Wafugaji wa mbwa wametakiwa kuzingatia suala la afya kwa wanyama hao ili kuwaepusha na maradhi mbalimbali yanayo weza kuwa kumba ikiwemo ugonjwa mbaya wa kichaa unao sababishwa na virusi vinavyo julikana kwa jina la Rhabdovirus.
Wafugaji wa mbwa wanatakiwa kuacha ufugaji wa mazoea usiofuata taratibu za kitaalamu na badala yake kufuga kitaalamu kwa kujali afya za wanayama hao ili kuwanusuru na maradhi hususani ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Pi ni vyema mfugaji akawa na utaratibu wa kumpatia chanjo ya ugonjwa huo kila mwaka ili kumlinda mnyama ikiwemo kuwanusuru wanyama wengine na binadamu wasipatwe na tatizo la kichaa cha bwa pindi inapotokea wamen’gatwa na mbwa, kwani endapo mnyama au binadamu ananapokuwa amen’gatwa na mbwa mwenye kichaa anaweza kupata tatizo hilo.
Kumbuka suala la kuwapatia mbwa chanjo ni suluhisho pekee la kumnusuru mnyama huyo dhidi ya ugonjwa wa kichaa kwa kuwa akisha athiriwa na tatizo hilo hakuna tiba itakoyo weza kumponya kwani anapopata ugonjwa huo hatma yake ni kifo.
Mfugaji mzuri wa mbwa ni yule anaefuatilia afya na maisha ya kila siku ya mnyama kwani ufuatiliaji huo unaweza kumsaidia kujua kama mnyama wake amebadili tabia au laa huku akizingatia tabia za mbwa mwenye kichaa kwa kuwa huanza kubadilika kwa kudhuru ovyo vitu mbalimbali ikiwemo wanyama wengine na binaadamu.
Unashauriwa kuwa endapo mfugaji ukigundua kuwa mfugo huo umebali tabia hatua ya kwanza anayotakiwa kuichukua kabla ya kumuona mtaalamu wa mifugo ni kumfungia sehemu tofauti na mbwa wengine ambao hawajaonesha dalilii ya mabadiliko yoyote ili asije kuwadhuru wanyama wengine.
............................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment