Ugonjwa huu huathiri kuku katika umri wowote na unapoingia kwenye kundi huweza kuua idadi kubwa ya kuku hao hadi kufikia asilimia tisini. Ndege wakubwa hustahimili kidogo kuliko wale wadogo kwasababu ya usugu mwilini (body immunity) uliojengeka kwa muda mrefu zaidi.
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha kirusi kiitwacho Paramyxo viridae na huenezwa kwa njia ya hewa na kugusana.
Dalili zake:
Kukohoa
na kuhema kwa shidaUte hutoka mdomoni na puaniKuku walioathirika hupata
kizunguzungu.Kuharisha uharo wa kijani na njanoKuzubaa, kusinzia na
mabawa kushukaBaada ya siku 2 kuku hupindisha shingoKuvimba
machoKuzungukaKuku hutaga mayai hafifu.90% ya kuku huweza
kufaTiba:Ugonjwa huu hauna dawa.
Kinga:
Kuchanja; Chanja kuku wako kila baada ya miezi mitatu /na mara nne kwa mwaka.
Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu, nazo ni;
Kuna chanjo aina mbili za ugonjwa huu, nazo ni;
1. Lasota :
Chanjo hii hutolewa katika dawa yenye umbile la kidonge kimoja kimoja ambacho kina dozi ya kuku 1000 na huwekwa kwenye maji ili kuku wanywe hiyo dawa.
Inashauriwa kuku wanaopewa dawa hii wanyimwe maji ya kunywa siku moja kabla yake
Ni vizuri kuwapa mchanganyiko maalum wa dawa wenye mchanganyiko wa vitamin na dawa ya kuwaongezea kuku nguvu. Dawa hii itolewe saa moja au zaidi baada ya kuwapa chanjo ya mdondo.
Ni vizuri kuwapa mchanganyiko maalum wa dawa wenye mchanganyiko wa vitamin na dawa ya kuwaongezea kuku nguvu. Dawa hii itolewe saa moja au zaidi baada ya kuwapa chanjo ya mdondo.
Huwekwa
katika chupa kimoja (vial) chenye dozi 400 za kukuChanjo hii inavumilia
joto ikikaa bils nje ya jokofu kwa muda mrefu zaidi.Imetengenezwa katika
mazingira ya nchi za joto.
Na inaweza kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa ipasavyo hata baada ya kutumia mara ya kwanza..
Na inaweza kukaa kwa siku 14-15 ikiwa itatunzwa ipasavyo hata baada ya kutumia mara ya kwanza..
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea cha protozoa cha jamii ya Eimeria (Eimeria tenela, Eimeria maxima, na Eimeria acervulina)
Kwa kawaida wadudu hawa hupenda kuishi kwenye mazingira machafu, kama vinyesi, vyakula vilivyooza na umaji maji.(moist environments).
Dalili zake:
Kinyesi chake huchanganyika na damu
1. Wakati mwingine kuku hunya damu.
2. Kuku hudhoofika sana.
3. Kuku huteremsha mabawa yake.
4. Hatimaye vifo hutokea.
Tiba;
Ugonjwa huu hutibika kwa kutumia dawa za
(i) Kundi la suphur
Mfano: sulphonamides (ESB3) kwa siku 3-4
Mfano: sulphonamides (ESB3) kwa siku 3-4
(ii) Amprolium
Dawa za ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo ukipatwa na tatizo hilo fika kwenye maduka ya dawa aua muone mganga wa mifugo.
Dawa za ugonjwa huu hupatikana madukani hivyo ukipatwa na tatizo hilo fika kwenye maduka ya dawa aua muone mganga wa mifugo.
Kinga:
Zingatia usafi mara kwa mara
Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na majimaji na uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu , ni vizuri kuhakikisha banda la kuku linakuwa safi na kavu wakati wote.
Zingatia usafi mara kwa mara
Kwakuwa ugonjwa huu huambatana na majimaji na uchafu wenye vimelea vya ugonjwa huu , ni vizuri kuhakikisha banda la kuku linakuwa safi na kavu wakati wote.
Tenga kuku wagonjwa kutoka kwa walio
wazima.Tumia dawa ya kinga ili kuepusha uwezekano wa kuku kuambukizwa
ugonjwa huuDawa inayopendekezwa ni zile zinzoitwa (coccidiostat.Tenga
kuku wadogo (vifaranga) kutoka kwenye kundi la wakubwa.
Husababishwa na vimelea vya wadudu wa bakteria wa jamii ya Salmonella.
Kimelea hicho cha bacteria huitwa Salmonella gallinarum.
Dalili zake:
Uharo
mweupe au wa kijaniVifo hufikia kiasi cha 50%Rangi ya minofu hugeuka
kuwa ya njanoViungo vya ndani kama maini , figo , bandama huvimbaMaini
hung’aa kwenye mwanga mkali.
Tiba :
Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.
Tiba :
Tumia dawa za antibiotiki kama vile furazolidone ili kutibu ugonjwa huu.
KINGA: Chanja kuku wako mara kwa mara .
Fanya usafi wa banda na vyombo vya kulishia na kunyweshea maji ipasavyo.
Ugonjwa
wa mafua ya ndege ni ugonjwa hatari sana kwa kuku na jamii nyingine za
ndege.Pia ugonjwa huweza kuambukizwa na kusababisha vifo kwa
binadamu.Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho Orthomyxo
virus.Ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kugusana baina ya ndege na ndege
na baina ya ndege na binadamu.
Dalili zake:
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana katika kipindi cha siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa.
Dalili hutofautiana kutokana na umri wa ndege.
Dalili zake:
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana katika kipindi cha siku 3-7 baada ya kuku kuambukizwa.
Dalili hutofautiana kutokana na umri wa ndege.
Baadhi ya dalili zake nihizi zifuatazo
Kuku
/ndege hupumua kwa shida (dyspnoea).Kuzubaa.Kutokwa na machozi.Kukohoa
na kupiga chafya.Kuharisha kinyesi chenye majimaji.Sehemu za kichwa
zisizo na manyoya huvimba.uvimbe wenye majimaji huonekana kichwani na
shingoni.Sehemu ya juu kichwani hubadilika na kuwa na rangi ya bluu
iliyopauka.Kuku hutaga mayai yenye maganda laini.
Tiba:
Ugonjwa huu hauna tiba .
Kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu:
Tiba:
Ugonjwa huu hauna tiba .
Kinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu:
Toa taarifa kwa
mganga (daktari wa mifugo aliye karibu ukiona dalili za ugonjwa
huu.Tenga mabanda ya kuku wagonjwa na walio wazima.Fungia kuku wako
wasitembee holela.Acha kununua kuku kutoka eneo linalohisiwa kuwa na
ugonjwa huu.Acha kusafirisha mifugo /ndege bila idhini ya daktari.Zuia
wageni kutembelea mabanda yako ya kuku.Acha kuhamisha mbolea ya kuku
kwenda shambani kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa ugonjwa
huu.Safisha mabanda na kuweka dawa chini ya usimamizi wa mtaalamu wa
mifugo na kulipumzisha kwa siku 21kabla ya kuanza kufuga tena.Choma moto
mkali au fukia chini mbolea kutoka kwenye banda la kuku wanaoumwa
ugonjwa huu.Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu
nawe.
Ugonjwa huu husababishwa na kirusi
Dalili zake:
Hushambulia
vifarangaUharo mweupeKuchafuka (dirting of anal area)KuvimbaKiwango
kikubwa cha vifoDamu hutapakaa eneo la kutolea kinyesi
Kinga:
1. Usafi
2. lishe bora
3. chanja vifaranga wakiwa na umri wa wiki tatu kwa kutumia chanjo hai (live vaccine)
6. Kifua Kikuu cha Ndege(Avian Tuberculosis-TB):
Husababishwa na kimelea aitwaye Mycobacterium avium.
Husababishwa na kimelea aitwaye Mycobacterium avium.
DALILI ZAKE:
Kukonda na Kupungua uzitoVidonda kwenye kishungiKupungua uzito/kukondaKuhara
Kinga:
Usafi:
Fanya usafi na vyombo , banda na mazingira .
Fanya usafi na vyombo , banda na mazingira .
Dalili za magonjwa haya hutegemea aina ya virutubisho vinavyokosekana mwilini
Kwa mfano:
Kupinda miguu (rickets)
husababishwa na upungufu wa Vit.D, madini ya calcium na
fosforasi.Vidonda vyenye vyenye damu husababishwa na vit.KKichaa cha
kuku na kusinyaa kwa misuli husababishwa na upungufu wa Vit.EMagamba ya
Mayai (egg shell)kuwa laini ama umbo kuwa bovu husababishwa na
upungufu wa madini ya calcium na fosforasi.Kudonoana kusababishwa kwa
njia moja au nyingine na upungufu wa chakula na madini ya fosforasi na
calciumKuvimba macho, upungufu wa damu huletwa na upungufu wa
vit.A.Kinga:Kuwapa kuku mlo kamiliKuelewa kwa kina aina za chakula kwa
kila rika na aina ya kuku ; vifaranga , kuku wa mayai na wa nyama.
(Poultry age and classes i.e chicks, layers and broilers)Kufanya
uchunguzi wa virutubisho vilivyomo katika aina ya chakula unachotumia.
8. Minyoo (Helminthiasis):
Minyoo iko ya aina tatu kama vile minyoo kamba, minyoo bapa na minyoo ya mviringo
Dalili zake:
Kudumaa Kuwa manyoya hafifuKupungua uzitoKukondaMinyoo huonekana kwenye kinyesi
KINGA / KUZUIA:
USAFI:
Fanya
usafi wa vyombo, banda na mazingira.Tenga vifaranga kutoka kwa wale
wakubwa.Badilisha matandazo kuondoa mazalia ya minyoo.Badilisha
matandazo kila baada ya miezi mitatu.
TIBA
Tumia dawa zinazopendekezwa na wataalamu hasa zile
zinazoua minyoo ya aina zote (mfano: piperazine citrate).Hakikisha kila
baada ya miezi mitatu unawapa kuku wako dawa za minyoo.
9. Kupe, Utitiri, Chawa na Viroboto
kupe laini waitwao Argus persicus, chawa na viroboto wanaong’ata .
Dalili zake:
Kujikung’uta.Kupiga
kelele.Kiasi cha damu hupungua mwilini.Utando wa ngozi ndani ya kope za
macho hupauka.Utando wa ngozi ya juu mwilini huwa mnene.Magamba ya
unga-unga hudondoka.
Kuzuia:
Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga.
Kuzuia:
Tupa au choma masalia ya mayai yasiyoanguliwa na magamba ya mayai yaliyoanguliwa vifaranga.
Safisha banda mara kwa mara na kunyunyizia dawa; kuna dawa zinazopendekezwa na wataalamu za kunyunyizia kwenye banda la kuku.
............................................................................................................................................................
............................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment