HAWA NDIO MBWA WENYE AKILI ZAIDI DUNIANI
WANYAMA wa wa kufugwa wao wa aina nyingi sana. Wapo ambao wanafugwa kwa ajili ya kitoweo, wapo wanaofugwa kwa mapambo, wapo tunaowafuga kama wanyama-kazi, na wapo pia wa mapambo ambao tunawatumia pia kwa ulinzi.
Ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, sungura, simbilisi au sili, kuku na jamii zote za ndege, hawa tunawafuga kwa ajili ya kitoweo.
Mshindo media inatambua
kwamba, wanyama wanaofugwa kwa ajili ya wanyama-kazi ni punda na
farasi, lakini pia ng’ombe anatumika kama mnyama kazi kwa kuvuta
mikokoteni na kulima kwa kutumia plau pezi, wakati ambapo farasi anaweza
kutumika kwa usafiri huku punda akitumika kubeba mizigo na hata kuvuta
mikokoteni.
Paka anafugwa kwa ajili ya mapambo, lakini ni mlinzi pia kwa sababu anapambana na wanyama wadogo waharibifu, hususan panya.
Sungura nao wapo wanaofugwa kwa mapambo na wapo wanaofugwa kwa nyama na mambo mengine.
Mbwa
ndiye mnyama ambaye kwa asilimia kubwa anafugwa kwa ajili ya ulinzi,
japo mara chache hufugwa kwa mapambao kutegemeana na aina ya mbwa
mwenyewe.
Mshindo media leo inazungumzia kuhusu aina mbalimbali za mbwa, hususan wenye uwezo mkubwa na akili kuliko jamii nyingine.
Unaweza kushangaa, lakini wanyama hawa ni werevu na aina zifuatazo zinawaelezea kwa kina zaidi;
1 - BORDER COLLIE
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHm-SaYfOIIX0SYFjc003O6jWghAr4xHovK5vA_HejGVqAS4Svt4UQYkwG3AEW6l5vx4NawDaIqkp1g-y8ZYqYojYhpNYsEYH1eXijZAF4UvTjCWtTVBHKRsJn2pBdxe9t2eTw80LT_Bvr/s640/Blonde_Border_Collie.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKnlf56pttGUT-I1H5KmQGmyLLQ7hEeFXInD5GKHw7b2HpXGwSiGp2Q9opQnQindqytom8u9n3sdH5yxRzYmyk2r-XB28-aWT30yOJLUEUoYYbyvOag386KoJMDh4ypK4xSUnqyL_hhVRW/s640/BORDER+COLLIE2.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJ8q9d9BzMLtpup5MIqDSQt5dibxi4rrljjkieFXwR-ehZqA7c_6OBSfhKYPZRUVjz0BHRYPaQkNWA7Hy6QaEcfnn1plSFpb2ZgZhr8Akg5pkOL9LNwE_-gX9KJP1NEidtqEQ4_n5-zMsK/s640/BORDER+COLLIE4.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEibsoEJ_FOoWcYQdGzmcKxS1nINL4bAsqmH9G5vUGWRDObs-G1-Q-RLpHpz0jC3T1gm23E9YPLKk5KivS9BT9ssC4rrAJVPlINd9lY2rXze8YsDzlKLOtmhOqIsvLWIhlrLw4ohbMvC5xIh/s640/BORDER+COLLIE5.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvZYkLckQHMB35ouKcer616H37V2IMTnpKLcsYbE8lKDqqZJC7BuME9xXUcaPwbTzJ3rl1t-q95BRbWVuK4KYEbcPl07I2W-g0UxL4UstpKm39ESjyLG8ungNoYEyxW_LLSZOi2qroaR7W/s640/BORDER+COLLIE6.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWivCgPKzsxT07BQyejtCDLxAT6hIZC7btaMSy5ZZHdnMIIc5o0oMyfByL9KA0RFiyefD6Ero3xAp8CPA0ArodxnUJXXGOJsCDc5rjMyOLUCzjKgkEeunm9V9ntkIX9keLbIOelOzdKieG/s640/BORDER+COLLIE7.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqu9jUQ_9N_Cc5peF8AGH6LQOHM1Y5lKBXQATZomaf1G6IxmuHPAnOcPmu1JYT0MSQmhKHLSRzwE-BZJlBo-mZPjTpOrrYbkMd6rabeIxZaKRXvRSSEU_YRUSO4H8ziZ8utgAQjOC4oTz-/s640/BORDER+COLLIE.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinhDdeJQDCDeJVJIcM5_m_4wTQFEE0z5fmywels_HWLxJWj7iui2tdAqxRa8O01Da-Jr7pAyOkYItjmCBmYLsV9EdYyPXgGbiwwQdzh7vgZER-abtlaK20z2ymlXesgpqEhrwC8rbh58ln/s640/Border_Collie_%2528Roy%2529_en_plein_travail.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyd0_KMYdH37BLxxsfJ06qLYQgju102gUOZpONHzc4MRDDMVuYvfhcBcBrvTzNJ2ENAQBd8UUcxGw_KfXaPzdYp6p6-eNsb0_xEoPYGsZ5u3Q6pUtVjXTeJxpai1IUM8JqwhqUU7tCc8kw/s640/Border_collie_of_nonstandard_appearance.jpg)
Mbwa
jamii ya Border Collie walianza kufugwa kwa nia ya kukusanya na
kuchunga kondoo katika eneo la milima la mpaka wa Scotland na England.
