Ng'ombe aliyekufa kutokana na Ndigana Kali
UGONJWA wa Ndigana Kali au kitaalam East Coast Fever (ECF) hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, nyati na nyati wa India wakaao kwenye maji (Water Buffalo).
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea (protozoa) vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo husambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanao kamaRhepicephalus Appendiculatus.
Kwa
kawaida, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya
wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa
mengine.
Ndigana
Kali ni ugonjwa ulioenea sana hapa nchini kwetu na Afrika Mashariki,
ambapo ng’ombe huanza kuugua siku 10 – 25 (wastani siku 14) tangu
kuambukizwa.
DALILI ZAKE
-Joto kali hadi kufikia 42c badala ya joto la kawaida la ng’ombe la nyuzijoto 38c
-Homa kali
-Mnyama kushindwa kupumua vizuri
-Kukohoa
-Kuharisha
-Kuvimba matezi ya shingoni
-Manyoya ya mgongoni husimama muda wote na huwa na rangi ya udongo (brown) kwa mbali
-Kutoa makamasi laini
-Kupe aina ya rephicephalus appendiculatus wataonekana ndani ya masikio ya mnyama (sio lazima)
-Mnyama hushindwa kula vizuri
-Pua (muzzle) huwa kavu bila unyevu unyevu.
MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za PARVAQUONE auBUTALEX kiasi cha ml 20 (soma
kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada ya siku moja
kupita, yaani akichomwa leo unarudia dozi kesho kutwa.
Pia mnyama achomwe dawa yaOTC 20% kipindi chote cha matibabu.
Dawa
aina ya BUTALEX ni maarufu sana hapa nchini kwa ajili ya kukabiliana na
ugonjwa huu, ni muhimu dalili za mwanzo zinapoonekana kumtaarifu
mtaalam wa mifugo na ikithibitika ni Ndigana Kali tiba ianze mara moja
ikiambatana na OTC 20% ili kushusha homa.
KINGA
Kinga kubwa ni kuogesha mifugo yako mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo.
Dawa ijulikanayo kama PARANEXhupatikana katika maduka yote ya kilimo na mifugo. Dawa nyingine nazo zinafaa kuogeshea kwa kufuata masharti ya mtengenezaji.
..........................................................................................................................................
..........................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment