GUMBORO (cevac IBDL)
SIKU YA 26 NEW CASTLE VACCINE (ND)
Ni vizuri Zaidi ukapata chanjo iliyochanganywa NCD(ND) + IB
SIKU YA 35 NEW CASTLE VACCINE (ND)
WIKI YA 6 – 8 FOWL POX VACCINE
VIGOSINE
WIKI YA 10 NEW CASTLE VACCINE
WIKI YA 16-18 SINDANO (ND+IB+EDS)
Injection of killed vaccine – Newcastle + infectious Bronchitis + Egg Drop shell
COCCODIOSIS
Ugonjwa huu umekuwa ukirudisha maendeleo ya wafugaji wa kuku wa kisasa na wakienyeji kwa kusababisha vifo vingi Tanzania na duniani kote.
UGONJWA WA KUHARISHA DAMU NI NINI?
- Ugonjwa huu wa kuharisha damu unawapata sana kuku.
UGONJWA HUU HUENEZWA VIPI?
Ugonjwa huu huenea kutoka mnyama mmoja hadi mwingine kwa njia zifuatazo:
- Kula chakula chenye vimelea hai vya ugonjwa.
- Binadamu huweza kupeleka ugonjwa toka kwenye banda lenye ugonjwa hadi banda la kuku wasio wagonjwa kupitia viatu, mikono na nguo.
- Pia ugonjwa huweza kuenezwa na wadudu kama vile mende, panya, ndege na wadudu warukao.
JE, NI ZIPI DALILI ZA UGONJWA HUU?
Dalili za ugonjwa huu zinaweza kuonekana waziwazi au kwa kujificha .
Dalili hizo ni:
- Kuku kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu na mara nyingine huharisha damu tupu.
- Kuku hudhoofika.
- Hatimaye huweza kufa.
ATHARI ZA UGONJWA
- Kudhoofisha vifaranga na hata kuku wakubwa
- Vifo – kutokana na kupoteza damu nyingi.
- Kuku hupunguza utagaji wa mayai.
JINSI YA KUGUNDUA UGONJWA.
- Fanya uchunguzi mara kwa mara kwa mifugo yako, mabadiliko yoyote ya kuku kinyesi.
- Peleka kuku wako wakafanyiwe uchunguzi kwenye maabara za mifugo ikiwa ni pamoja na kuku walio kufa ili wafanyiwe uchunguzi wa kina.
UTANGULIZI
Minyoo ya kuku ni hatari kwani huleta hasara kubwa kwa mfugaji wa kuku wa nyama na mayai. Minyoo husababisha vifo vingi kwa kuku na hivyo kumkosesha kipato na mtaji mfugaji. Hata hivyo; licha ya madhara lukuki, ni wakulima wachache mno huchukua hatua mahusisi za kulikabili na kuthibiti tatizo hili.
AINA ZA MINYOO YA KUKU
i. MINYOO MVIRINGO
ii. MINYOO BAPA
MINYOO MVIRINGO
(a) Ascaridia galli
-Ni mkubwa kuliko minyoo mviringo yote ya kuku.
-Hupatikana katika utumbo
mwembamba wa kuku
-Ipo aina dume ya minyoo yenye urefu
yapata sm 3 hadi sm 8 na minyoo ya
kike yenye urefu wa sm 6 hadi sm 12.
(b) Heterakis gallinae
-Hupatikana katika utumbo mpana.
-Minyoo dume ina urefu wa mm 4 hadi
mm 13 na ya kike ina urefu wa mm 8
hadi mm15.
(c) Syngamus trachea
Hupatikana kwenye koo
Minyoo jike ina urefu wa mm 25 hadi mm 40. Minyoo dume huwa na urefu mm 2 hadi mm 6.
(d) Oxyspirura mansoni
Hupatikana kwenye macho (conjuctival sac)
Minyoo jike ina urefu wa mm 12 hadi mm 19.
(e) Gongylonema ingluvicola
Hupatikana katika umio au gole la
ndege.
Minyoo jike ina urefu ya pata mm 32
hadi mm 55.
(f) Cheilospirura hamulosa
Hupatikana kwenye firigisi.
Minyoo jike ina urefu wa mm 16 hadi mm 25.
