script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




https://www.mshindoveterinarycentre.com/
DAWA ZA MIMEA TIBA KWA KUKU WAKO
1.Shubiri Mwitu-aloevera.
  Huu mmea una majina mengi sana kutegemeana na eneo ulilopo wanauitaje lakini kwa kingereza unaitwa aloevera.
*unatibu
a)kideri/mdondo_Newcastle disease.
b)homa ya matumbo_Fowl typhoid. c)mafua_Infectious coryza.
d)kipindupindu cha kuku_Fowl cholera.
Jinsi ya kuandaa;
   _chukua majani 3 had 5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa mda wa saa 12 had 16, wape kuku wanywe kwa siku 5 had 7 mfululizo. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.


Tahadhari; unapoyachuma majani yake mojakwamoja/papohapo unayaweka kwenye kikopo kinachotunza ule utomvu unaotoka usidondoke chini maana huo ndio unadawa nzuri yenye high quality 100%./ubora mzuri zaidi.
....
   Kama kuku anaumwa sana hawezi kula au kunywa, anasinzia, mpatie ule utomvu kwa kummiminia kinywani na pia unaweza kumuweka kwenye jua atapona mda mfupi huu utomvu wake ni imara zaidi.(unarangi ya njano).
Nb;
Kuku watapata kinga ya uhakika pale tuu unapomjengea mazoea ya kumpatia kila mwezi au mda ulioupangilia mfano kila miezi miwili, mwez, wiki tatu, n.k
Huu ndio mmea wenye kinga nzuri baada ya mlonge unafuata ule wenye majani ya miiba.

2.Mmea wa Mbarika(nyonyo)
*Mmea huu hutibu uvimbe.
Jinsi ya kuandaa;
   -weka majani ya mbarika ndani ya majani ya mgomba kisha utaweka kwenye jivu la moto.
Matumizi;
-utakanda sehemu yenye/zenye uvimbe.

3.Mmea wa mwembe.
*Mmea huu hutibu;
  -Homa ya matumbo au Fowl typhoid.
  -Mafua au Infectious Coryza
  -Kinga ya kideri/mdondo au Newcastle disease.
*Jinsi ya kuandaa;
   -Chemsha mikono miwili ya majani au mizizi ndani ya lita sita za maji hadi kubakia lita moja. Kuku Wapewe kwa siku moja.

4.Mmea wa Mwarobaini.
  *Mmea huu hutibu magonjwa yafuatayo;
   -Typhoid. Inaweza kuwa fowl typhoid, Avian paratyphoid au typhoid zingine zote.
   -Huzuia Kideri.
   -Kuharisha.
   -Mafua/Infectious Coryza.
   -Vidonda.
Tumia majani/maganda/au mizizi yake. Mikono miwili kwa lita moja.

5.Kitunguu swaumu.
*Kiungo hichi kinatibu;
  -Mafua, hichi ndio chenyewe kabisaaaa.
  -Typhoid/homa ya matumbo
  -Kuharisha kinyesi cheupe.
*pondaponda na changanya na maji lita tatu hadi nne kwa kitunguu swaumu kimoja.

6.Mmea wa Mtakalang'onyo (Eurphorbia)
  *mmea huu hutibu;
   -huzuia Kideri/mdondo
   -Gumboro.
   -Ndui.
   -Kuhara damu(coccidiosis).
   *maandalizi;
    -Chuma majani makubwa 3 had 5, pondaponda kisha weka ktk lita 10 za maji kwa masaa 12 had 16. Chuja kisha wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine (baada ya masaa 12 ya matumizi)
   *mmea huu unasemekana kuwa na dawa nzuri zaidi kuliko aloevera.

7.Pilipili kichaa/mbuzi/kali.
*Hii hutibu;
  -mafua
  -huzuia kideri/mdondo
*ili kuzuia kideri.
-Mchukue kuku miez mitatu na umwangalie mkiani kuna kaupele/jipu linalotoa usaha, kata na wembe mpya wa dukani na kitupe kile kijipu, baada ya hapo katakata eneo hilo kuelekea chini na kamua kutoa usaha. Paka pilipili na baada ya hapo panyunyizie majivu na umuachie.njia hii ni njia ya asili katika kutoa chanjo ya kideri iliyokuwa ikitumiwa tangu na mababu zetu kwa kuku wao.
*ili kutibu mafua
Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa mda wao.
    Nb;
      Pilipili inasemekana inatibu magonjwa mengi lakin bado haijulikan inatibu magonjwa yapi hasa.

8.Mmea wa mnyaa (Cactus)
*Mmea huu hutibu;
   -vidonda
   -Uzazi.
*maandalizi;
-Angalia hatua za kutengeneza aloevera.
-unaweza pia kupaka kwenye vidonda.
*Mmea huu unaweza kutibu magonjwa mengine lakin bado sijaujulia vizur.

9.Mmea wa Mlonge.
*Mmea huu una vitamin nyingi sana hasa A na C.
*hutibu;
-Mafua.
-Huzuia kideri/mdondo.
-Kipindupindu cha kuku(fowl cholera).
-Homa ya matumbo (fowl typhoid).
-Magonjwa ya ini.
-Huondoa sumu mwilin, kama chemichal zinazojijenga kupitia antibiotics, n.k
*maandalizi;
-Chukua majani mikono miwili kisha yapondeponde na kuyaweka katka lita 10 za maji na iache kwa mda wa masaa 12 had 16 ndipo uwape wanywe. Baada ya saa 12 mwaga na tengeneza nyingine. Wape siku nne mfululizo.
 Jenga tabia ya kuwapa kila mwez ama miez miwili.
 ..........................................................................................................................................

0 comments:

 
Top