Ufugaji Mseto wa Sato na Kambale
Polyculture ni uzalishaji wa samaki aina mbili au zaidi
ndani ya mazingira ya maji. Kwa kawaida polyculture hutokea katika mabwawa. Samaki
aina ya kambare na sato wanaweza kutumika. Aina hizi za samaki zinafaa na huleta
mafanikio mazuri.
Aidha vigezo vya kuchagua samaki kwa ajili ya polyculture ni hivi hapa chini;
- Kiwango cha juu ukuaji wa aina ya samaki;
- Samaki wanaohitajika kwa wingi katika masoko;
- Chagua aina wale ambayo wana kiwango cha juu cha ukuaji na kiwango cha chini cha vifo katika ukuaji;
- Aina ambayo hawakupatwi na magonjwa kwa urahisi.samaki ambao ni phytoplankton vorous au omnivorous.
Katika polyculture,
masuala ya kuzingatia ni kama vile Chakula, Mavuno na Masoko yanahitajika
kwanza.
Msongamano wa samaki katika bwawa unaosababishwa na uzalianaji wa Sato (Oreochromis niloticus) ambao husababisha mashindano katika kula chakula na matokeo yake ni mavuno
ya samaki kuwa wadogo sana na thamani yao kushuka chini katika masoko.
Moja ya mikakati ya kudhibiti
kuzaliana kwa wingi kwa sato katika bwawa ni polyculture.
Miaka michache iliyopita ,Kambare (Clarias gariepinus), wamechunguzwa na kujulikana kama wana uwezo mkubwa
katika polyculture.
Hata hivyo, idadi ya Sato inaweza kupunguzwa kwa ufugaji mseto wa Sato
pamoja na samaki Predator.
0 comments:
Post a Comment