script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




https://www.mshindoveterinarycentre.com/
 
Iwapo kuku watapewa chakula chenye viini lishe kidogo/kisicho na viini lishe muhimu kama vile; Protini, Wanga, Madini na Vitamini wanaweza kupata madhara yafuatayo;
  • Kudumaa Kupungua uzito,
  • Kupungukiwa na damu,
  • Mifupa kupinda/kuvimba/kutokuwa imara,
  • Utagaji wa mayai hupungua na uangaji wake pia huwa hafifu,
  • Ganda la yai huwa laini,
  • Manyoya huwa machache na laini,
  • Kujikunja kwa shingo/miguu na vidole,
  • Kuwa na majimengi mazito chini ya ngozi ya kifuani,
  • Kupata magonjwa mara kwa mara,
  • Hali hii inaweza kusababisha Kuku kufa.
Namna ya kuzuia.

Kuku wapewe chakula chenye mchanganyiko wa viinilishe vyote muhimu kama vile Vitamini, madini na Chokaa kufuatana na umri/aina na mahitaji yake.
Wapewe majani mabichi kama mchicha, kabichi na majani ya mapapai.
Wapewe mchanganyiko wa vitamin na madini kama chokaa na chumvi kwa kiwango maalum maana ikizidi pia yaweza kuathiri kuku.
Ili kuzuia magonjwa ya kuku na kupata faida kubwa kwa kufuga kuku, ni muhimu sana mtu anayehudumia kuku bandani aweze kutambua haraka dalili za magonjwa ya kuku kama nilivyoeleza hapo juu ikiwa ni pamoja na kuzingatia usafi wa banda. Ni lazima ajue tabia ya kuku ya kila siku. Kuku mgonjwa unaweza kumtambua kwa kuangalia yafuatayo;
Tabia ya kuku.
  • Kinyesi cha kuku (mabadiliko ya kinyesi).
  • Ulaji wa chakula na unywaji wa maji kama umepungua.
  • Utagaji wa mayai na uimara wa mayai kama vimepungua.
  • Kuku kutochangamka.
Vifo ni dalili ya mwisho.

