script>" " ".

Get our Android App in Playstore DOWNLOAD HERE!

X




Dawa ya vidonda vinavyotokana na Ndui ya kuku au vidonda vingine vyovyote:
Dalili ya Ndui
_ Kuku hupata vipele vya mviringo kwenye upanga wake wa kichwani, kwenye masikio,miguuni na kwingineko kusikokuwa na manyoya.
》Kuandaa
- Chukua majani ya Shubiri mwitu na kuyachana vipande vidogo vidogo. Vitwange na
pumba kidogo na kuvianika.
- Vikiisha kauka vitwange na kuchekecha upate unga laini.
- Hifadhi unga katika chombo kisafi na kikavu.
》Kutumia
- Safisha vidonda vilivyotokana na ndui au vidonda vyovyote vile na maji ya vugu vugu safi yaliyo na chumvi kiasi.
- Pakaa unga wa Shubiri mwitu katika vidonda vilivyosafishwa.
- Rudia baada ya siku moja. Tumia hivyo hadi vidonda vikauke.
》NAMNA YA PILI YA KUANDAA DAWA HII
Shubiri mwitu  ukikata jani lake huwa linatoka utovu/maji maji ( angalia picha)
Baada ya kusafisha vidonda vya ndui na maji ya vuguvugu yenye chumvi kiasi na wakati huo unavisafisha hakikisha unavibandua.
》 Utachukua jani la shubiri mwitu na kulikata yale maji maji yatakayotoka utayadondoshea kwenye vidonda vya ndui.

0 comments:

 
Top