Mbuzi ni wanyama ambao wanaweza kufugwa
kwa gharama nafuu pia ni wavumilivu wa ukame na maradhi tofauti na ngo’mbe kwa
kua wana umbile dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na nguvu kazi ndogo na
hata kwa wenye kipato kidogo.
Mbuzi wanaweza kufugwa kwa ajili ya
nyama/maziwa/ngozi/sufi na mazaomengine kama mbolea kwa matumizi ya familia na
kuongeza kipato.
NAMNA BORA YA
UFUGAJI:-
Wafugwe kwenye banda bora
Chagua kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji(uzalishaji)nyama/maziwa/sufi.
Walishwe chakula sahihi kulingana na umri
Kuzingtia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa.
Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
Kuzalisha nyama/maziwa/sufi bora unaokidhi mahitaji ya soko.

ZIZI/BANDA LA MBUZI
1.Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza
kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali(hatari) na wezi.
2.Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.
3.Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.
4.Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa
usafi.
UFUGAJI WA NDANI
ZINGATIA HAYA
Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi
kiafya,upepo/mvua n.k
Lenye hewa ya kutosha
Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya
kuwekea chakula na maji.
Liwe na vyumba tofauti kwa kuweka
vijitoto/wanao ugua/wanao kua.
UJENZI WA BANDA LA
MBUZI
Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
Sakafu iwe ya udongo/zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi/mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini
Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25 kati ya fito na fito au papi na papi,chumba cha mbuzi/kondoo wakubwa kiwe na sentimeta 1.9kati ya mbao na mbao.
........................................................................................................................

0 comments:
Post a Comment