UNAFAHAMU NINI MAANA HALISI YA UFUGAJI WA SAMAKI.
Ufugaji wa samaki ni kazi ya kupanda,kukuza na kutunza samaki katika
bwawa au uzio (uliotengenezwa kwa vyuma,miti pamoja na nyavu) au eneo lolote
ambao uthibiti wake uko chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe.Mabwawa yanaweza
yakawa ya kuchimbwa na watu(japo kuwa mabwawa ya asili pia yanaweza kufugia
samaki) wakati yale yanaweza yakawekwa katika eneo lolote lenye maji mengi kama
vile ya ziwa,mto au bahari.
Ufugaji wa samaki katika kiasi Fulani si sawa na ukuaji wa samaki
katika mito,maziwa na bahari.Tofauti kubwa iliyopo samaki wanaofugwa na
wasiofugwa ipo katika huduma,huduma wanazopata samaki wanaofugwa huwekwa kwa
idadi maalumu ndani ya bwawa,kupatiwa chakula na kuhudumiwa vizuri.
Ufugaji wa samaki sio kitu kipya kabisa hapa Tanzania,baadhi ya watu
wamekuwa wakifuga samaki kabla ya hata kupatikana kwa uhuru wa
Tanganyika.Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kwa samaki
hao,hivyo kupelekea mavuno hafifu katika ufugaji huo.kwa miaka ya hivi karibuni
serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imekuwa ikitilia mkazo katika
utoaji wa elimu (ugani) ili kuboresha mafanikio yake yaweze kupatikana kama
nchini nyingine zinazotekeleza miradi hii.Kupitia muongozo wa mafunzo haya kila
mtu atafahamu faida ya ufugaji na namna ya kuwafuga samaki wake ili waweze
kukua vizuri na kumletea tija katika shughuli hiyo,na pia kuwa ni sehemu ya
ajira hasa kwa vijana wazee walio katika umri wa kuustaafu hali itakayo
wasaidia kujiingizia kipato na kuishi bila shaka yeyote ya kipato.
Kwa sasa samaki ambao hufugwa zaidi katika maji baridi (maji yasiyo ya
chumvi) ambayo vyanzo vyake ni kama vile ya ziwa,mto,chemichemi ,kisima ya
bomba,ni sato/pelage (Tilapia) na kambale (catfish).Kwa upande wa samaki
wanaofugwa Zaidi katika maji chumvi(bahari) ni mwatiko/mkuyuyu (milk fish) na
Kamba (prawns).
...................................................................................
...................................................................................
0 comments:
Post a Comment