script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




MAMBO MUHIMU YA KUKUMBUKA/KUZINGATIA UNAPOTOA CHANJO NA TIBA

1. Chanjo hutolewa kutegemeana na aina ya ugonjwa unaotaka kudhibitiwa. 

2. Chanjo tofauti hutolewa kwa nyakati ratiba/ tofauti , kipimo, na masharti tofauti ya
utunzaji wa dawa ya chanjo. 

3. Chanjo hutolewa kabla ugonjwa haujatokea kwa sababu chanjo imekusudiwa kukinga
wala siyo kutibu. 

4. Ili Chanjo iweze kufanya kazi vizuri hutolewa kwa kuku wenye afya nzuri. 
H
5. Endapo chanjo itatolewa kwa kuku anayeumwa haitafanya kazi vizuri badala, yake
itaongezea kasi ya ugonjwa na hata kusababisha kifo.
Hivyo ni muhimu kila mfugaji aweze kutambua dalili za kuku wagonjwa ili asifanye makosa
ya kuwachanja, badala yake awatibu kwanza, wakishapona ndipo wapate chanjo.
6.Hakikisha maji yanayotumika kutoa chanjo ni safi na salama (Yachemshwe na kisha yapoe).
7. Zingatia muda wa kutoa chanjo kwa kuku. Mfano chanjo za kuwapa kwenye maji hakikisha unawajengea kuku wako *kiu* ndani ya masaa 2 ili utakapo wapa chanjo waweze kunywa wote.
8. Hakikisha kuna vyombo vya kutosha ili uweze kuchanja Kuku wako kwa wakati mmoja

*Kumbukumbu*

Mfugaji anashauriwa atunze kumbukumbu za chanjo na matibabu ili zimsaidie kujua
yafuatayo:-
i. Muda sahihi wa kuanza chanjo na kurudia chanjo.
ii. Idadi ya kuku wanaotakiwa kuchanjwa muda wa kuchanja ukifika.
iii. Kiasi cha dawa kinachohitajika (dozi) kuandaliwa.
iv. Aina ya chanjo inayohitajika kulingana na magonjwa yanayojitokeza mara kwa mara.

*Kushirikiana Kati Ya Wafugaji Na Wafugaji*

Udhibiti wa magonjwa kwa njia ya chanjo unahitaji nguvu ya pamoja ili kupata matokeo
mazuri. Ni vizuri wafugaji kwenye eneo moja wakishiriki kupanga mkakati na kusimamia
utekelezaji wa suala zima la uchanjaji. Umuhimu wa kuchanja kuku kwa wakati mmoja katika
eneo ni muhumu ili kudhibiti ugonjwa kwa wakati mmoja. Mfugaji anayeamua kuchanja
azingatie ratiba ya chanjo ya ugonjwa husika ili kuweza kupata matokeo mazuri.
Kumbuka siku zote:
Magonjwa tofauti yana Chanjo tofauti.
Kama umewachanja kuku wako ili kuwakinga na Mdondo, haina maana kuwa
umewakinga na magonjwa yote.
Hivyo, kila ugonjwa unaotakiwa kudhibitiwa kwa chanjo lazima ifanyike
chanjo yake tofauti. Nayo ifanywe kwa kuzingatia wakati uliopendekezwa na
wataalam.

*TIBA*

Tiba hufanyika baada ya kuona au kutambua kuwa kuku wana dalili za ugonjwa. Mfugaji awe
makini kufuatilia afya ya kuku wake ili kubaini matatizo ya ugonjwa mapema. Hii itamsaidia
kufanya matibabu mapema kbla hayajaleta madhara makubwa kwa wale wanaoumwa. Pia
itakuwezesha kudhibiti ugonjwa mapema ili usiendelee kuenea kwa kuku wengine.

*Zingatia yafuatayo unapotoa tiba:-*

• Toa dawa sahihi kwa ugonjwa husika kufuatana na maelekezo ya mtengenezaji
yakiwemo kiasi, muda wa kutoa na ratiba ya kurudia dawa. Vile vile chunguza ukomo
wa kutumia dawa ili utumie dawa yenye nguvu inayohitajika.
• Wakati wa kutibu usitumie dawa chini ya kiwango kilichopendekezwa. Ukifanya hivyo
vimelea vya ugonjwa unaotibu vitajijengea usugu kwa dawa hiyo na baada ya muda
dawa hiyo haitakuwa na nguvu ya kutibu.
• Dawa nyingine zina madhara kwa binadamu iwapo watakula nyama na mayai kutoka
kwa kuku walilotibiwa ndani ya kipindi kilichozuiliwa. Hivyo mfugaji asiuze mazao ya
kuku kabla kipindi hicho hakijapita ili kumkinga mlaji wa nyama au mayai.

*HITIMISHO*

Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba. Kanuni za ujumla ya kudhibiti magonjwa
katika ufugaji wa kuku ni kuhakikisha yafuatayo:-
• Kutunza usafi wa sehemu wanapokaa. Kama unafuga katika banda hakikisha
linakuwa safi bila kuwa na unyevu. Wadudu na vimelea vya magonjwa
huzaliana kwa urahisi katika mazingira yenye unyevu.
• Hakikisha kuwa vyombo vya kuwalishia na kuwanyweshea maji vinakuwa
visafi.
• Hakikisha hawakutani na kuku ambao tayari ni wagonjwa maana
wataambukizwa. Inawezekana kufanya hivi kama unafuga nusu ndani na
nusu nje kwenye uzio au ndani ya banda.
Kama unafuga huria watakuwa kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa na kuku
wengine.

*_NB, Hakikisha unasoma muda wake wa mwisho wa matumizi (expire date) dawa na chanjo kabla ya kununua/kutumia
............................................................................................................................................

0 comments:

 
Top