FAHAMU MAGONJA MAWILI HATARI KWA NGURUWE
UFUGAJI
Unahusisha wanyama wa aina mbalimbali ambapo leo tunawalenga wale wanaojihusisha na ufugaji wa nguruwe ambapo tunaangalia magonjwa mawili ambayo ni hatari kwa wanyama hao.
Homa ya Nguruwe (African Swine Fever)
Ni ugonjwa unaoambukizwa kutoka nguruwe mmoja kwenda kwa mwingine kwa kasi kubwa sana.
Dalili zake ni
- Nguruwe kuwa na vidonda mdomoni,
- Kuvuja na kusambaa damu kwenye viungo vingi vya mwili wa mnyama,
- nguruwe kuwa na madoa yenye damu,
- kutoa mimba,
- masikio kuwa mekundu kutokana na damu iliyovilia ndani ya ngozi,
- kuvimba kwa figo kutokana na kujaa damu.
Ugonjwa huu hauna tiba maalumu wala chanjo inayofaa hivyo mfugaji anatakiwa kuuzuia mapema kwa kutowaruhusu nguruwe kutembea ovyo.
Tegu (Tapeworm)
Ni aina ya minyoo inyosababisha ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama Cystcercosisi unaojitokeza kama viuvimbe vingi vilivyojaa maji katika mwili wa nguruwe.
Minyoo hawa wakiwa katika hatua ya lava humuingia nguruwe wakati wa kula chakula kilichochanganyika na kinyesi cha binadamu chenye mayai ya tegu.
Minyoo hawa wakiwa katika hatua ya lava humuingia nguruwe wakati wa kula chakula kilichochanganyika na kinyesi cha binadamu chenye mayai ya tegu.
Dalili zake si rahisi kuziona nguruwe akiwa hai hivyo uchunguzi wa nyama yake akiwa amechinjwa.
Dalili kuu ni
- mfumo wa fahamu na misuli kuvurugika,
- Malengelenge katika eneo la kutolea haja kubwa na chini ya ulimi,
- Afya kudhoofika,
- Mapigo ya moyo kushindwa kufanya kazi,
- Kuwa na uvimbe uliojaa maji yenye ukubwa wa milimita tano hadi nane kwa milimita tatu hadi tano, maji yake huwa na rangi ya kahawia Dalili nyingine ni
- vijipu katika moyo, ulimi, misuli ya mashavu, mabegani na kwenye koromeo.
- Matibabu yake ni dawa ya minyoo aina ya Oxfendazole
0 comments:
Post a Comment