script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X





Kwa miaka mingi imekuwa kawaida kwa watu wanapotajiwa ufugaji wa samaki moja kwa moja hupata picha au kuanza kufikiria mchakato wakupata makatapila au mtaji mkubwa kuchimba mabwawa.

Positive eye Co. Ltd inakuwa kampuni  ya kwanza kabisa kutambulisha Tanzania ufugaji wa samaki kisasa  na kibiashara katika mabwawa yasiyochimbwa ardhini ambayo yamekuwa yakitumika katika nchi nyingine mbalimbali ikiwemo Kenya kwa kitambo sasa, na hata sasa kampuni hii imeweza kubuni  na inaendelea na tafiti zakibunifu za aina nyingine ya mabwawa  ambayo hufaa kuamishika kwa wafugaji wanaokaa eneo lisilokuwa lakudumu au nyumba yakupangishwa kunufaika na ufugaji samaki.

Katika teknolojia hii ya ufugaji samaki kisasa, tofauti na inavyofaamika kitaalamu na ilivyosomwa na wataalam wetu wa kilimo kwa miaka mingi kuwa utaweza kufuga samaki 3-4 tu kwa eneo la mita moja mraba. Kwenye ufugaji huu teknolojia na uwezo wakuthubutu kujiongeza kijasiriamali vimebadilisha mambo, kwani utahitaji eneo la mita 4 urefu, mita 2 upana na mita 1 kina kuwezakufuga samaki 1000 aina ya kambale au wastani wa tilapia 300-400 na kulazimika kubadili maji nusu ya ujazo mara moja tu kwa wiki.

Kutengenezewa mabwawa haya utahitaji kuwa na mirunda kidogo na mabanzi ambayo yatatumika kutengeneza umbo la bwawa la samaki kwa kuinua juu bila kulazimika kuchimba chini na baada ya hapo yatawekewa karatasi maaalum yakuhifadhi maji(tazama picha hapo chini kwa uelewa zaidi). Karatasi hizi ziko za aina tofauti zikitofautiana kwa ubora na muda wakudumu, Japo wengi huanza mradi huu kulingana na uwezo wakimtaji wa mhusika lakini sisi tunashauri aina bora ya karatasi ambayo ni gharama juu kidogo kuinunua lakini inawezakudumu kwa wastani wa miaka hadi 30 endapo itatunzwa vyema

Katika ufugaji huu wa samaki kisasa samaki aina ya kambale watawezakufikia kuvunwa yaani uzito wa kati ya 1-1.5kg ndani ya kipindi cha miezi 6-8 tu, kutegemeana na sababu mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula bora ,hali joto ya wastani mzuri ambavyo huchangia ukuaji wa haraka wa samaki na maji.


Imethibitika upatikanaji wa samaki kwenye vyanzo vya asili umekuwa ukiendelea kuporomoka kutokana na uvuvi haramu, uchafuzi wa maji na kemikali toka viwandani, n.k,huku uhitaji wa nyama nyeupe umekuwa ukiendelea kuongezeka kwa kasi siku hadi siku. Tathmini inaonyesha miaka ya 1970 ni wastani wa 5% tu ya samaki walioliwa duniani walitoka kufugwa, Hivi leo nusu ya kiwango cha samaki wanaoliwa duniani ni wakufugwa, na baadhi ya wanasayansi wametabiri hadi ifikapo mwaka 2048 hazina ya samaki wote wapatikanao kwenye vyanzo vya asili itakuwa imekwisha hivyo kulazimisha uhitaji wote wa samaki duniani kutoshelezwa kwa samaki wafugwao kibiashara mashambani mwetu, hivyo kuthibitisha fursa ya kuzalisha samaki kulisha dunia na idadi kubwa ya watu inayoongezeka kwa kasi kuliko uzalishaji wa chakula kinachohitajika mwanadamu kuishi vyema


Kanuni ya kiuchumi ya uzalishaji na uhitaji inasema “mara zote kunapokuwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa yeyote  sokoni kuliko kiwango cha uzalishaji au upatikanaji wake basi bei itakuwa juu” na vivyo hivyo uzalishaji ukiwa mkubwa kuliko uhitaji bei ya bidhaa hiyo itakuwa chini. Kwa kutumia kanuni hiyo fanya ufuatiliaji utagundua nyama ya samaki inauzwa ghali kiasi cha watu wengi wa kipato cha chini  na kati kutomudu kuitumia kadiri wapendavyo. Na hiyo ni ishara yakuwa soko lake lipo ni kubwa.


0 comments:

 
Top