script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




DAWA ZA ASILI ZA MAGONJWA MBALIMBALI ZA KUKU

Madawa ya asili yatokanayo na mimea inayosaidia katika tiba na kinga za maradhi mbalimbali ya kuku.
Sehemu ya mimea yaweza kuwa.
Majani
Magome
Mbegu
Maua
Matunda
Umuhimu wa kutumia tiba zenye asili ya mimea;
Hupatikana kwa urahisi
Ni rahisi kutumia
Gharama nafuu
Zinatibu vizuri
Hazina madhara

BAADHI YA MIMEA INAYOTIBU MARADHI YA KUKU
1. Mwarobaini
Sehemu zitumikazo kwaajili ya tiba ni majani, mizizi na magome.   
Mwarobaini hutibu
magonjwa yafuatayo;
Typhoid
Kuzuia kideri
Kuhara
Mafua
Vidonda

2. Shubiri Mwita (Aloevera)
Aloevera hutimu magonjwa yafuatayo;
Kideri, Mdondo, Mdonde, Chikwemba, Kitonga, Chinoya, Sokota
Typhoid (Homa ya matumbo)
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera)
Chukua majani (3 – 5) makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 – 7. Isitumike tena baada ya masaa 12, mwaga na tengeneza tena nyingine baada ya masaa 12.
3. Matakatang’onyo (Euphorbia)
Matakatang’onyo hutibu au hukinga
Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba)
Ndui
Kuhara damu (Coccidiosis)

4. Mbarika (Nyonyo)
             Hutibu au hukinga
Uvimbe
Weka majani ya mbarika ndani ya maji ya mgomba kasha weka ndani ya jivu la moto, Kisha kanda sehemu yenye uvimbe kwa kutumi majani hayo.

5.   Mlonge (Mlonje)
Hutibu au hukinga
Mafua
Kideri
Kipindupindu cha kuku (Fowl cholera)
Homa ya matumbo
Ini
Ina vitamin A na C
Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili) Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita kumi za maji na uiache kwa masaa 12 hadi 16, Chuja na uwape kuku. Baada ya masaa 12 mwaga na tengeneza nyingine.

6.  Konfrei
Hutibu au hukinga
Vidonda
Majipu
Ina vitamin na madini mengi

7.  Ndulele (Ndungurusi, Makonde, Tura/Ndula)
Hutibu au hukinga
Majani hutibu minyoo
Matunda hutibu vidonda

8.  Papai (Majani)
Hutibu au hukinga
Minyoo
Kuharisha namna yoyote
Chemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi yabakie lita 1, poza kasha chuja husaidia kutibu minyoo.

0 comments:

 
Top