*Tumia Dakika 15-30 Kuwakagua Wanyama Wako Ili Kugundua Wazima Na Wagonjwa Asubuhi Na Jioni.*
*Akiwa mzima utakacho angalia ni:-*
*1.* Anachanganyika au amechangamka kama wenzake.
*2.* Anakula kwa raha na uhuru.
*3.* Kinyesi chao ni cha kawaida.
*4.* Upumuaji wake ni wakawaida.
*5.* Mbawa na manyoya viko sawa/kawaida.
*6.* Mwendo Au Utembeaji Wake Upo Sawa.
*7.* Pia Unapoingia Bandani Wanakukimbilia Wakijua Umeleta Chakula Au Unawafungulia.
Kama Kuna Watakao Zubaa Waangalie Kwa Makini Sana.
*8.* Kwa ng'ombe angalia kama anacheuwa vizuri (chewing).
*9.* Kwa ng'ombe angalia tezi zipo kawaida.
*10.* Macho yote ni mazima safi pasipo na machozi au matongotongo.
*11.* Pua na midomo viko sawa.
*12.* Sehemu za haja ni safi na kavu muda wore.
*Utakapoona Kinyume Na Hapo Juu Mnyama Wako Atakua Hayupo Sawa*
*NB.* Kumbuka Kufanya Ukaguzi Kabla Ya Usafi Na Kuwalisha Na Fanya Ukaguzi Baada Ya Kuwapa Chakula.
*Hii itakusaidia kugundua ugonjwa mapema na kuwahi tiba/kutoa taarifa kwa Dr Wa Mifugo na kuokoa maisha ya mnyama wako.*
*Pia Ni Vizuri Ukawa Na Mtaalamu Wakukutembelea Mara Kwa Mara Sio Lazima Mnyama Awe Mgonjwa Ila Kwa Ushauri Na Maboresho Tunaamini Kuna Vitu Huwezi Kugundua Ila Mtaalamu Atakapo Fika Ataweza Kuviona Na Kukupa Ushauri.*
*_Usafi Ni Kinga Namba 2 Ya Magonjwa_*
0 comments:
Post a Comment