Ufugaji wa samaki
Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.
Kuna
aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa
urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa
kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)
Urahisi
hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati
wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga)
sehemu nyingine.
Rasilimali muhimu za kuwa
nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu
na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna
gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au
kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na
sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)
Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.
Ukishachimba bwawa lako(aidha
na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi
2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa
kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya
samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na
mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na
kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka
mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki
kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe
wadogo(microorganisms)
Upatikanaji wa
vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua
kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under
right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa
kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana
kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo
wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa
Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI)
Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).
Ulishaji
wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki
hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa
tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha
asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye
gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.
Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.
Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.
Masoko yake haya samaki ni pamoja na
1.Supermarkets,
2.Wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.
Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.
Masoko yake haya samaki ni pamoja na
1.Supermarkets,
2.Wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.
.........................................................................................................
0 comments:
Post a Comment