Mbwa hawa wanafahamika kutokana na mtazamo wao, yaani macho, ambao
huutumia kulinda kundi la kondoo.
Kondoo wenyewe wakiwaona tu wanatulia kwa namna wanavyowatazama.
Mbwa
hawa wana nguvu nyingi, stamina, na wana bidii ya kazi, mambo
yanayomfanya awe mbwa bora zaidi kwa ajili ya kuchunga, na ndiyo maana
anaitwa mbwa mchungaji; mpaka sasa bado anatumiwa kuchunga kondoo katika
mashamba makubwa na ranchi za wanyama ulimwenguni.
Mshindo media inatambua
kwamba, mbwa wa jamii ya Border Collie aliyefunzwa kwa kiwango kikubwa
na mwenye akili pia anaweza kushiriki katika mashindano na michezo ya
wanyama, kama utiifu, kuruka, kukimbi, kukimbiza mpira na mashindano
mengine kama hayo.
Kwa ujumla, mbwa jamii ya
Border Collies wana maumbo ya kati na ngozi ya rangi mbalimbali,
japokuwa rangi nyeupe na nyeusi ndiyo maarufu. Mbwa dume wa jamii hii
ana urefu wa kati ye sentimeta 48 hadi 56 wakati jike ana urefu wa kati
ya sentimeta 46 na 53.
Mbwa wa jamii ya
Border Collies ndio wanaotajwa kuwa na akili kuliko wote duniani na
imekuwa ni jamii maarufu kama mbwa wa mapambo kutokana na kufundishika
kufanya mambo mbalimbali.
Mbwa hawa wanaweza
kuishi kati ya miaka 10 na 14, ingawa wastani wao ni miaka 12. Chanzo
kikuu cha vifo vyao ni saratani (23.6%), umri mkubwa (17.9%) na matatizo
ya ubongo (9.4%).
2 – POODLE
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgUxdevzzGTw1gGtePhzeLxOpmBR0mtH9j3TP4GJiz6O497mY2S3nS6mqJkJGZMiiQtpes8NtR-jT_7ppJO1n7QTF_MZoW74qHaLtDiFlYhyizKq3JfvOb9uesomfpvWXWR89Q18aWNqh3r/s640/POODLE.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhI4POn_GxC7Y9uVimBYRi7qo0sr_s_0hzJ-2KDqXUXD1j_NDAhJ1AufbsS5gaz5bJv-PmTtXhqzDADZy6bFUp7MXXFAtf9daPXWzBgHgcR2bxD6A0nJki7MgdctwbCcgppf6NI_aOCqilx/s640/poodle_apricot.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLvM1Fi32MFXha7wzdkkktA6y_gyWpR2sy-fP_lf7WPqg_ZmrCGCXITHSGUjMfRgm4L_NRXHN7Fyn43HEpo1m8PZsT5eTjbq2ybzG_n2mhOTmASMevHxpkGuzjdhqeDnuXuuBLvUieZxm3/s640/poodle_retrieving_a_duck.jpg)
Mbwa
wa jamii ya Poodle wako kundi la mbwa wa kawaida na wamegawanyika
katika makundi matatu au manne ambayo niStandard Poodle, Medium
Poodle,Miniature Poodle na Toy Poodle. Wanapatikana katika rangi
mbalimbali.
Mshindo media inajua
kwamba, mbwa hawa wanashika nafasi ya pili kwa kuwa na akili nyingi
nyuma ya Border Collie, lakini jamii hii wana uwezo mkubwa wa kushiriki
michezo mingi ya wanyama pamoja na shughuli mbalimbali, wana
Toy
Poodles walishinda mashindano ya "Best in Show" mwaka 1966 na 1982.