Kama utaona kuna kuku mgonjwa bandani basi mtenge na wenzie kama unavyowafanyia vifaranga. Ili uweze kuwahudumia peke yao. Wengine ambao hawajaonesha dalili wapewe dawa ya kinga haraka iwezekanavyo kupitia ushauri wa mtaalam wa mifugo aliye karibu.
Chanjo na matibabu yoyote yafuate ushauri wa mtaalam/mtengenezaji wa dawa husika bila kupuuzia ili upate mafanikio. Hii itakuwezesha kupunguza/kuponya magonjwa na kupunguza gharama za matibabu na vifo. Hakikisha kuwa chanjo/tiba zinatoka kwa mtaalam anayejua kutunza chanjo/dawa kwenye ubaridi unaotakiwa kulingana na maagizo ya mtengenezaji.
Mambo yafuatayo yanaweza kusababisha magonjwa au kupunguza uzalishaji hivyo kuleta hasara zisizo za lazima kwa mfugaji.;
  • Kufuga kuku wengi kwenye eneo dogo.
  • Chumba/banda lisilo na hewa na mwanga wa kutosha.
  • Banda kuwa chafu.
  • Vyombo vichache/visivyotesheleza kwaajili ya chakula na maji.
  • Vyombo vichafu vya maji na chakula.
  • Chakula kisicho na viini lishe vya kutosha/kichache.
  • Kubadili ladha ya chakula.
  • Kuchelewa kudhibiti magonjwa ya kuku.
  • Kuchanja/kutibu kuku bila utaratibu/ushauri wa kitaalam.
  • Kutishia kuku wakati wa kuingia bandani/kuwashika/kuwasumbuasumbua.
  • Mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Kufuga kiholela bila kuwachambua.
Chagua njia bora na rahisi inayokufaa kulingana na eneo ulilopo na mahitaji yako pia. Angalia njia itakayokupa faida kwa gharama ndogo.
Chagua kuku wenye uwezo wa kukua haraka, wanaostahimili magonjwa, wanaotaga mayai mengi, wanaoweza kuangua vifaranga wengi na kuwalea.
Chagua jogoo aliye na uzito mzuri na mwenye kucha fupi.
Uwiano wa jogoo kwa majike iwe ni jogoo 1 kwa majike/mitetea 10.
Kuku anayetazamiwa kuatamia mayai anatakiwa asiwe na chawa/viroboto/utitiri.
Kuku ambaye hakidhi sifa za kuwa kuku bora anayefaa kuwa kwenye kundi inafaa aondolewe ili asilishwe kwa hasara awapo bandani.
Minyoo na utitiri nalo ni tatizo linachangia kuku kutokutaga, unashauriwa kumpa kuku dawa za minyoo na utitiri kwa wakati.
Tunashauri kutumia mabanda ya ghorofa kwa ajili ya vifaranga ili kuepukana na bacteria wanatokana maranda kwetu utajionea na ni faida kwako.
MAGONJWA YANAYOSABABISHWA NA VIRUSI
1. Mdondo (Newcastle):
Dalili zake:
kuku kukohoa,kuhema kwa shida,kutokwa na ute mdomoni na puani,hupatwa na kizunguzungu, kuharrisha mharo wa kijani na manjano na hatimaye kuku hufa ghafla. Vifo huweza kufikia asilimia90
2. NDUI YA KUKU: Fowlpox)
Kuku hupatwa na vipele vya mviringo kwenye upanga, (masikio,miguu na sehemu zisizo na manyoya.vifo vichache kwa kuku wakubwa, wadogo huweza kufa nusu ya kundi.CHANJO WIKI YA NANE
(wapewe antibiotic na vitamini) hakuna tiba)
3. MAHEPE (.Marek’s disease)
Kuku kupooza miguu, mabawa na shingo huweza kupinda, mara nyingi huwapata kuku wenye umri wa wiki ya 16 hadi 30.kiasi cha robo ya mitemba wanaweza kufa.
(chanja vifaranga wakiwa na umri wa siku moja)
4. GUMBORO :
vifaranga huharisha mharo mweupe,huhangaikahangaika, hushindwa kuhema, manyoya husimama, hudumaa, hutetemeka na hatimaye hufa.vifo vyaweza kufikia 5% hadi 10%.
(Hakuna tiba wapatiwe chanjo ya gumburo)
5. MAGONJWA YASHAMBULIAYO MFUMO WA HEWA
(Infectious bronchitis, laryngotracheitis or chicken influenza)
upungufu wa mayai kwa kuku wanaotaga,vifaranga hupata matatizo ya kupumua na kupiga chafya na hufa kwa wingi
(huzuiwa kwa chanjo) hakuna tiba.)
6. MAFUA MAKALI YA NDEGE:
kupumua kwa shida, kukohoa na kupiga chafya, sehemu za kikole(kidevu na kishungi) hubadilika na kuwa rangi ya zambarau,kutokwa na machozi,kupinda shingo na kuanza kuzunguka, kuvimba kichwa, kuharisha kinyesi chenye majimaji, rangi ya kijani na baadaye kinyesi cheupe.
(hakuna tiba muone daktari
7. HOMA YA MATUMBO: (Salmonella gallinarum)
ugonjwa huu unaweza kurithiwa kupitia kwenye mayai au kuambukizwa kutokana na kuku wagonjwa, kinyesi, kudonoana, na mazingira machafu,
Kuku huharisha mharo wa kijani, vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu, manyoya husimama.vifo huweza kufikia 50%.
Weka banda katika hali ya usafi,ondoa kuku waliougua,usitumie mayai yenye ugonjwa kuangulia.
8. Pullorum bacillary white diarrhea (bacteria salmonella pullorum)
huathiri zaidi vifaranga(kabla ya umri wa wiki 4) vifaranga hujikusanya pamoja na kutetemeka kama waliopatwa na baridi.huharisha mharo mweupe hamu ya kula hupungua,manyoa hunyea na hupumua kwa taabu.vifo huweza kufikia asilimia 50.
9. kipindupindu cha kuku(Fowl cholera)
kuku kuhara mharo wa rangi ya njano.husinzia na kulegea,hulala kichwa kikining’inia kwenye mabawa.manyoya husimama,kuhema kwa shida,hushindwa kusimama na hatimaye hufa.vifo huweza kufikia asilimia 50
Usafi wa banda(huweza kutibika kwa dawa ya sulfa)
10.Ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa (chronic respiratory)
Kuku kupata mafua, kukohoa kushindwa kupumua, kutokwa na makamasi,vifaranga hudumaa,utagaji hupungua na viungo vya mifupa huweza kuvimba
Tiba: antibiotic hutibu,usafi wa banda.
11. UGONJWA WA KUHARA DAMU:
Kuku huharisha kinyesi kilichochanganyika na damu na mara nyingine damu tupu,hudhoofisha kuku, huteremsha mabawa na hatimaye kuku huweza kufa.
Usafi wa banda,hutibiwa kwa kutumia dawa kama vile Amprolium.salfa na Esb3.Muone daktari.

.......................................................................................................................................................

0 comments:

 
Top