script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Habari ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa website yetu,leo tujikumbushe namna ya kulea vifaranga.
Zifutazo ni hatua mbali mbali za maandalizi na mapokezi ya vifaranga.
1.MAANDALIZI YA BANDA
banda ni jambo la kwanza kwa mfugaji yoyote.banda la kuku huweza kujengwa kwa matofali,mbao,au hata miti na matope.
mfano wa banda la matofali lenye dirisha kubwa.
Banda la kuku linatakiwa liwe safi wakati wote

1.Sifa za banda la kuku
lipitishe mwanga wa kutosha
lisiwe na nafasi ya wadudu hatari na hata wanyama kupita
liwe karibu na makazi ya mfugaji
sakafu yake isiwe na matobo tobo mengi(iwe imesakafiwa vizuri kwa njia tofauti)
banda liwe na ukubwa wa kutosha sawa na idadi ya vifaranga.(mita 2 kwa 3)
ndani ya banda kuwepo mabox madogo madogo kwaajili ya kuwekea vifaranga.mabox hutunza joto na chini ya mabox hayo au vitalu kuwepo na pumba za mahindi au mpunga ili kuongeza joto.
mfano wa box hilo katika picha.

2.Andaa vyombo
vyombo kwaajili ya maji na chakula.unaweza kununua vyombo ua ukatumia sahani  za kawaida za nyumbani.kwa maji weka mawe madogo madogo  masafi katika vyombo hivyo ili vifaranga wasitawanye sana maji au wao kuloana na maji hayo.
mfano wa vyombo katika picha

3.Andaa taa ya chemli au bulb
Taa hutumika kwaajili ya kuongeza joto katika box au kitalu cha vifaranga.taa huwekwa ndani ya box hilo.Kwa wafugaji wakubwa hutumia bulb katika mabanda yao.joto katika vifaranga liongezwe wakati wa usiku na mchana liwe la kawaida.

4.Fahamu ratiba na chanjo kwa vifaranga kama ifatavyo.
siku 1-5 --dawa ya kufunga vitovu-

siku 7 --NEWCASTLE

siku 8, 9,10,11--VITAMIN

siku 14--Gomboro

Siku ya 15-20-VITAMIN

siku 21--gomboro Baada ya hapo endelea na vitamin hadi siku ya 27

 Siku ya 28-NEWCASTLE Kisha endelea na vitamin

wiki ya 5 chanjo ya ndui

wiki ya 6--Ampronium + ctc (siku tano)

wiki ya 7--Vitamin

wiki ya 8--dawa ya minyoo

ANGALIZO.EPUKA UCHAFU KATIKA BANDA ILI KUEPUSHA MAGONJWA KATIKA BANDA AMBAYO HUPELEKEA KUKU KUUMWA HIVYO KUTAFTIWA DAWA NYINGI ZAIDI NA KUPELEKEA KUONGEZEKA KWA GHARAMA ZA UFUGAJI.
5.CHAKULA
chakula cha kuku kiwe na mchanganyiko ufuatao.
nafaka(mahindi,uwele,mtama,ulezi nk)-------kg 40

pumba za nafaka_----------------------kg 27

chumvi ya jikoni--------------kg 0.5

virutubisho----------------------kg 0.05

unga wa chokaa na mifupa-----kg 2.25

mashudu ya alizeti ufuta au karanga --kg 20

dagaa na mabaki ya samaki---kg 10

6.ANDAA KUMBU KUMBU MUHIMU IWE NA;
tarehe ya kutotoresha

idadi ya vifaranga

kiasi cha chakula

vifo

vifaranga vilivyo uzwa

tarehe ya siku ya kurekodi

matibabu

ugonjwa
.............................................................

0 comments:

 
Top