Standard Poodles walishinda katika miaka ya 1955, 1985, 2002 na 2014.
Asili ya mbwa hawa inatatiza ingawa inaelezwa kwamba ni Ujerumani ambako walikuwa wakijulikana kama Pudelhund. Neno Pudel linatokana na lugha ya Kijerumani likimaanisha ‘kumwaga’, na neno Hund (maana
yake mbwa). Wengine wanasema asili yake ni Ufaransa kutokana na mbwa
aina ya Brbet ambaye inawezekana alipandishwa na jamii ya mbwa kutoka
Hungary. Huko Ufaransa wanafahamika kama retriever kutokana na kutumiwa
kutafuta vitu majini na wanajua kuogelea.
Mbwa wakubwa, yaani Standard Poodle,
ni wawindaji wakubwa na wanaweza kuwinda hata ndege, wanaweza kuruka
kwenye mashina ya miti na kadhalika. Wana akili sana kiasi kwamba
wanapoelekezwa wanaelewa mara moja.
Katika maandiko na tafiti mbalimbali ambazoMshindo media inazo,
mbwa wa jamii hii waliwahi kutumiwa hata kwenye vita kuanzia karne ya
17, na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia walitumika pia hasa kwenye
majeshi ya majini.
Katika kipindi cha miaka
20 iliyopita huko Amerika ya Kaskazini, mbwa wa jamii ya Standard Poodle
wamerejeshwa kwenye kazi yao ya mwanzo kabisa kama wawindaji wa bata na
ndege.
Umri wa kuishi wa mbwa hao ni kati ya
miaka 11.5 hadi 12. Vyanzo vikuu vya vifo vyao ni saratani (30%), uzee
(18%), GDV (6%), na magonjwa ya moyo (5%).
3 - GERMAN SHEPHERD / ALSATION
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVuOebTGwjfw7QobaoOaSmKWH6YdFdYY0d5T4mh-5LBWek-G0LVaCZ_7KHxXTFDbV5Ee-8sTs5To4hGeXBe5Saors5t3OoU2ThUUS6UhWaiB3gW6GVWhObg2K3LM9QuSLMZT5miq6BMEWb/s640/GERMAN+SHEPHERD+1.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJ0drWzIP7GyBDoc8uFi6jgXVz8NG-N57BiizOpsoeI7ILyViIeGLwcA9-8HJUllXa-yrSjJtACSZMV6Z1lYH-HmRCb-wuA5QyHH9ymZN1O7N5CQ77Kuzxohejn0RjBWPED4TKLqg1YaM-/s640/GERMAN+SHEPHERD+2.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4FiqyttItYYPELTUgSW0pTOAwy5pPjMoicv85qzM2axIKQGn6I4daQi56zxWbUC2MEB9KOU37DZDvxV3UJa9suVmZlgT637LjxozvFNLHzQwBXiDu8CLq5-GBDQuyQ7LcMrlFzxB2oK__/s640/GERMAN+SHEPHERD+3.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0ew0hFjgsvKN_HucPfuAMdWQPBCBL4hwY0Nauifihx0DpAHfYj1m9teYZZfj8GycAThPitYxpOftB2H1voZFX_vbKj5QiWVuxjY0xVRJ07LqeIaZyBBjYHxyfVaaZHu3iPb7JG1KV7fI6/s640/GERMAN+SHEPHERD.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvJ3zF2kspScJ49IUxju7ja-GDpKAvwz2pUQ_1ireYCTjtCRXDg8sl_b4pSigpv_IDfpTQxtrvPheEmMZGL127ijuyX71ZjoO1xxN2uj5C5SHOTxCRrW37o-EQTTJhdEkg7hDJ_r-upetc/s640/german+shepherddd.jpg)
Mbwa wa jamii ya German Shepherd (Kijerumani: Deutscher Schäferhund) ni jamii ya mbwa wa maumbile ya kati na makubwa wanaofanya kazi ambao asili yao ni Ujerumani.
Awali huko Uingereza walijulikana kama Alsatian.
Tangu ilipoendelezwa mwaka 1899, jamii ya Mbwa Mchungaji wa Kijerumani -
German Shepherd – walikuwa wakitumika kuchunga kondoo.