(g) Tetrameres americana
Hupatikana karibu na firigisi
Minyoo jike huwa na urefu wa mm 3.5
hadi 4.5
(h) Dyspharynx nasuta.
Hii pia hupatikana kwenye firigisi, minyoo hii hukua na kufikia mm 10 kwa ile ya kike.
TEGU WA KUKU
· Minyoo hii hupatikana kwenye utumbo mwembamba.
· Huathiri kuku na jamii ya ndege.
· Kuku hupata aina hii ya minyoo kwa kula wadudu wabebao mayai au viini vya minyoo. Mfano minyoo ardhi (earthworms), konokono, inzi n.k.
· Ina umbo bapa.
(a) Raillietina tetrogona
Urefu hadi sm 25
Wanapatikana kwenye utumbo mwembamba
(b) Raillietina echinobothridia
Urefu hadi sm 25
Mahali, utumbo mwembamba.
(c) Raillietina cesticillus
Urefu hadi sm 13
Mahali utumbo mwembamba
(d) Davainea proglottina.
Urefu hadi mm 3
Mahali, utumbo mwembamba
(e) Amoebotaemia sphenoides
Urefu hadi mm 4
Mahali, utumbo mwembamba
(f) Choanotaenia infundibulum
Urefu hadi cm 30
1. UENEZWAJI WA MINYOO
· Kupitia chakula
· Kupitia ngozi
· Vilevile kuku kupata minyoo kwa kula wadudu wabebao mayai au viini vya minyoo kama vile Inzi, konokono n.k.
2. DALILI ZA MINYOO
· Kuku hukosa hamu ya kula
· Ukondefu
· Kushuka chini kwa utagaji wa mayai
· Kuku hunyongea
· Baadhi ya minyoo hukaba koo na kumfanya kuku ashindwe kupumua
· Baadhi ya minyoo huleta muasho kwenye macho.
· Minyoo pia huzuia mpito wa chakula na hivyo kuleta njaa kwa kuku.
· Minyoo ikizidi huua kuku
· Kuku pia huweza kupatwa na maambukizo ya magonjwa nyemelezi hasa pale minyoo inapotoboa utumbo na kusababisha vidonda. Bakteria huweza kushambulia sehemu hizi.
· Upungufu wa damu.
LAYERS
MAGONJWA YA KUKU WA MAYAI.
NA.
|
MAGONJWA
|
DALILI
|
CHANJO/TIBA
|
1.
|
New Castle Disease (Mdondo).
|
- Vifo vingi vya ghafla.
- Kuharisha.
- Hutokea wakati wowote baada ya wiki mbili.
|
Chanjo siku ya 7, rudia siku ya 21 kila baada ya wiki 12.
|
2.
|
Gumboro.
|
- Vifo vya ghafla
- Kukunja mabawa chini.
- Kujikusanya pamoja.
- Kuharisha kinyesu cheupe.
- Ugonjwa hutokea kuanzia wiki ya 2 hadi 18.
|
Chanjo siku ya 10 – 14, rudia siku ya 28 na 42 kwa kuku wa mayai.
|
3.
|
Avian Leukosis Complex.
|
- Mavecks – humpata kuku kuanzia umri wa wiki tatu, lakini mara nyingi ni wiki ya 12 – 24.
- Dalili ni kupooza mabawa, kuvimba na kufa.
- Kuvimba miguu, maini, wengu na figo.
|
Tibu.
|
4.
|
Fowl Typhoid .
|
- Vifo vya kuku mmoja mmoja.
|
Tibu tumia antibiotic
|
5.
|
Pollorum.
|
- Huuwa zaidi vifaranga wadogo kuanzia siku ya kwanza hadi wiki tatu.
- Vifaranga hujikusanya karibu na chanzo cha joto na kusinzia na kutoka na uharo mweupe.
|
Zingatia usafi wa mabanda na tiba.
|
6.
|
Paratyphoid.
|
- Dalili hazionekani, vifo hutokea wiki ya kwanza vifaranga hudumaa, wachovu na wanaweza kuharisha.
|
Tibu tumia antibiotic
|
7.
|
Colibacilosis.
|
- Vifo wiki ya kwanza vitovu havikauki.
- Hushindwa kupumua.
- Macho na kichwa kuvimba.
- Tumbo hujaa maji (Ascitis).
|
Tibu tumia antibiotic
|
8.
|
mafua (Coryza)
|
- Kupiga chafya.
