script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




  •  Mfugaji anatakiwa awe na dhamira ya kweli ya ufugaji.
  • Kufanya tathmini ya rasilimali alizonazo kwaajili ya mradi.
  • Chanzo endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi.
  • Hulka ya uvumilivu na uthubutu.
  • Tathmini ya soko la bidhaa za samaki.
  • Kujipatia maarifa ya msingi ya ufugaji wa samaki.
  • Eneo linatakiwa liwe na maji ya kutosha kwa mwaka mzima.
  • Eneo la kufugia linatakiwa kuwa na udongo unaotuamisha maji.
  • Eneo zuri halitakiwi kuwa na historia ya mafuriko, kwani mafuriko yakija yana flash away samaki na bwawa kujaa udongo.
  • Eneo linatakiwa kufikika kiurahisi.
  • Kuwa na umiliki wa uhakika wa eneo.
   
            AINA ZA MABWAWA
1)Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea i.e earth pond
2)Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa simenti, matofali na  zege.
    UPANDIKIZAJI WA VIFARANGA
    Mfugaji anatakiwa asivimwage vifaranga kwenye bwawa moja kwa moja, bali anatakiwa kuruhusu maji aliyobebea yabadilishane joto na maji ya bwawani. Hapa mfugaji anatakiwa kuweka kontena au chombo alichobebea kielee kwenye bwawa kwa takribani nusu saa ndio awamwage vifaranga.
     Jambo lingine la kuzingatia ni kwamba usafirishaji wa vifaranga ufanyike wakati ambao hali ya hewa imepoa, yaani asubuhi au jioni, kwani kwenye nyakati hizo vifaranga huweza kuhimili misukosuko ya hali ya hewa.

     ULISHAJI WA SAMAKI
*Samaki wapewe chakula mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.
*Kuwalisha vyakula tofauti kulingana na silka ya aina ya samaki unaofuga.
*Kuna samaki wanaopendelea vyakula vya nyama nyama hawa ni kama kambale na sangara ( hawa hawali pumba). Sato na perege wanakula mchanganyiko wa nyama na mboga mboga. Pia kuna samaki wanaokula mimea tu hawa hujulikana kama carps.

        UVUNAJI WA SAMAKI
     Samaki wa kwenye mabwawa huchukua takriban miezi sita mpaka tisa. Huvunwa kwa kutegemea uzito au vile mfugaji atapoona inafaa. Kwa kawaida samaki huvunwa kwa kutumia nyavu au kwa kumwaga maji yote bwawani.
      Soko la samaki ni kubwa sana kwani uhitaji wake huongezeka kwa kasi sababu ya madhara yatokanayo na nyama nyekundu. Kuna soko la awali ambapo mfugaji huuza samaki wake moja kwa moja kwa mlaji. Pili kuna soko la kati, hapa mkulima huuza kwa wafanyabiashara wa kati ambao huwauzia walaji. Na tatu ni soko la kimataifa
.......................................................................................................

0 comments:

 
Top