Tangu
wakati huo, kutokana na nguvu zao, akili, uwezo wa kufundishika, na
utii, mbwa hawa wanapendwa ulimwenguni kote kwa ajili ya kazi
mbalimbali, ikiwemo kuwasaidia walemavu, kutafuta na kuokoa, polisi na
majeshi pia yanawatumia sana. Ndio wanaotumiwa hata kukamata dawa za
kulevya, mabomu na kadhalika.
Mbwa Wachungaji
wa Kijerumani wana maumbo ya kati na makubwa. Kimo chao ni kati ya
sentimeta 60 – 65 kwa madume na sentimeta 55-60 kwa majike wakati uzito
wao ni kati ya kilogram 30 – 40 kwa madume na kilogram 22 – 32 kwa
majike.
4 - GOLDEN RETRIEVER
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh0Mfk6NjskgOUbnhYRHTcUcDrkkEz-5lsWiEjFEgBgzV4iyBmhFExg9zccRVcad7fS54mUVFOwdAoEwHl-PFQLqH_Gt-YxYeLbQIBmA3Z6zO1C5JMLRqRDUqJ7Px8yxPGeivbuqIoJnYyP/s640/Golden_Retriever1.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgumaEEKUg9pVWsSIlMgm6VGA2lhGjTv3-fUf5DR87NHsa50D-EEU9B5rzlrDNF3yBeRhbkZI4VKhELfS0zWdIulBKCJiA16VboXdBCfL-I2RfYPleoD7A-qVBiVfQVZwQQqUlaIUQ2xTtX/s640/Golden_Retriever3.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiY2Z1K1ommYDsY8QiFD-26TcqvluIwFA2nU6rtFaeBdSEsu1FULiEaZ7KeBCsSDvlU-W87UDZj83v60BA1p1ixQN8Rk25kJEVJF6peKNkuWdn6E-dIPggz-KX-QeZGh7jXGJgZEgqndyyj/s640/Golden_Retriever_Carlos_%252810581910556%2529.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjh9W0Yf38b2l8AirEqFPioianvyBvwVx3yDeBX8TH9P3P-62XyavawAFgBFFABKAkpAFtqX-SqApEDQEPQtUan-_PWAc_6RqFtqNFZnset4pghP9-joqEqfCNIJQG0ZlxthnnrpyTg5G8b/s640/GoldenRetrieverSnow.jpg)
Golden Retriever mi
jamii ya mbwa wakubwa wanaofugwa kama mbwa wa bunduki – gun dogs – kwa
ajili ya kutafuta na kukamata mabata maji na ndege wakati wa uwindaji,
na waliitwa watafutaji kwa sababu ya uwezo wao wa kuwakamata ndege bila
kuwadhuru na kuwapeleka kwa wahusika.
Mbwa hawa wanapenda sana kuogelea majini na ni rahisi kuwafundisha misingi na mbinu za hali ya juu.
Mbwa hawa ambao wanajiamini sana, wana uwezo wa kuishi kati ya miaka 11 na 12.
Asili
ya mbwa hawa ni Scotland katikati ya karne ya 19. Wakati huo uwindaji
wa kanga ulikuwa mchezo maarufu kwa matajiri wa Uskochi.
5 - DOBERMAN PINSCHER
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGqpINqQY7boU3qQ-MX_zRFq748ysWUnCi3iiJwLmW7BT8Xs_bdNSwGZso1WadwfAypprOp769PZulOznmfVko1Gxp7L7OhjYKYHAC7qhbSZgX55UCgVdnM2QESerj4-cs_Be4-16j0Jxj/s640/Doberman_Pinschers_black_and_blue.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWC-lFfVMY95mtYyM5XCtLTagwySwU8gV33oZEnwCYM9fVWAqKACLUolNe9jpIJWu6DWCbbttKrT6nW67saOyEkPIlz-u078-27D0AQ8AjxK9vU3-MHIpki9hpwcQv-qNOcIsa9i2g_AsT/s640/Dobermann1.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEP-0quDeu_PwONYno3e0l8VA4ShkRx1yrnnWST0jUSgGUNcE0bYOaylkdsWz6YyxIevaoHdcpONjHWXLLeVHOKidBmEm2h69_wglNzS_4TpZRCp91CKGOF0XUEMG0_NNYIv4Q-NHFc7mS/s640/Dobermann.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhxxodoOiJkyLKfdMTmw1C9-EUqxEvG5-5VzYhtZxGdEKzwfyIRtQC3mwX7b61_jPcSJy0uxwube9-7oetDEjYkjd9j97_GgQ7X8iaQsYbd73MiX6DwjMcmzfx2d175ZBFDfsettX8Ksg2T/s640/Dobermann_Black_and_Tan_%2527Vito%2527.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnLH8DUTW570ZOiTvC0iLGXIaj-JWUQGRwjuFxq3qIf-qPYO1NAHJQgByIpbYba_MWQhbVtv0Hb0lrofrxuOidShpgYTSDTZo6u6vJE6IIV33gPlrzkFwkclkC04ghC71Vx2trCFsIMxp8/s640/Dobermannhuendin.jpg)
Mbwa jamii ya Doberman Pinscher wana maumbile makubwa ya kati na walianza kufugwa mwaka 1890 na Karl Friedrich Louis Dobermann, mtoza ushuru wa Ujerumani. Meno yake ni marefu na kama watang’ata basi wanaleta madhara makubwa.
Mbwa
wa kawaida wa jamii hii ana urefu wa kati ya sentimeta 69 hadi 72. Dume
mara nyingi huwa na uzito wa kilogram 40 hadi 45 na jike kilogram 32
hadi 35.
6 - SHETLAND SHEEPDOG
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLPdh00dfnkwf82ZrGUIyNMvtqF6rewbHcMzxfBsqAsANZWBs9ORmKAXW34sqlNDEo1s3o3tkvEhHvaF3_i4UiGcndLI-3NytWSJMRmakBGbCI91YJUoq-qf1mKLEpw5Q55LnjK5dXJ010/s640/Shetland_Sheepdog7.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEigd61cHgq5SInGM72Lc-lMFKlQE0vd8ypgptlZG5wLoGXkOYG4wvj8_HmArf-99dCbEmnWVzCzQcjAitamElow934Si6uzN8EhCUiT4NJ4SLybaZBYN-c4V7NgcAYrUKdafUMnIhvNA-mA/s640/Shetland_Sheepdog_600.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUf0CQkHLbcxQlG7ZBm0YeV8YwXtDlGygDiQR9LDgF8Rk7w-HGuSk423T8oagVwuVphoAVN_j9xESlR-yGGF2l9KkyP7LGYDhoZOlfQwJOaoowLoERMpE_Ine3qU75bwc7cxg9KxnqbUEt/s640/Shetland_Sheepdog_and_Rough_Collie.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmmOwZJ5R2aA8FSvABF75llQRoIzaE6_8rH4tUOP6AIXAKrjDksidOH27sHwSy9ErBgpNsm8dLcI0OvrL9OrIoB-6qVsSVxN8M_YtR0JaQQXwXylPejvrkPPPdSqeRoajqNBBlt7P_nnIU/s640/Shetland_Sheepdog_black_bicolour_agility.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6sq21hgUxwsMjWN6CcrkXEmX1zLWKzy26rl924x6woggzQfHNSJO189k1keIBvypXDc78FpIfwgdVp6HBZ7_12GGDva9lMCgIdWjnOWCoadeJmrD9bI9fklkmIa_bMmceT632jqIcDnJk/s640/ShetlandShpdogBlue2_wb.jpg)
Shetland Sheepdog, au Sheltie, kama jina lao lilivyo, ni mbwa wachungaji. Jina la asili la mbwa hawa ni Shetland Collie,
lakini hili likaleta mkanganyiko miongoni mwa wafugaji wa mbwa jamii ya
Collie wakati huo, hivyo jamii hii ikaitwa Shetland Sheepdog.
Kulingana na tafiti mbalimbali ambazo Mshindo media inazo,
mbwa hawa wadogo kwa maumbile wana akili, wanabweka sana,
wanafurahishhah, wana nguvu na wanafanya kazi kwa nguvu. Jamii hii
ilitambuliwa rasmi la klabu maarufu ya jamii za mbwa ya The Kennel Club mnamo mwaka 1909.
Historia
yake ya awali haijulikani vizuri. Japokuwa kinachojulikana ni kwamba
mbwa wa Sheltie ni kutoka katika uzao wa Collie. Sheltie ni uzao wa
mbegu ya mbwa jamii ya Scottish Collie na King Charles Spaniel.
Iliendelezwa kwa nia ya kuchunga kondoo katika Kisiwa cha Shetland,
ambako fukwe zake zenye miinuko zimesababisha kuwepo kwa wanyama wengine
wadogo.
Lakini leo hii Sheltie ni mbwa
wanafugwa kwa ajili ya ulinzi shambani na kama wanyama wa mapambo. Awali
walikuwa wadogo sana wakiwa na kimo cha inchi 8 hadi 12 kutoka mabegani
kabla ya kuwapandisha na jamii ya Collie kupata jamii ya sasa.
Kwa ujumla, mbwa wa jamii ya Sheltie wana uzito wa kilogram 5 hadi 11. Madume yana urefu wa sentimeta 37 na majike 36.
Sheltie wana uwezo mkubwa wa akili na wanashika nafasi ya sita kati ya jamii 132 za mbwa duniani.
Japokuwa
ni wafupi, lakini wanaweza kuruka hata kwenye ukuta wa urefu wa meta
moja na nusu na wanashiriki katika michezo mbalimbali ya mbwa.
7 - LABRADOR RETRIEVER
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgbLifi7uflOG-5Z2683rFufA2VTNCQfx11moIEG1ZSGjOJJtGh0d5gxVP2M_EBR8l6ZCbuWD6-5Kxtd1F2Op0b6agic_uFoKL9QFWP5HTyJEcGGNdxGxeb3wuRhwTbvP0CJuBErwnvKieo/s640/Labrador_Retriever2.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnxIrbbkNlDbcXaigZdJgsbdgPW0JNYXYzVCsC68K3I8KfKiR56_Azq4X3gZHWVZY2-3uPFblc093j7O9uEhVd-m_lMwKj9-h1T5n0UhXR05h75-tZ21CsyrACocKorViIvv4xCC7BNQtv/s640/Labrador_Retriever+Endal_Dickin.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhfnB8x_HqUBxG52VFiKU2AX2ot-i7WojxHuzs1r5knJOczx6caSCUdEp9rMdY5AYpe5tCGKnuT9Ow9m0bcIYqZPbqk425aa1cYbcg_Ri_9-u6l55rTz6b8LUwcCDMrNhSCWdrqR0CyPfC/s640/Labrador_Retriever_Chocolate_Brown_Portrait_-_Sam.jpg)
Mbwa wa jamii ya Labrador Retriever, ambao pia wanafahamika tu kama Labrador, wako katika kundi la mbwa watafutaji na wachunguzi. Jamii hii ya mbwa ni miongoni mwa mbwa maarufu Marekani na Uingereza.
Kutokana
na uwezo wao, Labrador wanafundishwa kuwaongoza wasioona katika nchi
nyingi, lakini pia wanatumiwa na polisi katika sehemu mbalimbali kwa
ajili ya kunusa vitu vya hatari zikiwemo dawa za kulevya na kadhalika.
Awali mbwa wa Labrador Retriever walifahamika kama St. John's water dog,
mbwa wa St. John, au Lesser Newfoundland. Wakati mbwa hao walipopelekwa
England katika eneo la Labrador ndipo wakaitwa Labrador Retrievers kwa
sababu walitumika kuzamia na kutafuta vitu kwenye Bahari ya Labrador.
Mbwa
wa Labrador wana maumbile ya kati na makubwa, huku madume yakiwa na
uzito wa kati ya kilogram 29 na 36 na majike kilogram 25 na 32. Kimo
chao ni kati ya sentimeta 57 na 62 kwa madume na sentimeta 55 na 60 kwa
majike.
Mbwa hawa ni wakali wanapowajibika,
lakini ni wapole kwa ujumla wake, wanapenda kutembea na wana asili ya
kuchunguza sana, ndiyo maana ni rahisi kuwafundisha hata kutafuta vitu
mbalimbali. Wanatumika kwenye majeshi ya majini na nchi kavu. Wanaweza
kufuatilia na kuwachunguza wanamagendo.
Wana
uwezo mkubwa wa kunusa na ndiyo maana hata polisi huwatumia kunusa
harufu ya vvitu mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya, kutambua
wanamagendo, wezi, magaidi na kadhalika.
Mbwa hawa wanaweza uwezo wa kuishi kati ya miaka 10 na 12.
8 – PAPILLON - KIPEPEO
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGc0r9emHCRg5tsMEdiwpysqfaRPMEEkOo6fxAN5RLyVemN9-j3uyJZL8ZQCiVRGbFUbPUNcKTG0ugbjdcHkjbW91xB9GYIUVdYfCBmhNB_myGaui1-4hVNZHNCyB4Y9xy-h7eMd7qJFzp/s640/Papillon_%2528dog%25291.jpeg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOBbPTPmWaESfTWXheVl8U5BZh21ntClv7WtFUHu0NWr0iVaSNRbjxAV1_Bg7K9NWzUKT3tJZ5ohdp3u-RP3aHIe6PysKCtc4XJWK-k75psKhqnQvz7_IsCRd0L_x6DVDADEkKdWnovrcU/s640/Papillon_%2528dog%2529.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjfxNT21W-YudyDpOiWBKT2AzeNooG-tTLl_QVYgVa4CTc-5jAmsmqsvMMWibhH3vN-MXOTLbGyDJLqowE0M2l9CIDvJgcPpkwX-Yf2VQn3np8bHf2A4Tz2HJN5yVddlAvrLj5s9llmryA3/s640/Papillon_dog_agility_jump.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTuNvwZCzx2s9Xs2pIfBcu1exdJxYOvD5xsHIHbWtoYif-K28kFsZlDHEORdVbA6p0igl5LNoFVYWplT0KKJmiM5Lp0LyIETLdtY8zbFJLQlweJoaHKOX6CJBoFQciu1Nl_2A5Vo3Q5p6h/s640/Papillon_Ears.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZMk1uo6KQ14BnigYr7z7X6xAsupz7J3nqmnAnWwPXK7YkzmZ4H6Wk1eEeCMrnVWytizjs_opb1j0060f-n1xLvGk8hNgtoU7xC6kJvh9ADCM3yYcQviGR05IA1TOB37y76BKYlgQHE7zt/s640/Papillon_portrait_Flickr.jpg)
Mbwa jamii ya Papillon ni wadogo kutoka jamii ya mbwa wanasesere wa Continental Toy Spaniel.
Pamoja na udogo wao, lakini mbwa hawa ambao ni jamii ya zamani sana
wana akili. Papillon ni jina la Kifaransa ambalo maana yake ni ‘kipepeo’
na Wafaransa, ambako ndiko iliko asili ya mbwa hao, walimwita hivyo kwa
jinsi alivyo mdogo.
Mbwa hawa daima ni
marafiki na wanapenda kutembea sana. Hawana aiba na wana nguvu. Japokuwa
ni mbwa mwenye urafiki, lakini lazima kumwangalia anapokuwa na watoto,
kama ilivyo kwa mbwa wengine, kwa sababu akichokozwa ni balaa.
Mbwa huyu, pamoja na udogo wake, lakini ana uwezo wa kuishi hadi miaka 17.
9 – ROTTWEILER
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLymcrZDO8ArT9iTtT4baf_YLN7YptSqsqgA3JLIqITrUAAp7TeCVujiHorzGUa8vJWlp6TJ3QZ4Jv2LmCjAHdotI_-a0i4fPgMZUEoCDkmj4gSeh2dWOa7_aD4V2oWhg-FfLR86Di7ghv/s640/Rottweiler1.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiAQORKIB0oR4B_ngLRhwCurWSdfscCbKdjbCM78ngb9JcRzjIY4k-Bd9TUEzf25wMiIIoD77exbOxfSKn9wBQPkDCJ7unhbwzR8QhuI_sSrwFOQ27lch5sR7sQfnFixVhPUDVC0FMSHMm9/s640/Rottweiler2.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTheDu2AhZqFaW4oYW-8ug2rSos9Of08NKhp9pyxHuxgGQaorkhli2KfuDR8EiJ8KwPkFcTuYegHMKYd77Afhl0faSrjh85ZKG1WnPx0nkudMUpgjwi4gT4vQpF8C7Zj_GaTWb5KEGNvox/s640/Rottweiler-Head.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoPtVDYR_NjXlt1j0y90K10nLyAiQ94QL4yVx1iE-Dd1zHLpIWH7sdhwpDRaXL8J_poviVHGeu_OdGO4v0Qd5JDk2HE5q75aF-ric63r7_PLJBtecFJhQvspGIwMLlrc_DrVyGrZ6EbQOd/s640/Rottweiler.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEPP9SiIgqTMb5Q4URn6ndxX6img1Zsmk2us9LT1ysAUkYpB-s_jj13URdug_1ZzaMjEkZRjQmpdNUo769yCPOv70UuwXpN_Lfkpy4gPPqAQdHaS_8S0KJpHNLcJap8RJAKr64L4CShqwK/s640/Rottweiler_herding_sheep_1.jpg)
Rottweiler ni jamii ya mbwa mwenye umbile la kati na kubwa ambaye asili yake ni Ujerumani ambako walijulikana kamaRottweiler Metzgerhund, ambayo maana yake ni mbwa wachinjaji wa Rottweil, yaani Rottweilbutchers'
dogs, kwa sababu mojawapo ya kazi zao ilikuwa kuchunga ng’ombe na
mifugo mingine na kuvuta mikokoteni yenye nyama kwa ajili ya kupeleka
sokoni.
Hii iliendelea hadi katikati ya karne ya 19 wakati wa ujio wa reli ambapo sasa kazi yao ikabakia kuchunga mifugo.
Kwa sasa mbwa hawa wanatumika kama watafutaji na waokoaji, mbwa waongozaji kwa wasioona, mbwa walinzi na mbwa wa polisi
Mbwa
wa umbile la kawaida ana urefu wa sentimeta 61 hadi 69 kwa dume, wakati
jike ni sentimeta 56 hadi 63, na wana uzito wa kilogram kati ya 50 na
60 kwa dume na kilogram 35 na 48 kwa jike.
Usicheze
na mbwa hawa, kwa sababu licha ya utii, ukakamavu, welekevu na jitihada
ya kazi, lakini ni wakali. Ukimwamuru tu, kazi imekwisha.
Kama
mfugaji wa mbwa jamii ya Rottweiler hatakuwa makini, anaweza
kusababisha madhara makubwa kwa jamii na ndiyo maana wengi wanafugwa
hata na majeshi ambako wanaweza kuwadhibiti.
Mbwa hawa wanaweza kuishi kati ya miaka 8 hadi 10.
10 - AUSTRALIAN CATTLE DOG
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrFs0FVZjXZzpDRy4eRRMkmAljuqtGHogSd7x1amrepP54RdvlucDMEAbQowusVMtZAsMwK9RTMDIbX4J0WpOXf34jeOYku5AkqmlLhVjh7HW28k18Mg6YFFcFIR7SKos-ITU6qlYHBpmT/s640/Australian_Cattle_Dog1.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxR7_H60lE6uO0rgWdM32A_4Mu63MXSJxAuMEnFoxqfPBQraprrvlzM-7k-merGtDhyBz9aUiQGThk7HpH7PGkTlqDIJ9BhU69BM05QLnsb5gPKjOIbpQ6fKIdduy0YJgVj3kJjwV5hhUL/s640/Australian_Cattle_Dog4.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjoFSddj1mebLUIn7SmS8emwAI2-9HDHLh1dAeaw2TlrJbcXyMY9tYsF4SvYp02gRty5w5qAi3c6CxA1aVu5uSrXcd1UqpqpSXnflYKQjLB_qz5l_tCUyvpaBcmU3AW0xptLpLwMvNH7L6e/s640/Australian_Cattle_Dog.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhyCrkA7JtA3FK75-C9dK6f92PUOuJW7-S4cVqk4RlAiEAWwG13B0uMQL1_ML1GNjS8g8u-xXNNosVYe4gNhW4yvNa2iZZ6keQw42HCuf6YCW_-VxTO2odnKgS3YbnRP8iAl2FpVUG-Iocy/s640/Australian_Cattle_Dog_Herding.jpg)
![https://www.mshindoveterinarycentre.com/ https://www.mshindoveterinarycentre.com/](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYvHIycCUyeDHxiyCsqNG50Y8fbZM_Rz-SpfKJ6yNwoMQT2EZBqDR5XmqU5Xit21eJOBcpIoYojAAcu-G5a_PbsvISlwGaWSZvR9fZzGfgWzLbPbWjVP5FFQHRarTzOMR8h0Re84XLasoP/s640/Australian_Cattle_Dog_puppy.jpg)
Australian Cattle Dog (ACD), auCattle Dog,
ni mbwa mchunga ng’ombe ambaye asili yake ni Australia ambako alifugwa
maalum kwa kuchunga ng’ombe katika maeneo ambayo ni vigumu binadamu
kupita kwa urahisi.
Mbwa hawa wana maumbile ya kati, wana nguvu, wakakamavu na wana akili huku wakipendelea zaidi kuwa huru, siyo kufuatwa fuatwa.
Wanaitikia vyema kwenye mafunzo, hasa kama mafunzo hayo yanavutia na magumu.
Awali
walifugwa kwa ajili ya kuchunga kwa kuwang’ata ng’ombe. Ni mbwa walinzi
wazuri kwa familia kwa sababu wanaweza kumwelewa kila mtu ndani ya
familia, ambapo kama itatokea mwanafamilia yuko hatari, wanaweza kutokea
kusaidia.
Mbwa hawa wanaweza kuishi kati ya miaka 12 hadi 14.
NI JUU YAKO, UNATAKA KUFUGA MBWA WA AINA GANI KATI YA HAWA
.....................................................................................................................................................
.....................................................................................................................................................
0 comments:
Post a Comment