- Kutoa makamasi.
- Kuvimba uso mara chache na kupata pneumonia.
|
Tibu tumia salfa/fluban/fluquin
|
9.
|
Coccidiosis (kuharihsa damu)
|
- Dalili zipo nyingi.
- Kinyesi kuwa na rangi ya ugoro au damu tupu.
- Vifaranga kudumaa.
|
Tibu tumia amprolium
|
10.
|
Foul Pox (Ndui).
|
- Kwa kuku wa mayai.
|
Kila kuku atachinjwa sahemu katika mbawa. Endelea kuwapa maji ya vitamin.
|
KIDERI
UGONJWA WA MDONDO/KIDERI (NEWCASTLE)
Mdondo/Kideri (Newcastle Disease)Maelezo
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ambao hushambulia aina zote za spishi za ndege, ijapokuwa kuku ndio aina
inayoathirika zaidi. Binadamu na wanyama wengine pia wanaweza kuambukizwa. Ugonjwa huathiri mifumo ya
fahamu, njia ya chakula na hewa.
Jinsi Ugonjwa Unavyoenea
• Chanzo cha maambukizi ni maji, chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa. Pia maambukuzi
huweza kupitia mfumo wa hewa kutoka kwa kuku wagonjwa.
• Kuku, vifaa vya kazi na bidhaa zitokanazo na kuku (nyama, mayai, manyoya na mbolea) kutoka mashamba
yenye ugonjwa zinaweza kueneza ugonjwa kutoka shamba moja hadi jingine.
• Vifaranga wanaweza kupata maambukizi kutoka vituo vya kutotolea vifaranga kutokana na maganda ya
mayai yaliyochafuliwa.
Dalili
• Vifo vya ghafla vya idadi kubwa ya kuku katika shamba/banda
• Kuku wanatetemeka na kushindwa kutembea
• Kuku hupooza miguu, mabawa na kupinda shingo; na hujizungusha mahali alipo
• Kuku huharisha kinyesi cha kijani na wakati mwingine chenye mchanganyiko wa rangi ya njano
• Kuku huzubaa na kuacha kula
• Kuku hukohoa, hupiga chafya na kupumua kwa shida
• Vifo vinaweza kufikia asilimia 100, kutegemea na umri na aina ya ndege
Uchunguzi wa Mzoga(POST MORTEM LESIONS)
Ugonjwa huathiri zaidi mfumo wa hewa na njia ya chakula, hivyo mabadiliko yanayoonekana kwenye mzoga ni
pamoja na:
• Madoa ya damu kwenye mfumo wa hewa
• Kamasi nzito zenye rangi ya njano kwenye koromeo
• Utandu mweupe kwenye mifuko ya hewa
• Bandama kuvimba
• Uvimbe kwenye kichwa na eneo la shingo
• Madoa madogo madogo ya damu kwenye kifua, mafuta na utandu wa tumboni
• Damu kuvia kwenye mfumo wa usagaji chakula - juju, firigisi, tumbo na utumbo
Tiba
• Hakuna tiba ya ugonjwa huu ila kuku wapewe antibiotiki.
• Pata ushauri wa daktari.
Kuzuia na Kinga
• Weka utaratibu wa kuhakikisha wafanyakazi , wageni na ndege hawaingii hovyo kwenye shamba/banda
• Angamiza mizoga yote kwa njia stahiki kwa kuchoma moto au kufukia kwenye shimo refu ardhini.
• Hakikisha banda la kuku lina hewa ya kutosha na epuka msongamano mkubwa wa kuku.
• Fanya usafi wa mara kwa mara kwenye vyombo vya kuwekea maji na chakula, pamoja na mabanda ya
kuku.
• Zuia uingizaji holela wa kuku wageni wasiochanjwa kwenye shamba/banda. Kuku wanaoingia shambani/
bandani watoke maeneo yasiyokuwa na ugonjwa.
• Tenganisha kuku kufuatana na umri
• Maeneo yenye ugonjwa yawekwe chini ya karantini na mabanda yapulizwe dawa
• Kuku wapewe Chanjo tangu vifaranga wa umri wa siku 3, baada ya wiki 3 – 4, na baadaye kila baada ya
miezi 3.
......................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment