![]() |
Mshindo media |
Changamoto zake za magonjwa kama mfugaji hauna budi kuzikabili na kuhakikisha unazuia maambukizi ya magonjwa,
Leo tunakuletea kufahamu zaidi ugonjwa wa ndui ya kuku .
Ndui ni ugonjwa umbao unasababishwa na virus aina ya avipoxvirus ambao hushambulia zaidi kuku na jamii yote ya ndege,katika umri wowote wa kuku ndui inaweza ikampata kuku.
Virus aina ya avipoxvirus.
Virusi hivi vya Ndui husambaa kwa njia nyingi yaweza ikiwemo.
- Kwa njia ya kuku kudonoana.
- Kupitia ndege wa porini kwa kuingiliana vyombo vya maji na chakula.
- Pia vyombo vya maji na chakula vinavyo chafuliwa na kuku mwenye vimelea vya ugonjwa wa ndui.
- Pia maabukizi ya virus vya ugonjwa wa ndui kwa kuku husababisha kuku kudumaa na kua na ukuaji usio mzuri,kuku hupunguza kiwango cha utagaji.
- Pia virus avipoxvirus vinaweza kuishi katika mazingira kwa mda mrefu.
- Hushambulia zaidi sehemu zilizo wazi zisizo na manyonya kwa uwepo wa vinundu(viuvimbe)vya rangi ya kahawia.
- Kupumua kwa shida,macho ya kuku kuonekana kusinzia na kuwa na mfano wa kitu cheupe kwenye jicho,
- Utando mweupe mdomoni,vifo vinaweza kufikia hadi 50%
Jinsi Ya Kuuzuia Maambukuzi Na Usambaaji Wa Virusi Vya Ugonjwa wa Ndui.
Kinga na tiba;
ugonjwa wa ndui hauna tiba unashauriwa kuchanja kuku wako mapema hasa kipindi cha miezi ya joto wachanje wakiwa na umri wa wiki 7 hadi wiki 14, tenga kuku wanao umwa ili kuzuia maambukizo kuenea.
Fukia au choma mizoga yote iliyo kufa kwa ugonjwa.
Kuku anae umwa mpatie vitamini pamoja na glucose ili kupunguza makali ya ugonjwa,pia tumia antibiotic ili kuzuia maambukizi mapya yanayo weza kujitokea,
- Jinsi ya kuchanja chanjo ya ndui kwa kutumia sindano maalum chanja katikati ya ngozi kwa kutumia utando wa ngozi kwenye bawa.
Inashauriwa kuchanja kuku wakiwa na umri wa kuanzia wiki mbili.
- Hivyo wapatie chanjo fowl-pox vaccine.
- Kuku wakiugua wapewe (multi vitamini) vitamin na antibiotiki.
- kama OTC 20% kutibu vidonda.
Mambo Yakuzingatia Katika Kuzuia Magonjwa Katika Kuku.
- Hakikisha unawapatia chanjo zote za muhimu katika uzuiaji wa magonjwa yanayosambazwa na virusi kwani magonjwa haya hayana tiba endapo pale yanapo kuwa yamewapata kuku, ikiwemo, ndui ya kuku, ndui ya kuku na gumboro.
- Usafi wa mabanda ni jambo lingine la msingi sana kuzingatia kwa ufugaji unaozingatia uzuiaji wa magonjwa.
- Tenganisha kuku wote wenye dalili na waliokwosha patwa na magonjwa ya aina yotote iwe yanayosababishwa na bacteria kama kuvimba uso, kuharisha kinyensi cheupe, na hata yale yanayosababishwa na virusi kama ndui na hata mdondo/kideri.
- Kwa ushauri wasiliana na wataalamu au taasisi zinanazo jishughulisha na utaalamu na tiba za mifugo ................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment